SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Wazungu wanakula mahindi sio ugali
Fala wewe, kwahiyo mtu anayekula vitumbua hali mchele!?,unga wa ugali si unatokana na mahindi!?, Kwahiyo unga wa mahindi una matatizo, ila mahindi hayana shida!?,hivi jamii forums imevamiwa na watoto siku hizi!??
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Eti Kenya na Rwanda hawali ugali 🤣🤣🤣 sidhani kama umewahi hata kuishi huko

Wewe endelea kula chips mayai za Dar
 
Sijatembea Kenya na Nigeria sana nj3 ya miji mikuu lagos na Nairobi, ila kule Ugali wanapiga bila huruma , nmetokea siku hizi kuupenda sana , nina miezi kama sita bila kuugusa wali, mwili una nguvu sana na afya tele
 
Ugali si chakula
kataa ugali
unagali unadumaza akili
ugali unadumaza mwili
ugali ni sumu
ugali hauna nutrients zinazohitajika mwilini
kula ugali ni kujaza tumbo tu
samia piga marufuku ulaji wa maugali tanzania.
Tatizo ni umasikini
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Kuleni wali kama watu wa Dar ambao hawawezi kazi ngumu zaidi ya utapeli!
 
Wazee wetu wangekuwa timamu kama unavyowanadi wangewatawala wakoloni au wangeukataa ugali.
Chips yai zinawasahaulisha sana mpaka mmeanza kujiona mna aleji na UGALI
Miaka hiyo wazee walikuwa na taaluma ya ku detect sumu kwenye msosi

Kipindi hicho mtu mbaya alikuwa hawezi kukuletea msosi usio na sumu.

Wazee walipoona hakuna sumu wakawaona wazungu ni watu waungwana sana.
 
Back
Top Bottom