Ukweni ni kuzuri ukiwa na uwezo wa kuwabadilishia maisha yao kuwa bora

Ukweni ni kuzuri ukiwa na uwezo wa kuwabadilishia maisha yao kuwa bora

Imetokea baba mkwe anafariki rafiki zako wanakusindikiza nyumba ni mbavu za mbwa hata jeneza halipiti.
Tatizo liko wapi Sasa hao marafiki Wana takiwa kujua Kuwa huo sio wajibu wangu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Yaani nijiingize ktk gharama zisizo nihusu kisa kwaajili ya kufikiria marafiki wata nionaje !?

You must be kidding
 
View attachment 2326476
Umekutana na mchumba, anakupeleka nyumbani unakuta ni nyumba ya mbavu za mbwa. Wazazi waliwekeza hela zao nyingi katika elimu ya binti yao, amefanikiwa kumaliza kidato cha nne na ana certificate ya chuo lakini haja pata ajira.

Wakwe ni wakarimu na ni waungwana. Unaamua kupeleka barua ya posa na ugeni wa kujitambulisha. Baada ya hapo harusi mnaifanya mjini kwakua ni centre kwa ndugu wa mume, wa mke na marafiki.

Umeshapiga hesabu nyumba simple ya wakwe itagharimu milioni 25-30. Unaongea na baba mkwe akuonyeshe eneo ambalo angependa nyumba yake isimame. Unapeleka Lori la matofali na baada ya miezi sita nyumba inafanyiwa finishing.

Si hayo tu, umepigiwa simu kuna msiba ukweni. Unamtaarifu mke wako na mnaweka mafuta katika IST yenu. Unanunua kilo 30 za sukari na debe la mafuta ya korie. Ukifika pale unaonyeshwa sehemu ya kupark IST tena ni mbele kabisa ya nyumba kwa usalama. Ukimsalimia baba mkwe unamuomba muende kando na unamkabidhi laki mbili zimsaidie kunyoosha mambo katika msiba.

Huyu baba atakuombea dua jema maisha yake yote na hata mke wako akipeleka malalamiko juu ya mchepuko yako hata kaa asikilizwe.
Mkuu hapo sio Lindi liwale kweli, hiyo ndio sitaili yetu ya kujenga Nyumba huku
 
Tatizo liko wapi Sasa hao marafiki Wana takiwa kujua Kuwa huo sio wajibu wangu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Yaani nijiingize ktk gharama zisizo nihusu kisa kwaajili ya kufikiria marafiki wata nionaje !?

You must be kidding
Kwa mawazo haya hatutakaa tutokomeze mabavu za mbwa Tanzania.
 
Kwenu kuna afadhali kidogo, Mzee alipopata pension yake ya uwalimu alimalizia pagala lake na sasa hivi wanaishi kwenye nyumba bora.
Wapi ni sahihi kuanza kujenga kati ya kwenu na ukweni
Ikiwa pande zote zinauhitaji?
 
Wakwe zako ni wazazi wako pia ni vizuri kuwaboreshea pia maisha yao kama hawajiwezi.
Kwann michepuko kama ujamaliza ujana kwann uingie kwenye ndoa
 
Binadamu hana shukurani. Hata umfanyie nini.

Utafanya mengi mazuri, Ukikosea moja. Umefuta yote mazuri.

Be real
Wajibu wako ni kutenda wema na sio kugoja shukrani.
 
Nihitimishe kwa kusema vijana tutafute Hela tena hela nyingi sana
 
Huo upumbavu kwangu never bora nijengee baba na mama watanibless hizo shida zao kama mpaka wanazeeka wameshindwa kuzitatua ts over, ujana wangu ni muhimu kwa future yangu, nitasaidia mengine but not to that extent hata wao silently wataniona boya. Huko ni kutafuta huruma isiyo na lazima meanwhile life has no mercy.
Ni mtazamo wako tu.
Kwani kwa waganga na mitume mbona mnachunwa pesa nyingi Sana zaidi unapata nini cha ziada.Wakwe ni babu na bibi wa watoto wako labda tu kuepuka hayo kaoe kwa matajiri.
Wanaweza wakawa ni masikini lakini Wana good heart.
 
Kwenu umeshamaliza kufanya haya au huna wazazi
Yaani ujenge kwako na familia yako, ujenge Kwa mkeo, ujenge kwenu.

Bado usomeshe wanao, wadogo zako, ndugu wa mkeo.

Bado usaidie ndugu zako, wazazi wako,

Bado michango ya jamii.

Hapo kipato chako take home 400,000 mwalimu wa Grade A na ajira umepata ukiwa na Miaka 35!!

Halafu utarajia kutoka kwenye umasikini?????

😄😄
 
Ukitoka Dar tu unaanza kukutana na mbavu za mbwa. Sehemu ambayo hizi nyumba zimepotea ni Kilimanjaro.
Acha uwongo.

Hizo nyumba zipo sana.

Ingawa huku wanajengea Mbao ( Kwa zamani ) na nyingine wanatumia Tope lililochanganywa na nyasi.
 
Duuuh kujenga ukweni tena, mbona tunaanza kupotoshana kimya kimya
 
Yaani ujenge kwako na familia yako, ujenge Kwa mkeo, ujenge kwenu.

Bado usomeshe wanao, wadogo zako, ndugu wa mkeo.

Bado usaidie ndugu zako, wazazi wako,

Bado michango ya jamii.

Hapo kipato chako take home 400,000 mwalimu wa Grade A na ajira umepata ukiwa na Miaka 35!!

Halafu utarajia kutoka kwenye umasikini?????

😄😄
Anatupotosha huyo, huo mpango wakujengea wakwe umeanza lini tena
 
Ni mtazamo wako tu.
Kwani kwa waganga na mitume mbona mnachunwa pesa nyingi Sana zaidi unapata nini cha ziada.Wakwe ni babu na bibi wa watoto wako labda tu kuepuka hayo kaoe kwa matajiri.
Wanaweza wakawa ni masikini lakini Wana good heart.
No research no right to speak, how sure kwmb mimi ni mwendaji kwa waganga na wakwenda huko kwa wachungaji and uko sawa kwamb ni mtazamo wangu and never kujenga ukweni ntayafanya mengne yote ila si kujenga kama hawatakuwa thankfull kw hivyo ntakavyofanya basi ni jibu tosha na sababu yakutojengewa.
 
Ipo tofauti ya kujenga ukweni na kuwajengea babu na bibi wa watoto wako upande kwa mama yao.
Unaishi kwenye ghorofa town unajisikiaje kupeleka watoto wako wakawasalimie babu na bibi yao wanaokaa nyumba mbavu za mbwa huku ukibadili magari makali.Hali ukiwapa milioni 3 tu kijijini wanajenga nyumba fresh tu
 
Back
Top Bottom