SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Ijapokuwa kuna chembechembe za kweli, hii mada yako ni uongo kwa asilimia karibu 78.

1. Ugali ni bora kama unga haujakobolewa, unga ukikobolewa unapoteza angalau 75% ya virutubisho vyake.

2. Ugali ni chakula bora sana, ni chanzo kikubwa cha starch(wanga), ambayo humeng'enywa kutengeneza glucose. Kwa bahati mbaya, wengi wamezoea kula kiasi kikubwa sana cha ugali kuliko uhitaji wa miili yao. Hili linasababisha shibe inayoambatana na usingizi mzito na kuchoka kwa mwili kutokana na mwili kutumia nguvu nyingi kwenye kumeng'enya starch.

3. Changamoto kubwa zaidi kwenye ugali ipo kwenye kutokausha maindi vzuri ndio yahifadhiwe. Hili linasababisha maindi mengine kuharibika kwa kupata cyanide. Maindi haya yakikobolewa, ugali huwa hatarishi kama chakula.

4. It is fiber rich delicasy, so it prevents constipation(nnya laiiiiniii.)

5. Inasaidia kwenye emeng'enyaji wa chakula kutokana na utajiri wake wa fibres.

6.ugali una utajiri wa proteins ambazo ni muhimu kwenye kujenga afya bora.

7. Ulaji wa ugali haswa ambao haijakobolewa, husaidia kwenye kujenga ngozi bora(ndio maana unapendwa na Wanawake) na madini yaliyopo ndani yake, hutumiwa kuboresha afya kwa mlaji.

Juu ya yote, jamii kadhaa za Kenya kama wajaluo, wakisii, wakamba pamoja na waluhya wanapenda ugali kupitiliza. So kusema wakenya hawapendelei ugali ni unafki.
Mwisho, usikilaumu chakula. Jilaumu wewe kwa kushindilia ugali mwingi kuliko mahitaji ya mwili wako. Ila ugali ni chakula bora sana na ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
Wakenya hao uwatajao wanakula ugali utokanao na mahindi au mtama?
 
Ungejipanga vizuri kabla ya kuandika, siwezi kuamini kuwa wasukuma, wanyamwezi na watu wa mikoa ya Mara na Singida ni makabila madogo! Hawa wote wala ugali.
Zambia ugali mara tatu kwa siku na Malawi ni wala ugali, Afrika Magharibi wala ugali wote hawa tofauti ni aina ya unga wanaotumia.
Kanda ya Ziwa wanakula ugali wa Mtama na siyo mahindi
 
Habari Mtoa Mada ngara23
Unaweza kuwa unahoja lakini uwasilishaji wako Ukavuruga hata maana ya amada yako uliyoitoa..

Ni kweli kuna baadhi ya vitu unaweza ukawa ulisema kweli..

Kama uliposema (Ntanukuu)

"Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli"

Hili ni Kweli kabisa watu wengi wanaamini hivyo Ilihali si kweli...Kuna vyakula vingine vya kuupa Mwili nguvu vya kiasili kama magimbi,Viazi aina zote,Mihogo n.k

Hilo ni jambo ambalo kati ya yote Ndilo uliloelezea ukweli mengine ila mengine yanatia mashaka

MisInformation Ulizotoa Kuhusu Ugali

  • KUHUSU SUMU Na KUWA UGALI HAUNA NUTRIENTS ZOZOTE
Ugali Ni Sumu , Jibu "Partially True and Partially false "Ni ukweli na pia ni Uongo"

ni kweli kwamba kuna baadhi ya mahindi, Unga na hata ugali una chembe chembe za Heavy metal ambazo ni mycotoxins zinazoitwa Aflatoxins au kwa jina jingine Aspergillus flavus zipo kiwango kidogo sana yaani (μg g−1)..

Japo kama utakula Wingi sana wa mahindi na ugali wenye chembe za Aflatoxin..Utapata Kitu kinaitwa kitaalam aflatoxicosis..
Ambazo inaweza kukusababishia maradhi mengine kama cancer, Infertility, organ failure hasa Kidney..

Lakini Angalizo ni kuwa Si kila Ugali au kila unga unakuwa na Mycotoxin mpaka uwe umekula Mahindi au Ugali wenye Toxin hiyo ndo utapata hayo maradhi...

Lakini kwa Tanzania Kuna case ambazo.ni chini ya 2% ya wagonjwa wote waliowahi kutibiwa kwa kupata Aflatoxicosis...
Kwahyo Tanzania Tuko safe na ugali tulionao..

  • KUHUSU UGALI KUTOKUWA NA NUTRIENTS YOYOTE
Hili lina Ukweli kwa 0.001% na lina uongo kwa 99.99%
kwanini..?

