LGE2024 Ulaghai wa bei ya korosho na kiki za kisiasa za CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

LGE2024 Ulaghai wa bei ya korosho na kiki za kisiasa za CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sawa. Nafikiri kwa ulimwengu huu wa teknologia, ni wakati sasa wakulima wapate taarifa kupitia simu zao kwa njia ya sms mara tu mnunuzi anapopatikana na kufanya malipo. Ni mawazo yangu.
Mwaka huu mfumo kidogo umeanza kuboreshwa nadhani mpaka misimu ijayo mambo yatakuwa hayo
 
Bei ya 4k ilikua ni bei ya danganya toto,kiki za kisiasa na ni maelekezo ya wanasiasa kwa wafanyabiashara.

Hapo ndio ujue kuna ushenzi mwingi sana unafanyika kwenye bei ya hili zao.
Kwahiyo bei halisi ilikuwa shiling ngapi?
 
Bei inategemeana na ushindani wa soko.... je unafikiri siasa inaharibu?
 
Kwahiyo bei halisi ilikuwa shiling ngapi?
Kama zao linaweza ongeza bei kipindi cha uchaguzi kutoka kwa maagizo ya wanasiasa,jiulize wanacheza na bei za mazao mangapi ukiachilia korosho.

Tazama tu bei ya korosho ghafi katika soko la kimataifa ndio utajua,umasikini wa wakulima hapa bongo sio bahati mbaya bali ni kwasababu ya uongozi mbovu na wanasiasa wabinafsi.
 
Pongezi kwa serikali mwaka huu bei imefika elf 3+ ukilinganisha na mwaka jana ya elf 2.

Nyie madalali blabla zenu hukuhuku mitandaoni. Wananchi wameanza kupokea pesa zao na wanafurahia jitihada za serikali
Wewe kweli ni dustbin maana umebeba takataka kichwani mwako [emoji867]
 
Kama zao linaweza ongeza bei kipindi cha uchaguzi kutoka kwa maagizo ya wanasiasa,jiulize wanacheza na bei za mazao mangapi ukiachilia korosho.

Tazama tu bei ya korosho ghafi katika soko la kimataifa ndio utajua,umasikini wa wakulima hapa bongo sio bahati mbaya bali ni kwasababu ya uongozi mbovu na wanasiasa wabinafsi.
Sawa sikatai hayo uliyoyaandika ila swali langu ni hivi umedai bei ya 4000 sio halisi ndio nikakuuliza kwahiyo bei ya kweli ni ipi?
 
Mkuu kinachozungumzwa humu ndani na kilichopo mtaani ni tofauti sana nakuambia hivyo kwasababu mimi nipo kijijijini na ninalima mazao mchanganyiko na pia ninanunua ,Na mazao ninayolima kwaajili ya kupata pesa ni kunde,korosho,njugu,karanga na ufuta na amini nakuambia kuwa hayo mazao yote nikiuza huwa napata sio chini ya milion 15 na huu ni mwaka wa 5 napata wastani wa hicho kiasi.....na hizo kilo nilizopima sio kwamba korosho zimekwisha shambani kwasababu nategemea kupata mara 2 ya hizo kilo nilizopima awali,,,nawashauri vijana humu ndani tusipotoshane nakumbuka kuna mtu alileta mada ya kuhusu kilimo cha mpunga chakushangaza humu ndani waliponda sana mara oooh kilimo cha kutegemea mvua hakilipi kabisa mara blahblah kibao wakati ukienda majimoto kule unakuta watu wanatajirika kwa kilimo cha mpunga chakutegemea hizihizi mvua
Mbona umejikita sana kuelezea shughuli zako binafsi kuliko kupinga hoja Kwa hoja?
 
Wewe ni mpotoshaji. Kinachochangia korosho kushuka bei ni supply kuwa kubwa. Mnada wa pili wa korosho chama Kikuyu cha ushirika cha Newala na Tandahimba (TANECU) kiliuza tani 20,000 ni zaidi ya uzalishaji wa wilaya ya Newala kwa mwaka mzima.

Mnada wa kwanza hadi wa tatu bodi ya korosho imesimamia kuuza korosho tani 100,000 plus, kiasi ambacho ni zaidi ya nusu ya makusanyo yote ya minada 14 ya msimu uliopita. Unaweza kuona ni jinsi gani uzalishaji umekuwa mkubwa. Wamakonde wamekausha benki kuu tawi la mtwara na benki zote hazina cash tangu Jana.

Kuhusiana na suala la korosho kutokusafiri , suala ni lile lile kuwa supply ni kubwa kuliko vyombo vya usafiri vilivyopo. Lakini kikubwa ni miundombinu hasa maghala makuu ya mnada, yamezidiwa uwezo. Makuli wa kisukuma pale Agrofocus Newala wamekimbia kazi ya kushusha na kupakia.

Kama munataka kazi njoo mtwara, na sio humu jamii forum munakowapotosha watu. Maghala yamejaa hamna sehemu ya kushusha korosho. Makuli wamechoka kazi. Hivyo kuna foleni kubwa ya kusubiri kushusha mzigo ili gari zirudi shamba.
Kwahyo wewe kuli upo newala au tandahimba?
 
