LGE2024 Ulaghai wa bei ya korosho na kiki za kisiasa za CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sawa. Nafikiri kwa ulimwengu huu wa teknologia, ni wakati sasa wakulima wapate taarifa kupitia simu zao kwa njia ya sms mara tu mnunuzi anapopatikana na kufanya malipo. Ni mawazo yangu.
Mwaka huu mfumo kidogo umeanza kuboreshwa nadhani mpaka misimu ijayo mambo yatakuwa hayo
 
Bei ya 4k ilikua ni bei ya danganya toto,kiki za kisiasa na ni maelekezo ya wanasiasa kwa wafanyabiashara.

Hapo ndio ujue kuna ushenzi mwingi sana unafanyika kwenye bei ya hili zao.
Kwahiyo bei halisi ilikuwa shiling ngapi?
 
Bei inategemeana na ushindani wa soko.... je unafikiri siasa inaharibu?
 
Kwahiyo bei halisi ilikuwa shiling ngapi?
Kama zao linaweza ongeza bei kipindi cha uchaguzi kutoka kwa maagizo ya wanasiasa,jiulize wanacheza na bei za mazao mangapi ukiachilia korosho.

Tazama tu bei ya korosho ghafi katika soko la kimataifa ndio utajua,umasikini wa wakulima hapa bongo sio bahati mbaya bali ni kwasababu ya uongozi mbovu na wanasiasa wabinafsi.
 
Pongezi kwa serikali mwaka huu bei imefika elf 3+ ukilinganisha na mwaka jana ya elf 2.

Nyie madalali blabla zenu hukuhuku mitandaoni. Wananchi wameanza kupokea pesa zao na wanafurahia jitihada za serikali
Wewe kweli ni dustbin maana umebeba takataka kichwani mwako [emoji867]
 
Sawa sikatai hayo uliyoyaandika ila swali langu ni hivi umedai bei ya 4000 sio halisi ndio nikakuuliza kwahiyo bei ya kweli ni ipi?
 
Mbona umejikita sana kuelezea shughuli zako binafsi kuliko kupinga hoja Kwa hoja?
 
Kwahyo wewe kuli upo newala au tandahimba?
 
Mbona umejikita sana kuelezea shughuli zako binafsi kuliko kupinga hoja Kwa hoja?
Lengo langu la kuandika hayo ni kwamba ni kutimiza matakwa ya uanzishwaji wa jamii forum ambayo ni kuelimishana na sio kupotoshana kama afanyavyo huyo mtoa mada na wenzie wengi....humu jukwaani kuna watu kazi yao ni kukatisha watu tamaa na kuwatisha hususani kwenye upande wa kilimo jambo ambalo ni hatari sana kwa vijana wa humu ambao wanataka waingie kwenye kilimo kwa mara ya kwanza,Na unaposema kuwa eti nipinge hoja hapo kwa akili yako unaiona hoja au uzushi ?jiulize mbona nilipoandika mimi tu hajatokea tena huyo mtoa mada?
 
Nyie wakulima ndiyo hamjui. Jengeni maghala kupitia vyama vyenu vya ushirika, myasajili hayo maghala kupitia bodi ya stakabadhi ghalani. Na mnada ufanyike huko. Ila huu utaratibu wa kupeleka sijui mtakesha
Hili nalo wazo. Ila kuna maeneo ni korofi maghala yake yatakuwa hayafikiki kiurahisi, kwa hiyo wanunuzi watasita kununua maeneo hayo. Sasa mjini walau kunafikika.
 
Sawa. Nafikiri kwa ulimwengu huu wa teknologia, ni wakati sasa wakulima wapate taarifa kupitia simu zao kwa njia ya sms mara tu mnunuzi anapopatikana na kufanya malipo. Ni mawazo yangu.
Ndio tumeanza hiyo hatua, kuna kitu kinaitwa kilimo ujazo, Bashe najitahidi, mwaka huu tumeanza hatua za awali, msimu ujao baada ya kupitia changamoto za msimu huu, tutaenda full. Tumeshasajili tsarina za wakulima wa kila Amcos, wapo kwenye system sasa. Akipima mzigo wake anaupata SMS, mwakani atapata SMS punde mzigo ukiuzwa
 
we chadema umeshindwa sisi wakulima wa korosho sasa hivi tunaongeza wake tu kwa furaha tuliyonayo kwa mama ssh maana tuna pesa za kutosha wewe endelea kupiga porojo zako za kipinzani sisi tunasherehekea mavuno na pesa nyngiiiiii
 
