LGE2024 Ulaghai wa bei ya korosho na kiki za kisiasa za CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
View attachment 3140820
Endeleeni kupotosha huku kazi
 
Sometimes Tanzania ya mtandaoni inachanganya
Ukiwasikiliza sana wazee wa mtandaoni hautafanya lolote lile kwasababu kila kitu utaona hakilipi....kuna mdau aliwahi kupost humu kuwa kilimo cha tumbaku kinalipa sana chakushangaza asilimia 80% ya wachangiaji walimpopoa mno mtoa mada kuwa tumbaku inaleta umaskini hailipi wala nini ila mimi nina ndugu zangu wengi wamejenga nyumba na kununua usafiri pamoja na kuongeza kununua mashamba kutokana na hiyohiyo tumbaku
 
Mimi ninachoshukuru nilipima kilo 2360 na nikalipwa hiyo 4000
Utaratibu wa malipo kwa mkulima baada ya mauzo ukoje? Mkulima anapata taarifa ya mauzo ya korosho zake kupitia njia ipi na muda gani tangu ziuzwe kwenye mnada ili kuanza kushangilia bingo?
 
Nyie wakulima ndiyo hamjui. Jengeni maghala kupitia vyama vyenu vya ushirika, myasajili hayo maghala kupitia bodi ya stakabadhi ghalani. Na mnada ufanyike huko. Ila huu utaratibu wa kupeleka sijui mtakesha
 
Utaratibu wa malipo kwa mkulima baada ya mauzo ukoje? Mkulima anapata taarifa ya mauzo ya korosho zake kupitia njia ipi na muda gani tangu ziuzwe kwenye mnada ili kuanza kushangilia bingo?
Utaratibu ni kwamba mnada ukishafanyika hatua inayofuata ni mkulima kuingiziwa pesa kwenye akaunti yake ya bank na huwa haizidi wiki kutoka siku ya mnada hadi kutiliwa pesa kwenye akaunti...mkulima huwa anapata taarifa ya mauzo kwasababu mnada huwa unafanyika mbele ya wakulima wenyewe huwa watu wa chama cha ushirika hutoa taarifa mapema kuwa mnada ujao tutafanyia kijiji au sehemu fulani kwahiyo wananchi munaombwa mufike ili muulizwe kama munaikubali bei ambayo makampuni yaliyoomba kununua korosho yametaja,kwasababu watu wa chama watawaambia wakulima waliokusanyika hapo kuwa tumepokea maombi ya kampuni fulani na fulani na fulani kuwa wanataka korosho kwa bei fulani kwahiyo muna uwezo wa kukataa au kukubali hiyo bei kwenye huo mnada
 
Utaratibu wa malipo kwa mkulima baada ya mauzo ukoje? Mkulima anapata taarifa ya mauzo ya korosho zake kupitia njia ipi na muda gani tangu ziuzwe kwenye mnada ili kuanza kushangilia bingo?
Mnada uko live kupitia screen kubwa ya tmx, bei zinaonekana pale namna wanaposhindana hadi kupata real buyers. Then alieshinda anapewa 48 working hours awe America. Mara pengi mnada ukiwa ijumaa, malipo tunafanya alhamisi au ijumaa inayofuata. Mimi ni katibu wa Amcos.
 
Unajisikiaje kupotosha watu kwa mgongo wa siasa
 
Bei ya 4k ilikua ni bei ya danganya toto,kiki za kisiasa na ni maelekezo ya wanasiasa kwa wafanyabiashara.

Hapo ndio ujue kuna ushenzi mwingi sana unafanyika kwenye bei ya hili zao.
 
Hapo kwenye uwazi wa minada mpo sawa. Swali langu ni; mkulima ambaye sidhani kama anahudhuria kwenye mnada/minada, anapataje taarifa kwamba, leo mnada umefanyika na korosho zako kilo kiasi fulani zimeuzwa kwa bei hii?
 
Sawa. Nafikiri kwa ulimwengu huu wa teknologia, ni wakati sasa wakulima wapate taarifa kupitia simu zao kwa njia ya sms mara tu mnunuzi anapopatikana na kufanya malipo. Ni mawazo yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…