Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Shukran kiongozi kwa ukumbusho.
Pamoja na ccm kuukana ujamaa na kubariki ubepari hata hivyo ktk dhana zote mbili kuna nidhamu moja wamefafana.
Nidhamu hiyo ni Secularism.
Usekula kwasasa una maana tofauti, lkn asili yake ni ile ile kukanusha kuwepo kwa mungu na hivyo dini kwayo haina maana yyt.
Kwa historia mifumo yote ya utawala ilishikwa na viongozi was dini. Lkn baada ya viongozi was dini kuvimbiwa na madaraka, uongozi ukawa si ule wa kumtegemea mungu. Na baada ya dhiki na mateso ndipo wakajitokeza watu kupinga utawala huo unaitwa unamtangaluza mungu. Ndio ikaja hoja ya usekula.
Kwa uoni wangu historia mpya ya uongozi inapaswa kujengwa uongozi utakao mtanguliza mungu na usekula.
Nadharia hiyo kwa lugha nyepesi huitwa ya Diversity au Serikali jumuishi.
Kwani kwa uhalisia pamoja na tz kujipambanua hadi Leo kuwa haichanganyi mambo ya mungu na siasa. Hata hivyo huchanganywa. Hivyo Usecular umebaki kuwa ni jinamizi la kuwanyima haki baadhi ya dini nchini.
Waznz kwa mfano 98% ni waislam lkn mabinti walio jeshini wananyimwa haki ya kuvaa mavazi ya stara sawa na dini yao. Vazi la stara ni moja ya ibada kwa waislam.
Lkn hizi kwa mznzr mwenyewe haoni shida. Kwasasabu ingawa ni waislam lkn wameathiriwa na ujamaa. Na matokeo yake wanaleta siasa za ubaguzi kama ujamaa wenyewe ulivyo.
Nilikuuliza umeusoma ujamaa wa Ki marx , hujanijibu , nikakuambia CCM Haifuati kabisa umarxism Na umejibu kuwa wanashabihiana. Sasa niambie wanashabihiana katika nini ?
Halafu unaleta mambo ya ZNZ Na wanawake , kwani huelewi Kuwa ZNZ ilivamiwa Na Tanganyika kuanzia 1964. Na Tanganyika imeweka majeshi yake kila kipembe.
Ubaguzi uko wapi zaidi ya kudai Nchi yetu kutoka kwa mvamizi ? Na nyinyi ndio mnaotuulia ndugu zetu kuanzia nyinyi waislamu Ma Alhaaji Mahita , Mwinyi Na wengine
Yaani mapenzi yenu kwetu ni kutuuwa, kuwanajisi mama Na dada zetu , kututia vilema Na kutuwekea vibaraka viongozi Tu halafu unalalamika tunawabagua?