DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
View attachment 3140820Mkuu kinachozungumzwa humu ndani na kilichopo mtaani ni tofauti sana nakuambia hivyo kwasababu mimi nipo kijijijini na ninalima mazao mchanganyiko na pia ninanunua ,Na mazao ninayolima kwaajili ya kupata pesa ni kunde,korosho,njugu,karanga na ufuta na amini nakuambia kuwa hayo mazao yote nikiuza huwa napata sio chini ya milion 15 na huu ni mwaka wa 5 napata wastani wa hicho kiasi.....na hizo kilo nilizopima sio kwamba korosho zimekwisha shambani kwasababu nategemea kupata mara 2 ya hizo kilo nilizopima awali,,,nawashauri vijana humu ndani tusipotoshane nakumbuka kuna mtu alileta mada ya kuhusu kilimo cha mpunga chakushangaza humu ndani waliponda sana mara oooh kilimo cha kutegemea mvua hakilipi kabisa mara blahblah kibao wakati ukienda majimoto kule unakuta watu wanatajirika kwa kilimo cha mpunga chakutegemea hizihizi mvua
Endeleeni kupotosha huku kazi