SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Protein gani ambazo zipo kwenye ugali?
Ugali ukiwa na 100g..
Ina contain 7g of Protein ambayo ni sawa na 14%

Na Protein inayopatikana kwenye ugali inautwa zein pamoja na Gluten..

Japo hizo protein zote zinafahamika kama prolamine protein maana yake Ili ziweze kufanya kazi ya kutengeneza Essential protein Ambayo itatupa amino acid kwa ajili ya mwili wetu lazma kwepo kwa protein nyingine..

Na ndo hiyo inabidi ile mboga ili Uipate..
Huwezi kula ugali peke yake..

Ukipiga na maharage au nyama ana mboga za majani bhasi Unaiaxtivate hiyo Protein iliyopo kwenye ugali then kitu mwake
 
Huo uchafu tumelishwa sana boarding, wakichange wakawa wanatupa kande ujinga ule ule. Saizi naweza maliza mwaka sijagusa ugali!
Zamani nlikua nakula ugali vizur tu Ila now days ugali nafsi inakataa kabisa Yan Nikila Nakua najoforce sana
 
Kwani makuli wapo Tz peke yake?
Nchi ambayo kwa mwaka hayafiki makontena 1mil

Nigeria hawali ugali ila wana miili mikubwa
Nigeria ipi ambayo hawali ugali??
NIgeria wanakula Fufu au "Akple" ambalo ni jina jingine la.ugali kwao
 
Habari Mtoa Mada ngara23
Unaweza kuwa unahoja lakini uwasilishaji wako Ukavuruga hata maana ya amada yako uliyoitoa..

Ni kweli kuna baadhi ya vitu unaweza ukawa ulisema kweli..

Kama uliposema (Ntanukuu)

"Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli"

Hili ni Kweli kabisa watu wengi wanaamini hivyo Ilihali si kweli...Kuna vyakula vingine vya kuupa Mwili nguvu vya kiasili kama magimbi,Viazi aina zote,Mihogo n.k

Hilo ni jambo ambalo kati ya yote Ndilo uliloelezea ukweli mengine yote umeongea Uongo kwa 100%

MisInformation Ulizotoa Kuhusu Ugali

  • KUHUSU SUMU Na KUWA UGALI HAUNA NUTRIENTS ZOZOTE
Ugali Ni Sumu , Jibu "Partially True and Partially false "Ni ukweli na pia ni Uongo"

ni kweli kwamba kuna baadhi ya mahindi, Unga na hata ugali una chembe chembe za Heavy metal ambazo ni mycotoxins zinazoitwa Aflatoxins au kwa jina jingine Aspergillus flavus zipo kiwango kidogo sana yaani (μg g−1)..

Japo kama utakula Wingi sana wa mahindi na ugali wenye chembe za Aflatoxin..Utapata Kitu kinaitwa kitaalam aflatoxicosis..
Ambazo inaweza kukusababishia maradhi mengine kama cancer, Infertility, organ failure hasa Kidney..

Lakini Angalizo ni kuwa Si kila Ugali au kila unga unakuwa na Mycotoxin mpaka uwe umekula Mahindi au Ugali wenye Toxin hiyo ndo utapata hayo maradhi...

Lakini kwa Tanzania Kuna case ambazo.ni chini ya 2% ya wagonjwa wote waliowahi kutibiwa kwa kupata Aflatoxicosis...
Kwahyo Tanzania Tuko safe na ugali tulionao..

  • KUHUSU UGALI KUTOKUWA NA NUTRIENTS YOYOTE
Hili lina Ukweli kwa 0.001% na lina uongo kwa 99.99%
kwanini..?

