Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Umekutana na mchumba, anakupeleka nyumbani unakuta ni nyumba ya mbavu za mbwa. Wazazi waliwekeza hela zao nyingi katika elimu ya binti yao, amefanikiwa kumaliza kidato cha nne na ana certificate ya chuo lakini haja pata ajira.
Wakwe ni wakarimu na ni waungwana. Unaamua kupeleka barua ya posa na ugeni wa kujitambulisha. Baada ya hapo harusi mnaifanya mjini kwakua ni centre kwa ndugu wa mume, wa mke na marafiki.
Umeshapiga hesabu nyumba simple ya wakwe itagharimu milioni 25-30. Unaongea na baba mkwe akuonyeshe eneo ambalo angependa nyumba yake isimame. Unapeleka Lori la matofali na baada ya miezi sita nyumba inafanyiwa finishing.
Si hayo tu, umepigiwa simu kuna msiba ukweni. Unamtaarifu mke wako na mnaweka mafuta katika IST yenu. Unanunua kilo 30 za sukari na debe la mafuta ya korie. Ukifika pale unaonyeshwa sehemu ya kupark IST tena ni mbele kabisa ya nyumba kwa usalama. Ukimsalimia baba mkwe unamuomba muende kando na unamkabidhi laki mbili zimsaidie kunyoosha mambo katika msiba.
Huyu baba atakuombea dua jema maisha yake yote na hata mke wako akipeleka malalamiko juu ya mchepuko yako hata kaa asikilizwe.