Ulaji wa Panya mikoa ya Kusini: Safari yangu ya siku 37 ilivyonifungua mambo mengi

Chezea atoro wewe
 
Panya wa porini wana proteins nyingi sana. Ni nyama nzuri tu kwa matumizi ya binadamu kama ilivyo ndezi.

Ni utamaduni hasa wa wamakua kutoka Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara. Panya ni watamu sana.

Ahsante.
 
Mkuu vipi mzunguko wa pesa Lindi na Mtwara upo? Kuna fursa gani zinapatikana huko?
 
Umemaliza mwaka gani Mahiwa Mkuu.
 
Nimesoma o level pale Kaka
Nimemaliza 2011..Bila Shaka Kwa hili swali lako unapajua mahiwa
Napajua mkuu,ingawa sijasoma hapo ila nilikuwa na mdogo wangu,akawa anasoma Advance hapo Mahiwa High school,kamailiza six 2011. Nikawa namtembelea nyakati za likizo.
 
Napajua mkuu,ingawa sijasoma hapo ila nilikuwa na mdogo wangu,akawa anasoma Advance hapo Mahiwa High school,kamailiza six 2011. Nikawa namtembelea nyakati za likizo.
Aliitwa Nani..yawezekana namjua
 
Habar zingine zinahitaj moyo kuzisoma,mnavyozisifia panya nimechefukwa mno adi nahis kutapika,ila nimejifunza kitu apo
 
Unajua Mungu kaumba viumbe wawili wawili wenye kama kufanana fanana hivi.

Panya wa nyumbani na panya wa porini wanafanana haoo.

Binadamu na tumbili wanafanana hao.

Kenge na mamba wanafanana hao.

Paka na chui hufanana hao.

Tandu na jongoo hufanana hao.

Nyoka na mkunga hufanana haoo.(kuna watu wanakula mkunga nyoka hawali)

Pwngine panya wa porini sio panya ila walipewa jina la panya na watu fulani kswa kuona wamefanana na wale wa nyumbani na kuwafanya wote kuwa panya.

Pengine hata mkunga angepewa jina la nyoka laiti tungelichelewaa kidogo na ingekuwa kumla mkunga inasemwa uamemla nyokaaa
 
Katika safari yako ya siku 35,ulibahatika kupiga kitoweo hicho mara ngapi ndugu,na ulikionaje,ulikifurahia ama?
 
Duuu aisee wewe jamaa wa Nyumbani kabisaaa!!!
Mwezi wa Tisa nakuja Masasi Kwenye msimu wa korosho naomba uniandalie panya kadhaa nitawapokea hapo ndanda
 
Panya wa porini wana proteins nyingi sana. Ni nyama nzuri tu kwa matumizi ya binadamu kama ilivyo ndezi.

Ni utamaduni hasa wa wamakua kutoka Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara. Panya ni watamu sana.

Ahsante.
Na wayao pia wanapatikana masasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…