Katika vyakula vya Asili,Ugali ni miongoni mwa vyakula vyenye Lishe bora sana na hasa chanzo kikubwa cha wanga na Nishati..
Katika kila 100 grams ya Unga wa Ugali kuna viti vifuatavyo (Kumbuka Mtu mzima anakula Walau robo ya Ugali ila hapo kwa kila Tonge au Nusu tonge)
  • Calories 370
  • Total Fat 1.8 g ambayo ni sawa na 2% ya Daily value kama utakula hivyo kila siku
  • Saturated fat 0.2 g daily value ya 1%
  • Trans fat regulation 0 g
  • Cholesterol 0 mg
  • Sodium 7 mg0%
  • Potassium 142 mg4%
  • Total Carbohydrate 79 g26%
  • Dietary fiber 3.9 g15%
  • Sugar 1.6 g
  • Protein 7 g14%
  • Vitamin C0%Calcium0%
  • Iron6%Vitamin D0%
  • Vitamin B610%
  • Cobalamin0%
  • Magnesium8%
Hapo ni kwa kiasi sijataja zote halafu unakuja unasema kuwa Haina Nultrients unajua maana ya Nutrients??

Umezungumzia kuhus Mataifa mengine afrika kwmaba hawali Ugali

Hapa ndo nilipogundua kumbe kuna uwezekano hujatembea hata Afrika yote hata kenya Tu hujafika! Uganda pia Hujafika?

Sasa nisikilize!
Hakuna nchi Afrika ambayo haili ugali..

Uganda na Kenya na Tanzania wote wanakula Ugali..
  • Ukienda kenya watauita Sima/Nsima
  • Ukienda uganda wataita Posho
  • Tanzania wataita Ugali/Nguna/Dona/Bondo
  • Central Africa na zambia,Malawi pamoja na Kongo huko wanaita Nshima
  • Zimbabwe wanaita Sadza
  • South Africa na sehemu na Botswana wanaita Pap kwa ule mlaini ila ule wenyewe wa Kisukuma mgumu wanaita Bogobe au
    Stywe
  • Sierra Leone, Guinea, Liberia, Cote D'Ivoire, Burkina Faso, Benin, Togo,Nigeria, Cameroon, Angola na Gabon huko wao wanaita Fufu
  • Ghana wanaita Banku au Akple
Kama kuna Nchi au sehemu sijataja nikumbushe nitakuambia wanaitaje..

Mwishoni Umeweka sawa kuwa hupendi ugali bhasi kitu ambacho hukipendi usikipakazie Mambo mabaya ili na wngine wakichukie..
Hata mimi sipendi ugali ila siwezi kuufanya wengine wasile
Dr. Shukrani Kwa michango but naomba nirekebishe kidogo kwenye hii hoja hapa;
'Unga na hata ugali una chembe chembe za Heavy metal ambazo ni mycotoxins zinazoitwa Aflatoxins au kwa jina jingine Aspergillus flavus zipo kiwango kidogo sana yaani (μg g−1)..'
Hoja ya Kwanza: Chembe chembe za heavy metals Kwa Kiswahili ni madini tembo na yapo ya aina nyingi kama zebaki, lead, Arsenic etc. so heavy metals zinastand alone. in most cases unga wa mahindi ni nadra sana kuwa na Kiasi kikubwa cha madini tembo ( Heavy metals). Labda kama process ilikuwa very very contaminated au kuna uchafuzi wa hali ya juu huko mashambani kutokana na sumu za kuuwa wadudu mbolea n.k
Hoja ya pili: Ni kweli mycotoxins Zipo za aina nyingi moja wapo ni hii inaitwa aflatoxin Kwa Kiswahili 'SUMUKUVU'. Sumu kuvu ni sumu zinazozalishwa na ukungu au Kwa lugha ya kigeni moulds ambao huota kwenye hizo nafaka na bidhaa zake kama unga, mikate, maandazi, mihogo n.k. Kuna ukungu WA Aina nyingi lakini ambao unaweza zalisha sumukuvu ni pamoja na hao Aspergilus flavus penicillium, fusarium etc.
HOJA YA MSINGI. Mahindi na Karanga
huwa yatashambuliwa Kwa wingi na Kwa urahisi Sana na hao ukungu wanaozalisha sumukuvu. In most cases mashambulizi haya yanatokana na uhifadhi mbaya WA nafaka na bidhaa zake. Chanzo kikuu cha mashambulizi ni uhifadhi unaosababisha unyevu pamoja na uchafu.
Sumu zingine kwenye hizi nafaka zetu ni vihifadhi au Kwa lugha ingine pesticides ambazo wengi huweka ili nafaka ziliharibiwe na wadudu waharibifu. Tatizo kubwa kinakuwa kwenye withdrawal period ambapo wengi ya wakulima huwa hawazingatii.. maelekezo wanasema sumu ikitpulizwa mahindi yasitumike Kwa miezi mitatu but wengi wao wanapuliza leo wanauza kesho. Sasa sumu hizi si rahisi kuziona au kuzinusa au kuziona, so the safe side ni kuyaosha na kuyakoboa haya mahindi, çoz hatujui Kipi kilifanyika nyumba ya pazia. But kama unauhakika na value chain ya mahindi yako basi yasage Dona.
 
