SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
We
Mimi nisipokula ugali week huwa nahisi kuhaha na nitautafuta kokote unakopatikana niukule kwanza.

Ugali huwa ni mtamu sana licha ya kwamba hauliki bila mboga ila utamu wake huwezi kuuona kama unakula kwasababu hauna machaguo mengine ya vyakula kwa maana huo ndio unakopatikana kutokana na budget yako, hapo lazima ukuchoshe.

Na hapo kwenye kula na mboga au bila mboga nadhani inaweza kumake sense ila ni kama inakuja halafu inakataa kwa maana ugali unatokana na mahindi au muhogo sasa ukiangalia mahindi ni kwamba yanauwezo wakutoa vyakula vingi ambavyo mtu anaweza kula bila mboga na the same kwa mihogo.

Kwahiyo maybe kinachofanya ugali ushindwe kuliwa bila mboga ni zile hatua za uandaaji wake Kwahiyo inawezekana kama kungekua na namna tofauti ya kuuandaa ugali basi ungeweza kuliwa bila mboga, kwa maana ugali hauwekwi chumvi hauwekwi mavuta hauwekwi nyanya wala kitunguu wala nazi wala chochote kile kama vyakula vingine vinavyoliwa bila mboga ila wenyewe ni maji na unga tu shwaaaaaaaa unakitoa kituuuuuu 😆😆😆

Ugali uheshimiwe guys.
Bila shaka utakuwa unatokea mkoa wa mara maana watu wa mara na ugali utadhani umewekewa sukari
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Kweli ugali una punguza uwezo wa kufikiri ndo maana hata ww mleta mada uliyekula ugali umeleta mada ambayo hujaifanyia Tafiti. Wamarekani kutumia mahindi kuzalisha chakula cha wanyama haifanyi mahindi yanapoliwa na binadamu kushusha uwezo wa kufikiri. Labda uje na data za kukusapoti.

Lakini pia hata ukienda supermarket za wazungu mbona mahindi mabichi yako packed na yanaliwa vizuri Sana kwenye salads na matumizi mengine??
Hata ukienda kwenye vyuo vya wazungu huko ulaya na america wanaikimbiza kitaaluma ni waafrika
 
Nilishagundua hata wanyama wengi hawahufagilii kabisa ugali,ila kuna wakati wanakula tu bas kupoza njaa

Kuku,mbwa,nyau na nguruwe pamoja na kuwa huyu bwana hakosagi apetitte na anakula chochote lakin ugali huwa haupend kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
ndugu zangu tuwe na adabu katika mambo haya riziki sote humu tunajua ugali umetulea na kutukuza tulio wengi lakini baadhi wakipata hela wanasahau walikotoka kisa amepata uwezo wa kula anachotaka tusisahau pia watanzania wengi tunakula tulichojaaliwa kupata na sio tunacho kitamani isipokuwa wachache tu..la msingi shibe inapatikana sote tunakula ili tuishi maana shibe kuwa ni ile ile haina tofauti yoyote baina ya watu bila kujali umekula nini kwani hata uende kula lunch Dubai na mm ninaekula ugali bado wote tutaenda chooni na makimba yatafanana sasa tumezidiana nini hapo.! tuacheni dharau za kijinga kwa vyakula vilivyotukuza na kutulea kisa tumepata viji pesa tena usikute anayekula ugali ana afya nzuri na imara kuliko ww unayekula vinono vitamu tuweni na akiba ya maneno kwani kuna maisha baada ya leo unachokikashifu leo unaweza kihitaji siku za usoni kikunusuru kwenye njaa na usikipate kisa kashfa zako za leo..kama umepanda level ya kuchagua kula unachopenda na kukitamani mshukuru mungu ila wenzio mfumo umewabana unawachagulia wale nini kulingana na hali zao kiuchumi..hayo maneno ooh ugali chakula cha ajabu,ugali unadumaza akili..acheni dunia inazunguka hii tena wengine wana bahati babu na bibi zao kwa wazazi wapo hai ni ugali huu huu ndio umewakuza ila kijana umeshika pesa leo ndio full dharau kwa kilichokusitiri miaka kibao tuwe na shukran.
 
View attachment 3114645

Ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

Ni chakula maarufu zaidi kwenye sehemu za mateso kama jela, watoto wasiojitambua wanalishwa kinguvu.

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k,

hapo zamani watumwa walilishwa ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri, ni dawa iliyotumika kupunguza uwezo wa kufikiria (Thinking capacity), Mtu anaweza kuwa genius anaekula ugali lakini ilibidi awe mara 3 zaidi bila ugali.

kwa hapa nchini ukifuatilia sehem zinazotoa vichwa utagundua hawali sana ugali, lakini bado sio uwezo wao kamili kwasababu siku mbili au tatu za wiki wanakula ugali.

Mboga za majani na samaki wanaweza kuongeza akili lakini kosa linalofanywaa huwa ni kutumia ugali, nguvu ya ugali inaenda kuyeyusha / ku dilute virutubisho vya ubongo.

Ushauri wa bure kabisa, ukitaka kumuongezea mtoto uwezo wa akili usimzoeshe ugali, kiwe ni chakula cha kufanyia mazoezi ajifunze kufinya matonge ili ugenini asitie aibu.
Ukipika ugali wa ngano nae unadumaza akili?
 
Mimi nisipokula ugali week huwa nahisi kuhaha na nitautafuta kokote unakopatikana niukule kwanza.

Ugali huwa ni mtamu sana licha ya kwamba hauliki bila mboga ila utamu wake huwezi kuuona kama unakula kwasababu hauna machaguo mengine ya vyakula kwa maana huo ndio unakopatikana kutokana na budget yako, hapo lazima ukuchoshe.

Na hapo kwenye kula na mboga au bila mboga nadhani inaweza kumake sense ila ni kama inakuja halafu inakataa kwa maana ugali unatokana na mahindi au muhogo sasa ukiangalia mahindi ni kwamba yanauwezo wakutoa vyakula vingi ambavyo mtu anaweza kula bila mboga na the same kwa mihogo.

Kwahiyo maybe kinachofanya ugali ushindwe kuliwa bila mboga ni zile hatua za uandaaji wake Kwahiyo inawezekana kama kungekua na namna tofauti ya kuuandaa ugali basi ungeweza kuliwa bila mboga, kwa maana ugali hauwekwi chumvi hauwekwi mavuta hauwekwi nyanya wala kitunguu wala nazi wala chochote kile kama vyakula vingine vinavyoliwa bila mboga ila wenyewe ni maji na unga tu shwaaaaaaaa unakitoa kituuuuuu 😆😆😆

Ugali uheshimiwe guys.
mbona mahindi ya kuchemsha na kuchoma tunakula bila mboga
 
Back
Top Bottom