SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Mimi heri mninyang'anye vyote ila mniachie tu ugali.

Mluhya original kutoka magharibi mwa Kenya.
 
Wazee wetu wangekuwa timamu kama unavyowanadi wangewatawala wakoloni au wangeukataa ugali.
Chips yai zinawasahaulisha sana mpaka mmeanza kujiona mna aleji na UGALI
Kabisa. wazee wetu wangekuwa na akili wasingekuwa wanasakwa na Mwaarabu moja kama ng'ombe kutoka Ujiji hadi Bagamoyo. Tena kuna sehemu anasinzia na kulala, wanamlinda hadi aamke then anawasaka tena. Kuna mahali anachoka, wanambeba kwa kupokezana. Wazee wetu walikuwa Fake-n kama sisi sisi wajukuu zao wa chipsi mayai. Vile unavyomuona Mwikaju na Machawa wengine wa CCM ndivyo walivyokuwa wengi wa wazee wetu ingawa inawezaka si wote.
 
Ugali ni chakula cha maskini. Inadumaza akili za watoto. Kama Uchumi wako upo vizuri kidogo piga marukufu ulaji wa ugali wa mahindi kwa watoto wanaokua. Pia, Mungu akikubariki kidogo uchumi wako ukawa bora ondoa ugali wa mahindi katika ratiba ya ulaji wa nyumbani kwako. Zidisha Protini na wanyama na mime na vitaminis (matunda na mbogamboga) katika kapu la chakula cha familia yako kila siku.
 
Ugali ni chakula cha maskini. Inadumaza akili za watoto. Kama Uchumi wako upo vizuri kidogo piga marukufu ulaji wa ugali wa mahindi kwa watoto wanaokua. Pia, Mungu akikubariki kidogo uchumi wako ukawa bora ondoa ugali wa mahindi katika ratiba ya ulaji wa nyumbani kwako. Zidisha Protini na wanyama na mime na vitaminis (matunda na mbogamboga) katika kapu la chakula cha familia yako kila siku.
Umenena kweli Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza mbwa wenyewe wa kibongo wasile ugali si watakufa njaa.
Ukiongelea mbwa sio hao uliosema wa kibongo, hao ni mbwa koko..... ndo wanakula ugali sababu ya kukosa chaguo tu.
 
Vyovyote tutakufa tu,
Nmekumbuka ugali dagaa Dah umatemate umenitoka ,nkajipikilishe tu😅
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Kwani nutrients unazipata kwa kula kitu kimoja pekee? Je, huo ugali unaliwa peke yake?. Wewe sema huna hela ya kununua samaki wa kula na ugali.
 
Umeandika kwa mifano ya nchi nyingine pengine ukiwa hauna hata uhakika...

Nimekula ugali Kenya, nimekula ugali SA na nimekula ugali wa kighana nikiwa China...

Ugali una majina tofauti tofauti kulingana na eneo mfano, corn fufu (West Africa), Ugali (Kenya, Tanzania) Nshima (Zambia), Nsima (Malawi), Sadza (Zimbabwe) na Pap (South Africa)
Ugali (pap) nilikutana nao Botswana, basi na zile nyama zao za ng'ombe utakula tu hata kama haupendi.
 
Nimecheka kama mazuri ... kama sijakosea, ingia Google kisha tafuta matumizi ya mahindi kwa mataifa yanayolima mahindi kwa wingi duniani.. matumizi ya mahindi ni kwa kutengenezea chakula cha mifugo.. kuna majedwali utaona kuwa matumizi ya binadamu ni mwisho kabisa (wametumia neno "kwa matumizi mengineyo"

Source Google

Around 60% of the total maize production in China is utilized for animal feed, and only 10% is used for human food and seeds.

...animal feed and ethanol production collectively make up around 73% of U.S. corn usage. Other uses of corn include the production of sweeteners, starch, cereal, and alcoholic

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugali wa mtama mwekundu uliochanganywa na muhogo plus maziwa ya mgando plus supu ya utumbo,nilikula 2016 katoro pale Kwa mama yangu mdogo aiseh nilikumbuka mbali Sana hasa Kule kibara Busambara kwa Bibi yangu Nganzi!!!

Moja ya mlo Bora kabisa niliowahi kuula!!

Shida ilianza baada ya kuja Dodoma aiseh ugali mahindi ukaanzia hapo warangi hawali ugali wa mtama na mhogo!

So sad!!!mahindi ya plastic haya DK no hatari kwa afya!!
 
Nini kilitangulia kati ya wakoloni na kilimo cha mahindi,.!?,nyie watu mna matatizo kichwani hata kutumia google hamjui. Ila mna justify upumbavu wenu kwasababu nyepesi nyepesi..
Mahindi yaliletwa na Portuguese.
 
Ugali wa mtama mwekundu uliochanganywa na muhogo plus maziwa ya mgando plus supu ya utumbo,nilikula 2016 katoro pale Kwa mama yangu mdogo aiseh nilikumbuka mbali Sana hasa Kule kibara Busambara kwa Bibi yangu Nganzi!!!

Moja ya mlo Bora kabisa niliowahi kuula!!

Shida ilianza baada ya kuja Dodoma aiseh ugali mahindi ukaanzia hapo warangi hawali ugali wa mtama na mhogo!

So sad!!!mahindi ya plastic haya DK no hatari kwa afya!!
Ugali haufai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwana, unazidiwa akili mpaka na panya? Ukikoboa mahindi unabaki unakula makapi ambayo haya panya hayali! Yaani wewe unachukua mahindi tu kutoka kwa wauzaji na kwenda kusaga? Hopeless kabisa!
Twende Kwa facts, hizo story za makapi huwa wanaongea malayman wasiojua chochote kuhusu nutrition. Embu tujue ukikoboa unaondoa virutubisho gani ambavyo havipatikani kwingine? most of the time ugali huwa unaliwa na mboga hauliwi mkavu, kiini cha indi ambacho kinaondolewa kina fat kwa wingi na protein kidogo, vitamins kidogo plus fibers ambazo zinapatikana kwenye ganda la nje. Vyote hivyo unaweza vipata Kwa usalama kabisa toka kwenye mboga zako za majani au hata maarage, iwapo itakula ugali ndondo. Ukikoboa utabakiza starch na fats, starch ndicho kitu kikuu unachokufuatwa kwenye mahindi.
Cha msingi ni wewe ni kuchagua unahitaji hayo MAFUTA na some little protein with a cocktail of toxins au ukoboe ili uoñdokane na majanga ili hivyo vitu unavyoondoa upate kwenye source zingine.
 
Sina uhakika kuhusu faida za ugali mwilini, ila umedanganya kuhusu mataifa mengine kula ugali. Africa nzima chakula kikuu ni ugali kama unasema Nigeria, Ghana, Cameroon na west kwa ujumla hawali ugali basi inaonekana hujasafiri kwenda popote. Halafu hujui hata Corn flakes, pop corn 🌽 wanazobugia wazungu ni mahindi hayohayo tofauti ni mbeguna mapishi tu?.. kama ugali ungekuwa na shida yoyote basi hata shuleni na vyuoni kusingekuwa na wakufunzi, maana wote wamelelewa na ugali na maharage. Sema nini, unaonekana una ulimbukeni fulani hivi..
Kapata mgao wa mafao ndo anakuja kuropoka huku.
 
Back
Top Bottom