SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Ijapokuwa kuna chembechembe za kweli, hii mada yako ni uongo kwa asilimia karibu 78.

1. Ugali ni bora kama unga haujakobolewa, unga ukikobolewa unapoteza angalau 75% ya virutubisho vyake.

2. Ugali ni chakula bora sana, ni chanzo kikubwa cha starch(wanga), ambayo humeng'enywa kutengeneza glucose. Kwa bahati mbaya, wengi wamezoea kula kiasi kikubwa sana cha ugali kuliko uhitaji wa miili yao. Hili linasababisha shibe inayoambatana na usingizi mzito na kuchoka kwa mwili kutokana na mwili kutumia nguvu nyingi kwenye kumeng'enya starch.

3. Changamoto kubwa zaidi kwenye ugali ipo kwenye kutokausha maindi vzuri ndio yahifadhiwe. Hili linasababisha maindi mengine kuharibika kwa kupata cyanide. Maindi haya yakikobolewa, ugali huwa hatarishi kama chakula.

4. It is fiber rich delicasy, so it prevents constipation(nnya laiiiiniii.)

5. Inasaidia kwenye emeng'enyaji wa chakula kutokana na utajiri wake wa fibres.

6.ugali una utajiri wa proteins ambazo ni muhimu kwenye kujenga afya bora.

7. Ulaji wa ugali haswa ambao haijakobolewa, husaidia kwenye kujenga ngozi bora(ndio maana unapendwa na Wanawake) na madini yaliyopo ndani yake, hutumiwa kuboresha afya kwa mlaji.

Juu ya yote, jamii kadhaa za Kenya kama wajaluo, wakisii, wakamba pamoja na waluhya wanapenda ugali kupitiliza. So kusema wakenya hawapendelei ugali ni unafki.
Mwisho, usikilaumu chakula. Jilaumu wewe kwa kushindilia ugali mwingi kuliko mahitaji ya mwili wako. Ila ugali ni chakula bora sana na ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
1. Ugali 'Bora' ni ule uliokobolewa, coz kiasi cha sumu za kuhifadhia hayo mahindi hupungua kupigia ukoboaji, labda kama hayo mahindi umelima wewe. Ugali Bora ni sembe kwani wafanyabiashara wengi wakiona mahindi yameharibika au kuoza ( Kuota fungus) hupendelea kuyasaga moja Kwa moja kuwa unga. Sembe ni Bora Kwa kuwa sembe inakaa muda mrefu bila kuharibika ukilinganisha na Dona kutokana na MAFUTA. Dona ina MAFUTA mengi kuliko sembe sababu ya kiini cha mbegu za mahindi ambacho kwenye sembe huwa kinaondolewa. Dona nyinginzilizopo madukani huwa zinawahi kuharibika nankuwa chungu kutokana na oxidation ya MAFUTA inayosabanishwa na uwepo wa hayo mafuta ikichangiwa na mwanga na joto. Athari unazoweza zipata Kwa Kula unga ulikuwa oxidized ni pamoja na cancer n.k
2. Kuna vyanzo vingi vya starch kama wali, tambi, viazi n.k wataalamu wanasema starch na sukari siyo nzuri Kwa Afya yako, matatizo mengi yabkiafya yanasababishwa na starch) sukari yakiwemo matatizo ya ini, kisukari, figo n.k
3. Mahindi hayana cyanide. Cyanide iponkwemye mihogo, na ni natural compound inayozalishwa kwenye mihogo ili kujilinda. So si kweli usipokausha vzuri mahindi yatatengeza cyanide, instead yatashambuliwa na fungus wanaosababisha sumukuvu.
4. Opt vegetables instead if you real need fibers.
5. As 4 above.
6. Animal proteins is better coz unapoila haina vipingamizi kama vilivyopo kwemye plant based proteins. Proteins za mimea zinakuwa na vipingamizi vingi ( anti nutritional factors) ambazo vinapunguza bioavailability yake.
7. Kuhusu ngozi SINA uhakika..hope tumeelewana
 
Mimi ugali naokul
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika

Sent using Jamii Forums mobile app
Ugali naokula mimi ni mahindi na ngano
 
Source: TRUST ME BRO
 
Unapokataza kula ugali tuambie pambio lingine la mlo tule nini!!
Vinginevyo unatudanganya.
 
Asili ya mahindi ni Amerika ya kati na Mexico.

Hata ukiangalia katika nchi zenye uzalishaji wa mahindi kidunia utaona katika nchi 15, ni nchi 3 tu ambazo ni za Afrika.

Nazo hizo zimeshika nafasi ya mwishoni.
View attachment 2944737

Mahindi yalikuja Afrika karne ya saba yakianzia Pwani ya Afrika.

Kabla ya karne ya saba, Afrika hakukuwa na kitu kinachoitwa mahindi.
Huko wanazalisha Kwa wingi kulisha mifugo kama ng'ombe nguruwe sio kula kama ninyi!
 
Mwenyewe nilishtuka mapema nashukur Mungu nikajiuliza kwann wazungu hawali maindi, binafsi mm kitu kama mzungu hatumii na mm siwez tumia ndio utamadun wangu coz wazungu wapo mbele kifikra miaka elfu tano kuliko sisi ngozi nyeusi!! Hata kama mtakataaa.

Hvo nikapiga marufuku ugal pale home ni mwendo wa wali ndizi,viazi.naona positive changes nyingi sana .

Ugali na maindi kiujumla ni chakula Cha wanyama..wengi hamuwez elewa huyu mtoa mada anamaanisha nn sabb ugali ushawaathiri uwezo wenu wa kufikiri!!

Mwisho ugali ni sumu inayoua taratibu kama sigara na pombekali
 
Back
Top Bottom