Mbona umejikita sana kuelezea shughuli zako binafsi kuliko kupinga hoja Kwa hoja?
Lengo langu la kuandika hayo ni kwamba ni kutimiza matakwa ya uanzishwaji wa jamii forum ambayo ni kuelimishana na sio kupotoshana kama afanyavyo huyo mtoa mada na wenzie wengi....humu jukwaani kuna watu kazi yao ni kukatisha watu tamaa na kuwatisha hususani kwenye upande wa kilimo jambo ambalo ni hatari sana kwa vijana wa humu ambao wanataka waingie kwenye kilimo kwa mara ya kwanza,Na unaposema kuwa eti nipinge hoja hapo kwa akili yako unaiona hoja au uzushi ?jiulize mbona nilipoandika mimi tu hajatokea tena huyo mtoa mada?
 
Wewe kweli ni dustbin maana umebeba takataka kichwani mwako [emoji867]
IMG-20241102-WA0016.jpg

Chukua takakata nyingine hiyo
 
Nyie wakulima ndiyo hamjui. Jengeni maghala kupitia vyama vyenu vya ushirika, myasajili hayo maghala kupitia bodi ya stakabadhi ghalani. Na mnada ufanyike huko. Ila huu utaratibu wa kupeleka sijui mtakesha
Hili nalo wazo. Ila kuna maeneo ni korofi maghala yake yatakuwa hayafikiki kiurahisi, kwa hiyo wanunuzi watasita kununua maeneo hayo. Sasa mjini walau kunafikika.
 
Sawa. Nafikiri kwa ulimwengu huu wa teknologia, ni wakati sasa wakulima wapate taarifa kupitia simu zao kwa njia ya sms mara tu mnunuzi anapopatikana na kufanya malipo. Ni mawazo yangu.
Ndio tumeanza hiyo hatua, kuna kitu kinaitwa kilimo ujazo, Bashe najitahidi, mwaka huu tumeanza hatua za awali, msimu ujao baada ya kupitia changamoto za msimu huu, tutaenda full. Tumeshasajili tsarina za wakulima wa kila Amcos, wapo kwenye system sasa. Akipima mzigo wake anaupata SMS, mwakani atapata SMS punde mzigo ukiuzwa
 
Mnada wa kwanza wa korosho uliofanyika 11/10/2024 ulifunguliwa kwa bei ya TSh 4150/= kwa kilo moja ya korosho. Kwenye mnada huu kulikuwa na tani chache sana za korosho. Ukafuata mnada wa pili ambapo bei ilishuka mpk kufikia TSh 3750/=, napo pia kulikuwa na tani chache sana za korosho. Bei imeendelea kushuka na sasa imefikia TSh 3400/= ndani ya mwezi October. Na kumekuwa na janja ya kihuni ya kukwepa kubeba korosho za wakulima kupeleka kwenye ghala kuu ili kusubiri bei ishuke halafu korosho za wakulima zinunuliwe kwa bei ndogo baadaye.

Mavuno makubwa ya korosho yatafanyika mwezi huu wa November, ambapo ndipo wakulima wengi watauza korosho zao.
Kwa inavyoelekea bei ya korosho itakuwa TSh 2000/= (bei isiyofaa na inayomuumiza mkulima).

Kwahiyo bei ya TSh 4150/= ilikuwa ni danganya toto iliyovalishwa boksa ya kiki za kisiasa iliyolenga kuisaidia ccm kupiga kampeni kwenye chaguzi za serikali za mitaa.
we chadema umeshindwa sisi wakulima wa korosho sasa hivi tunaongeza wake tu kwa furaha tuliyonayo kwa mama ssh maana tuna pesa za kutosha wewe endelea kupiga porojo zako za kipinzani sisi tunasherehekea mavuno na pesa nyngiiiiii
 
Hapo kwenye uwazi wa minada mpo sawa. Swali langu ni; mkulima ambaye sidhani kama anahudhuria kwenye mnada/minada, anapataje taarifa kwamba, leo mnada umefanyika na korosho zako kilo kiasi fulani zimeuzwa kwa bei hii?
Ukiwa na simu janja unaweza kufuatilia mbada katika link ya tmx. Lakini mfumo wa kilimo ujazo umeandaliwa mwaka Jana tumeanza kuutumia mwaka huu kwa hatua za awali. Tunapokea korosho kwa mfumo, tunasafirisha kwa mfumo na tunauza kwa mfumo. Mwakani tutalipa kwa mfumo. Mkulima atapokea SMS punde tu mzigo ukiuzwa. Kwa sasa anaupata SMS muda wa kupima mzigo wake.
 
Hapo kwenye uwazi wa minada mpo sawa. Swali langu ni; mkulima ambaye sidhani kama anahudhuria kwenye mnada/minada, anapataje taarifa kwamba, leo mnada umefanyika na korosho zako kilo kiasi fulani zimeuzwa kwa bei hii?
Kinachofanyika ni kwamba korosho zote zilizofika ghala kuu na kupimwa uzito hununuliwa kwa bei iliyopitishwa ktk mnada huo ( bei huwa moja tu).

