Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli
Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.
Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali
Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.
Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.
Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa
Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.
Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.
Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali
Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali
Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali
#kataa ugali Mtanganyika
Habari Mtoa Mada
ngara23
Unaweza kuwa unahoja lakini uwasilishaji wako Ukavuruga hata maana ya amada yako uliyoitoa..
Ni kweli kuna baadhi ya vitu unaweza ukawa ulisema kweli..
Kama uliposema (Ntanukuu)
"Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli"
Hili ni Kweli kabisa watu wengi wanaamini hivyo Ilihali si kweli...Kuna vyakula vingine vya kuupa Mwili nguvu vya kiasili kama magimbi,Viazi aina zote,Mihogo n.k
Hilo ni jambo ambalo kati ya yote Ndilo uliloelezea ukweli mengine ila mengine yanatia mashaka
MisInformation Ulizotoa Kuhusu Ugali
- KUHUSU SUMU Na KUWA UGALI HAUNA NUTRIENTS ZOZOTE
Ugali Ni Sumu , Jibu "Partially True and Partially false "Ni ukweli na pia ni Uongo"
ni kweli kwamba kuna baadhi ya mahindi, Unga na hata ugali una chembe chembe za Heavy metal ambazo ni
mycotoxins zinazoitwa
Aflatoxins au kwa jina jingine
Aspergillus flavus zipo kiwango kidogo sana yaani (μg g−1)..
Japo kama utakula Wingi sana wa mahindi na ugali wenye chembe za Aflatoxin..Utapata Kitu kinaitwa kitaalam
aflatoxicosis..
Ambazo inaweza kukusababishia maradhi mengine kama cancer, Infertility, organ failure hasa Kidney..
Lakini Angalizo ni kuwa Si kila Ugali au kila unga unakuwa na Mycotoxin mpaka uwe umekula Mahindi au Ugali wenye Toxin hiyo ndo utapata hayo maradhi...
Lakini kwa Tanzania Kuna case ambazo.ni chini ya 2% ya wagonjwa wote waliowahi kutibiwa kwa kupata Aflatoxicosis...
Kwahyo Tanzania Tuko safe na ugali tulionao..
- KUHUSU UGALI KUTOKUWA NA NUTRIENTS YOYOTE
Hili lina Ukweli kwa 0.001% na lina uongo kwa 99.99%
kwanini..?
Katika vyakula vya Asili,Ugali ni miongoni mwa vyakula vyenye Lishe bora sana na hasa chanzo kikubwa cha wanga na Nishati..
Katika kila 100 grams ya Unga wa Ugali kuna viti vifuatavyo (
Kumbuka Mtu mzima anakula Walau robo ya Ugali ila hapo kwa kila Tonge au Nusu tonge)
- Calories 370
- Total Fat 1.8 g ambayo ni sawa na 2% ya Daily value kama utakula hivyo kila siku
- Saturated fat 0.2 g daily value ya 1%
- Trans fat regulation 0 g
- Cholesterol 0 mg
- Sodium 7 mg0%
- Potassium 142 mg4%
- Total Carbohydrate 79 g26%
- Dietary fiber 3.9 g15%
- Sugar 1.6 g
- Protein 7 g14%
- Vitamin C0%Calcium0%
- Iron6%Vitamin D0%
- Vitamin B610%
- Cobalamin0%
- Magnesium8%
Hapo ni kwa kiasi sijataja zote halafu unakuja unasema kuwa Haina Nultrients unajua maana ya Nutrients??
Umezungumzia kuhus Mataifa mengine afrika kwmaba hawali Ugali
Hapa ndo nilipogundua kumbe kuna uwezekano hujatembea hata Afrika yote hata kenya Tu hujafika! Uganda pia Hujafika?
Sasa nisikilize!
Hakuna nchi Afrika ambayo haili ugali..
Uganda na Kenya na Tanzania wote wanakula Ugali..
- Ukienda kenya watauita Sima/Nsima
- Ukienda uganda wataita Posho
- Tanzania wataita Ugali/Nguna/Dona/Bondo
- Central Africa na zambia,Malawi pamoja na Kongo huko wanaita Nshima
- Zimbabwe wanaita Sadza
- South Africa na sehemu na Botswana wanaita Pap kwa ule mlaini ila ule wenyewe wa Kisukuma mgumu wanaita Bogobe au
Stywe
- Sierra Leone, Guinea, Liberia, Cote D'Ivoire, Burkina Faso, Benin, Togo,Nigeria, Cameroon, Angola na Gabon huko wao wanaita Fufu
- Ghana wanaita Banku au Akple
Kama kuna Nchi au sehemu sijataja nikumbushe nitakuambia wanaitaje..
Mwishoni Umeweka sawa kuwa hupendi ugali bhasi kitu ambacho hukipendi usikipakazie Mambo mabaya ili na wngine wakichukie..
Hata mimi sipendi ugali ila siwezi kuufanya wengine wasile