Hapo kwenye uwazi wa minada mpo sawa. Swali langu ni; mkulima ambaye sidhani kama anahudhuria kwenye mnada/minada, anapataje taarifa kwamba, leo mnada umefanyika na korosho zako kilo kiasi fulani zimeuzwa kwa bei hii?
Ukiwa na simu janja unaweza kufuatilia mbada katika link ya tmx. Lakini mfumo wa kilimo ujazo umeandaliwa mwaka Jana tumeanza kuutumia mwaka huu kwa hatua za awali. Tunapokea korosho kwa mfumo, tunasafirisha kwa mfumo na tunauza kwa mfumo. Mwakani tutalipa kwa mfumo. Mkulima atapokea SMS punde tu mzigo ukiuzwa. Kwa sasa anaupata SMS muda wa kupima mzigo wake.
 
Hapo kwenye uwazi wa minada mpo sawa. Swali langu ni; mkulima ambaye sidhani kama anahudhuria kwenye mnada/minada, anapataje taarifa kwamba, leo mnada umefanyika na korosho zako kilo kiasi fulani zimeuzwa kwa bei hii?
Kinachofanyika ni kwamba korosho zote zilizofika ghala kuu na kupimwa uzito hununuliwa kwa bei iliyopitishwa ktk mnada huo ( bei huwa moja tu).

Na kwa kuwa mkulima anakuwa tayari snafahamu idadi ya kilo zake za korosho, hivyo automatically atajuwa na kiasi cha mapato yake.
 
Sawa sikatai hayo uliyoyaandika ila swali langu ni hivi umedai bei ya 4000 sio halisi ndio nikakuuliza kwahiyo bei ya kweli ni ipi?
Bei halisi itakuwa 2k, kwasabb hiyo bei ya 4k imetolewa wakati zao bado korosho hazijafikia kilele cha mavuno. Ni zile korosho zinazopatikana kwa kuokoto moja moja kwenye miti.

Sasa kila mnada unaofuata bei inashuka. Hivi iko 2.9k na ndiyo mavuno ya korosho yameanza kuchanganya. Sijui unaelewa ?? CCM washenzi sana
 
Kwenye Uzi wako kuna ukweli kwa kuwalaumu upande wa wenye maulana, lakini pia lipo suala la elimu kwa upande wa wakulima. Walaji wakuu wa korosho ya Tanzania ni America na Ulaya na bei ya korosho huko ni kubwa, hasa korosho ya Tanzania inayosadikika kuwa ndio Bora zaidi duniani. Lakini mataifa hayo ya magharibi hawanunui korosho direct kutoka Tanzania, wananunulia India, na Vietnam, na sasa China. Hii inatokana na hatujawa wasuri kwenye kuziandaa korosho setup na zikakidhi international standard zikaliwa huko magharibi. Storage yetu ni very poor, kiasi kwamba wapo jamii ya funza kwenye korosho wakifika Ulaya hiyo korosho inakuwa rejected. Wakulima korosho shambani hawazi grade, wanatia tu mbovu na mzuri. Pia wakulima hawazikaushi korosho vizuri. Kwahiyo manunuzi anapokuja kununua anatoa bei nusu ya bei halisi, kwa kuamini kuwa mzigo anaoununua, mzigo halisi utakao kuwa Bora sokoni ni nusu yake. Yaani gari ya tan 20. Korosho itakayo kuwa na u Bora wake mpaka muda wa kubanguliwa kule India na Vietnam ni tani 10. Hivyo kumi nyingine ni hasara. Kwahiyo usitegemee kwa mfumo huo mfanya biashara atoe bei mzuri. Kwahiyo ukitazama bei ya korosho soko la dunia ukafananisha na bei ya korosho Tanzania kisha uka draw conclusion itakuwa umekosea. Tuna safari ndefu ya kwenda ili kulifikia soko la dunia Sisi wenyewe. Korosho ya Tanzania haiendi soko la dunia na wa Tanzania wenyewe. Inaenda India, Vietnam na China wanaiboresha na kupeleka soko la dunia kama zinatoka kwenye mataifa Yao. Wa magharibi hawaagizi korosho Tanzania Bali wanaagiza india, Vietnam na China kwa sasa
 
Shida hizi ziko kote,zao ambalo halina kelele ni maharage,kiukweli korosho ni zao poa,kwani wale Wazee wa ufipa hata kutafuta soko hawawezi,wao kazi yao kulialia,kwanini Wazee wa ufipa kazi yao michango na makesi yasiyoisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…