Na kwa kuwa mkulima anakuwa tayari snafahamu idadi ya kilo zake za korosho, hivyo automatically atajuwa na kiasi cha mapato yake.
 
Sawa sikatai hayo uliyoyaandika ila swali langu ni hivi umedai bei ya 4000 sio halisi ndio nikakuuliza kwahiyo bei ya kweli ni ipi?
Bei halisi itakuwa 2k, kwasabb hiyo bei ya 4k imetolewa wakati zao bado korosho hazijafikia kilele cha mavuno. Ni zile korosho zinazopatikana kwa kuokoto moja moja kwenye miti.

Sasa kila mnada unaofuata bei inashuka. Hivi iko 2.9k na ndiyo mavuno ya korosho yameanza kuchanganya. Sijui unaelewa ?? CCM washenzi sana
 
Kama zao linaweza ongeza bei kipindi cha uchaguzi kutoka kwa maagizo ya wanasiasa,jiulize wanacheza na bei za mazao mangapi ukiachilia korosho.

Tazama tu bei ya korosho ghafi katika soko la kimataifa ndio utajua,umasikini wa wakulima hapa bongo sio bahati mbaya bali ni kwasababu ya uongozi mbovu na wanasiasa wabinafsi.
Kwenye Uzi wako kuna ukweli kwa kuwalaumu upande wa wenye maulana, lakini pia lipo suala la elimu kwa upande wa wakulima. Walaji wakuu wa korosho ya Tanzania ni America na Ulaya na bei ya korosho huko ni kubwa, hasa korosho ya Tanzania inayosadikika kuwa ndio Bora zaidi duniani. Lakini mataifa hayo ya magharibi hawanunui korosho direct kutoka Tanzania, wananunulia India, na Vietnam, na sasa China. Hii inatokana na hatujawa wasuri kwenye kuziandaa korosho setup na zikakidhi international standard zikaliwa huko magharibi. Storage yetu ni very poor, kiasi kwamba wapo jamii ya funza kwenye korosho wakifika Ulaya hiyo korosho inakuwa rejected. Wakulima korosho shambani hawazi grade, wanatia tu mbovu na mzuri. Pia wakulima hawazikaushi korosho vizuri. Kwahiyo manunuzi anapokuja kununua anatoa bei nusu ya bei halisi, kwa kuamini kuwa mzigo anaoununua, mzigo halisi utakao kuwa Bora sokoni ni nusu yake. Yaani gari ya tan 20. Korosho itakayo kuwa na u Bora wake mpaka muda wa kubanguliwa kule India na Vietnam ni tani 10. Hivyo kumi nyingine ni hasara. Kwahiyo usitegemee kwa mfumo huo mfanya biashara atoe bei mzuri. Kwahiyo ukitazama bei ya korosho soko la dunia ukafananisha na bei ya korosho Tanzania kisha uka draw conclusion itakuwa umekosea. Tuna safari ndefu ya kwenda ili kulifikia soko la dunia Sisi wenyewe. Korosho ya Tanzania haiendi soko la dunia na wa Tanzania wenyewe. Inaenda India, Vietnam na China wanaiboresha na kupeleka soko la dunia kama zinatoka kwenye mataifa Yao. Wa magharibi hawaagizi korosho Tanzania Bali wanaagiza india, Vietnam na China kwa sasa
 
Wewe ni mpotoshaji. Kinachochangia korosho kushuka bei ni supply kuwa kubwa. Mnada wa pili wa korosho chama Kikuyu cha ushirika cha Newala na Tandahimba (TANECU) kiliuza tani 20,000 ni zaidi ya uzalishaji wa wilaya ya Newala kwa mwaka mzima.

Mnada wa kwanza hadi wa tatu bodi ya korosho imesimamia kuuza korosho tani 100,000 plus, kiasi ambacho ni zaidi ya nusu ya makusanyo yote ya minada 14 ya msimu uliopita. Unaweza kuona ni jinsi gani uzalishaji umekuwa mkubwa. Wamakonde wamekausha benki kuu tawi la mtwara na benki zote hazina cash tangu Jana.

Kuhusiana na suala la korosho kutokusafiri , suala ni lile lile kuwa supply ni kubwa kuliko vyombo vya usafiri vilivyopo. Lakini kikubwa ni miundombinu hasa maghala makuu ya mnada, yamezidiwa uwezo. Makuli wa kisukuma pale Agrofocus Newala wamekimbia kazi ya kushusha na kupakia.

Kama munataka kazi njoo mtwara, na sio humu jamii forum munakowapotosha watu. Maghala yamejaa hamna sehemu ya kushusha korosho. Makuli wamechoka kazi. Hivyo kuna foleni kubwa ya kusubiri kushusha mzigo ili gari zirudi shamba.
Shida hizi ziko kote,zao ambalo halina kelele ni maharage,kiukweli korosho ni zao poa,kwani wale Wazee wa ufipa hata kutafuta soko hawawezi,wao kazi yao kulialia,kwanini Wazee wa ufipa kazi yao michango na makesi yasiyoisha.
 
Back
Top Bottom