Ulaji wa Panya mikoa ya Kusini: Safari yangu ya siku 37 ilivyonifungua mambo mengi

Mi nitaenda Mtwara kwa mambo mengine kabisa ila si kula au mambo ya Panya
 
Watamuu sanaaa
Sema watani zangu mnakula vitu vya kushangaza! Ngedere,nyani, viwavi (chavi chavi) nyie mnatupia tu! Mradi kaumba Mungu
 
Hata baadhi ya watu wa njombe wanakula panya hao wa shambani.
Panya wa njombe tofauti, wanaitwa ndezi na kupa ni wakubwa kama sungura wengine wanazidi hata kwa sungura,siyo jamii ya panya kama wa mtwara na lindi.
 
Watu wakiwa mjini huku wanalishana uongo mwingi. Ukikuta panya wameandaliwa hata hawa wanaopondea wengi watakula.
 
Usisahau pale Mwena
 
vile kina njomba nchumali wakiwahi samaki nchanga sokoni
 
Sema watani zangu mnakula vitu vya kushangaza! Ngedere,nyani, viwavi (chavi chavi) nyie mnatupia tu! Mradi kaumba Mungu
kuna wamakonde chale (wamawia) nasikia, wana asili ya msumbiji.........hao ni kama wachina linapokuja suala la malaji. hata wachache waliopo huku tz upande wa kusini huwa kama wanatengwa flani hv au wanajitenga maana ni kawaida kukuta mtaa wao kabisa au kijiji chao. hao balaa, mkigombana na wakahisi kuna hatari kwao basi kijiji kizima huweza kuhama ndani ya dakika tu.
 
Niliwakuta wengi Sana wiki mbili zilizopita maeneo ya MWENA MKALAPA CHIGUGU katika harakt zangu za maisha

Nilichogundua kumbe sio panya hawa wa majumban wao ni tofaut kabisa Kuna jamaa alinionesha panya ambaye hajabanikwa

Ila inahitji moyo kuwala

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Asee nimeishi Sana kilwa hasa maeneo ya kipatimo masoko pande nakiu nanjirinji kiranjeranje kinjumbi chumo kibata sijawah ona watu wakila chatu au panya si kweli

Panya wanaliwa maeneo ya masasi mangaka Tena mangaka au nanyumbu n maeneo machache Sana


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Km unavyojua mikoa ya Lindi na Mtwara ulaji wa panya ni kitu cha kawaida sana
Sio kweli!! Ni Masasi peke yake ndiko panya wanakoliwa kwa wingi! Hakuna sehemu yoyote Lindi unakoweza kuta panya wanaliwa kwa wingi, na ukiona watu wanakula panya basi huyo ni mwenyeji wa Masasi! Ni kama Zanzibar ukute mtu au baadhi ya watu wanakula kitimoto halafu u-conclude kwamba ni jambo la kawaida sana Zanzibar kuona watu wanakula kitimoto!

Ukikuta mahali Lindi wanakula panya basi ni kama kukuta Zanzibar watu wanakula kitimoto!! Pia sio rahisi ukute panya wanaliwa kwa wingi wilaya zingine za hata mkoa wa Mtwara mbali na Masasi kwa sababu, ukitoa Masasi, wilaya karibu zote Mtwara zimejaa Waislamu!!

Hili nalifahamu vizuri kwa sababu nimezunguka sehemu mbalimbali za mkoa wa Lindi na Mtwara kuanzia mwezi March hadi June.
 
Huyo jamaa muongo!!
 
Acha bas🤪
 
Wewe muongo!!! Ukitoa wilaya ya Masasi (ambayo ndiyo inachanganya na Namtumbo), maeneo mengine uliyotaja yote sio kweli. Mahali kama Newala ukikuta panya basi ni kwa uchache, na watakuwa wanaliwa na wenyeji wa Masasi, au labda watu wa Msumbiji ambao wao ndio ula hadi Chatu, lakini Mmakonde wa kawaida, ambao wengi ni Waislamu, huwezi kukuta wanakula panya au chatu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…