Shukrani sana Chief nakubali marekebisho!
Japo Nilikosea, lengo nilikuwa ni kuandila Heavy metal na mycotoxins..
Ila kwa bahati mbaya Nilisahau kiunganishi "Na" baina ya maneno hayo..

Sina elimu Kubwa sana kuhusu Afya ya Mazingira "Enviromental Health" na Elimu ya Mimea "Botanist"

Kuhusu Lini hasa Sumu hizo Za mycotoxins huingia kwenye Mahindi..
Mycotoxins "Fusarium" na "Aspergillus species" inashambulia Mhindi na mahindi Kwenye stage mbili ambazo ni both pre-harvest na storage stage..

Kuna studies nyingi zilizofanyika na zimeonyesha hivyo moja ya study ni hii hapa chini..

A Comprehensive Study on the Occurrence of Mycotoxins and Their Producing Fungi during the Maize Production Cycle in Spain contamination is one of,pre-harvest and during storage.
 
Yah: Mashambulizi na Uchafuzi yanaweza tokea katika stage yeyote katika value chains ya mahindi. Inaweza kuwa shambani, wakati wakati uhifadhi usafirishaji, na hata pale nyumbani. So stage zote lazima watu wawe makini. Kinachowezekana kufanya kifanyike Kwa umakini na Kwa wakati.
 
Na kwa mikoa yenye Uhanga wa mvua na mvua Nyingi Inatokea sana
 
Mwaka 2017 watu kadhaa walifariki Dodoma na Manyama kutokana na Kula chakula Cheney sumukuvu. So Tanzania pia tuna hili tatizo.
NAfahamu na Lipo kwa kasi sana..
Japo kwenye Mihogo huwa ndo lina Onekana sana..

Ila kwenye mahindi Huwa ni kiasi kidogo na inaathiri Polepole..

Kama Umesoma hiyo report means kama hizo zina high level means nyingi kama sio zote zina Low level..

So hakuna hata mmoja aliye huru na Sumu hii wote tuko infected kama tukiendelea kula ugali..
 
NAfahamu na Lipo kwa kasi sana..
Japo kwenye Mihogo huwa ndo lina Onekana sana..

Ila kwenye mahindi Huwa ni kiasi kidogo na inaathiri Polepole..

Kama Umesoma hiyo report means kama hizo zina high level means nyingi kama sio zote zina Low level
Ukungu wanaoota kwenye mihogo siyo wale wanaozalisha sumukuvu. Au ata wakitokea kuivamia mihogo basi wanakuwa hawapati stress ya kuweza kuzalisha sumukuvu. Kuna species zaidi ya 40 za ukungu/ moulds. Kuna ambao wanazlisha sumukuvu na ambao hawazalishi. Ukungu wanafanana kimuonekano wa nje kwani huonekani Kwa rangi, kama njano, Kijani, kijivu n.k inahitaji laboratory procedure kuweza watofautisha
 
Shukrani kwa somo mkuu..
Mnatakiwa sana mtufundishe..

Haya mambo tunahitaji sana kuyajua Vinginevyo tutaisha sana
 
Ukungu wanaoota kwenye mihogo siyo wale wanaozalisha sumukuvu. Au ata wakitokea kuivamia mihogo basi wanakuwa hawapati stress ya kuweza kuzalisha sumukuvu. Kuna species zaidi ya 40 za ukungu/ moulds. Kuna ambao wanazlisha sumukuvu na ambao hawazalishi. Ukungu wanafanana kimuonekano wa nje kwani huonekani Kwa rangi, kama njano, Kijani, kijivu n.k inahitaji laboratory procedure kuweza watofautisha
Asante kwa elimu Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MTU kutokuwa na akili tatizo sio u gal I MTU mweusi dunia nzima yupo hana maendeleo
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Acha utani
 
ukila ugali ujue na kufanya kazi za nguvu kama wasukuma. piga jembe sawasawa
 
Back
Top Bottom