Ulaji wa Panya mikoa ya Kusini: Safari yangu ya siku 37 ilivyonifungua mambo mengi

Mleta Mada Wale Sio Panya bali wanaitwa Fuko Fuko na huwa hawali nyama au dagaa au unga, ila wanakula mizizi ya mimea kama karanga, mihogo na vinginevyo.

Blaza ungeuliza wanaitwaje hao viumbe kuliko kuja na jina la Panya tena wakati umeshatambua ni kiumbe gani. Umehswahi kuona panya hali nyama au samaki au dagaa?
 
Ni Panya, jamii yenyewe wanaita Panya how comes niite jina tofauti?? Inawezekana unachosema ni kweli lakini siyo kwa jamii ya watu wa Kusini.
 
Ugeweka na kapicha ingependeza zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uongo..panya ni panya na fuko ni fuko..wanyama wawili tofauti
 
Acha uongo..panya ni panya na fuko ni fuko..wanyama wawili tofauti
Umemwelewa mto mada wewe kweli? Umewahi kuona panya anakula mizizi na anatengeneza shimo lenye urefu hata wa mita 100? Watoto mmekua wengi sana Jamii forum siku hizi
 
Panya walioungwa kwa Nazi au karanga wanapatikana?!
 
Ni Panya, jamii yenyewe wanaita Panya how comes niite jina tofauti?? Inawezekana unachosema ni kweli lakini siyo kwa jamii ya watu wa Kusini.
Mie naishi Masasi na ninalima Tunduru kwahiyo naelewa zaidi ya unavyofikiria. Ukanda wote wa kusini kuanzia Namtumbo, Lusewa, Tunduru, Mtambaswala, Mangaka, Masasi, Ndanda, Mtama, Newala, Lindi hadi Kilwa wanakula hao viumbe. Pia na chatu analiwa vizuri sana
 
Umemwelewa mto mada wewe kweli? Umewahi kuona panya anakula mizizi na anatengeneza shimo lenye urefu hata wa mita 100? Watoto mmekua wengi sana Jamii forum siku hizi
Kula mizizi? Kwani mihogo na viaz vitamu siyo mizizi?au mizizi kwako unaelewaje..
Kutengeneza shimo la urefu wa Mita Mia hapana..panya wa porini ana uwezo wa kuchimba shimo refu lkn siyo Mita Mia[emoji16]
 
Hakuna viumbe wanaosumbua kama hao shambani ndo maana kuna mitego hiyo na watu wanawafukizia moshi. Ila ukitaka kuchimba shimo ulifatilie unaweza jikuta umefikisa kilometa moja na usimpate. Kinachosaidia kumpata ni pale utakapokuta udongo aliotufua kwa juu ambao ni mbichi, hapo ndo utajua hayupo mbali na hapo. Maana akishaingia ndani huwa anafukia shimo lake kwa ajili ya usalama.
 
Siyo watu wa mtwara tu ndio wanaokula panya! Hata jule iringa hasa wilaya ya kilolo hao wanyama wanaliwa sana
 
Nami pia nimebahatika kukaa na watu wa sumbawanga nao ni walaji wazuri wa panya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…