Katika vyakula vya Asili,Ugali ni miongoni mwa vyakula vyenye Lishe bora sana na hasa chanzo kikubwa cha wanga na Nishati..
Katika kila 100 grams ya Unga wa Ugali kuna viti vifuatavyo (Kumbuka Mtu mzima anakula Walau robo ya Ugali ila hapo kwa kila Tonge au Nusu tonge)
  • Calories 370
  • Total Fat 1.8 g ambayo ni sawa na 2% ya Daily value kama utakula hivyo kila siku
  • Saturated fat 0.2 g daily value ya 1%
  • Trans fat regulation 0 g
  • Cholesterol 0 mg
  • Sodium 7 mg0%
  • Potassium 142 mg4%
  • Total Carbohydrate 79 g26%
  • Dietary fiber 3.9 g15%
  • Sugar 1.6 g
  • Protein 7 g14%
  • Vitamin C0%Calcium0%
  • Iron6%Vitamin D0%
  • Vitamin B610%
  • Cobalamin0%
  • Magnesium8%
Hapo ni kwa kiasi sijataja zote halafu unakuja unasema kuwa Haina Nultrients unajua maana ya Nutrients??

Umezungumzia kuhus Mataifa mengine afrika kwmaba hawali Ugali

Hapa ndo nilipogundua kumbe kuna uwezekano hujatembea hata Afrika yote hata kenya Tu hujafika! Uganda pia Hujafika?

Sasa nisikilize!
Hakuna nchi Afrika ambayo haili ugali..

Uganda na Kenya na Tanzania wote wanakula Ugali..
  • Ukienda kenya watauita Sima/Nsima
  • Ukienda uganda wataita Posho
  • Tanzania wataita Ugali/Nguna/Dona/Bondo
  • Central Africa na zambia,Malawi pamoja na Kongo huko wanaita Nshima
  • Zimbabwe wanaita Sadza
  • South Africa na sehemu na Botswana wanaita Pap kwa ule mlaini ila ule wenyewe wa Kisukuma mgumu wanaita Bogobe au
    Stywe
  • Sierra Leone, Guinea, Liberia, Cote D'Ivoire, Burkina Faso, Benin, Togo,Nigeria, Cameroon, Angola na Gabon huko wao wanaita Fufu
  • Ghana wanaita Banku au Akple
Kama kuna Nchi au sehemu sijataja nikumbushe nitakuambia wanaitaje..

Mwishoni Umeweka sawa kuwa hupendi ugali bhasi kitu ambacho hukipendi usikipakazie Mambo mabaya ili na wngine wakichukie..
Hata mimi sipendi ugali ila siwezi kuufanya wengine wasile
Huu ugali uliolezea hapa ni wa UNGA wa Dona au sembe
 
....

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

........
Unafahamu Kenke, unafahamu Banku zinatokana na nini?
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Wakenya Hawali ugali. We kenge kwerikweri
 
Mkuu japo nakuunga mkono ila research yako haiko sawa.
Kenya, uganda hata west africa wanakula ugali. Kagera now ndizi kutojana na mnyauko wanakula ugali sana.
Ila naunga mkono hoja ugali si chakula safi ni sumu na kinadumaza ubongo.
 
Ugali Bora ni sembe kwani wafanyabiashara wengi wakiona mahindi yameharibika au kuoza ( Kuota fungus) hupendelea kuyasaga moja Kwa moja kuwa unga. Sembe ni Bora Kwa kuwa sembe inakaa muda mrefu bila kuharibika ukilinganisha na Dona kutokana na MAFUTA. Dona ina MAFUTA mengi kuliko sembe sababu ya kiini cha mbegu za mahindi ambacho kwenye sembe huwa kinaondolewa. Dona nyinginzilizopo madukani huwa zinawahi kuharibika nankuwa chu
Mwana, unazidiwa akili mpaka na panya? Ukikoboa mahindi unabaki unakula makapi ambayo haya panya hayali! Yaani wewe unachukua mahindi tu kutoka kwa wauzaji na kwenda kusaga? Hopeless kabisa!
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Mkuu una matatizo makubwa sana ya kifikra na uelewa, tulia usome na kujifunza vyema. Ulichoandika ni utumbo uliopitiliza, hadi nashindwa hata nikusaidije, kifupi uelewa wako wa ulichokiandika ni mdogo sana. Ni ajabu na wewe unajiita GT na unatoa pumba kama hizi.
 
Back
Top Bottom