SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Sukar
 
Hakikisha unachanganya mahindi na ngano au unga wa ngano na unga wa mahindi...kupunguza udumavu wa akili
 
Tatizo la kusomea ungwini badala ya Masomo ya sayansi ....
....
Nchi imezalisha vilaza na wapiga domo wengi.

Ugali ni Carbohydrate kama ilivyo keki kinachotakiwa ni kupamba pishi la ugali(kama mchuzi wa samaki unavyoitwa makange halafu unauziwa 20,000 au mihogo ya kukaanga inayouzwa 20,000) ....
inabidi hoteli za Tanzania ziweke special menu ya Ugali mfano:
-Brown Ugali
-Squared Ugali
-Air dried ugali
-Soft Ugali(kwante) n.k
 
Ni kweli mleta mada hajaweka takwimu za kitaalamu hivyo basi hii inabaki kama mtazamo wake binafsi, kimsingi mahindi kama mahindi yana nutrition muhimu kwa kiwango kikubwa kabisa. Mfano food composition ya unga wa mahindi kwa 100g unapata; energy 363kcal, 8.4g of protein na 1.2g of fat. Ukilinganisha na unga wa ngano; energy 364kcal, 10.9g of protein, 1.1g of fat. Hapo tunaona utofauti ni mdogo sana.

Shida ni maandalizi yake, mahindi ni tofauti na ugali. Mara nyingi mahindi yanaliwa yakiwa freshy kabisa tofauti na ugali. Kwa mtazamo wangu na experience yangu binafsi, ugali unaharakisha mchakato wa kuleta usingizi. Sasa basi kama unaleta usingizi hapo tayari ni kisababishi cha kupunguza uwezo wa ufanisi kwa muda. Kama tunavyojua katika hali ya usingizi kunaambatana na uchovu na hali ya uchovu unaathiri utendaji wa ubongo.
 
Ugali waliouharibu ni wale wa kuukoboa ni ugali mbaya sana , Sema mm ugali wangu nauwekea mahindi yasiyokobolewa , Ngano isiyokobolewa, kitu kimoja kitamu sana mboga za majani na samaki weuweeeeee angalau ni chakula ninayokula kila mara nne Kwa wiki.

Ugali mweupe kama yangeyange uwa sili kabisa
 
Ugali ni msosi poa tu. Huwezi kula bila mboga sababu hauna chumvi, mafuta wala sukari kama hivyo vingine. Ugali ni chakula chenye calories nyingi sana. Ekari moja ya mahindi inaweza kulisha watu wengi kuliko ngano, mpunga na nafaka nyingine yoyote ile.
 
Ugali uheshimiwe.. Tulioenda JKT miaka ile... mtakuwa mnanielewa.. Siku za mwanzo, kuna vislay vilikuja na biscuit, na vikawa havichukui ugali..Vinachukua maharage na kula na biscuit..Combania ilivyochanganya wote walinyooka kwenda kukimbilia mkombozi ugali, na makuruta waliokuwa na chati, ni wale walioweza kupata ugali wa ziada, au muda wote kuaccess source ya kupata ugali..
Inadhihirisha ugali ni muokozi halisi, ndio maana unaweza ukatumika maeneo yote , hayo mashuleni, jela, kwenye makambi nk..

Tuheshimu ugali
 
Ugali umekukosea wapi boss
 
Mbona ugali uko poa tu kunywea chai, ila lazima uubanike kwenye moto. Pia ukoko wa ugali ni mtamu kuliko pilau au chapati, ukiunyunyuzia mchuzi basi siku hiyo utakukurushana na sufuria mpaka majirani wasikie. Wenzako ugali unaliwa asubuhi badala ya chai, unaliwa mchana na pia unaliwa usiku, wali unaliwa wakati unasubiri ugali uive, familia hizi zina watoto si chini ya kumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…