SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Ni kweli mleta mada hajaweka takwimu za kitaalamu hivyo basi hii inabaki kama mtazamo wake binafsi, kimsingi mahindi kama mahindi yana nutrition muhimu kwa kiwango kikubwa kabisa. Mfano food composition ya unga wa mahindi kwa 100g unapata; energy 363kcal, 8.4g of protein na 1.2g of fat. Ukilinganisha na unga wa ngano; energy 364kcal, 10.9g of protein, 1.1g of fat. Hapo tunaona utofauti ni mdogo sana.

Shida ni maandalizi yake, mahindi ni tofauti na ugali. Mara nyingi mahindi yanaliwa yakiwa freshy kabisa tofauti na ugali. Kwa mtazamo wangu na experience yangu binafsi, ugali unaharakisha mchakato wa kuleta usingizi. Sasa basi kama unaleta usingizi hapo tayari ni kisababishi cha kupunguza uwezo wa ufanisi kwa muda. Kama tunavyojua katika hali ya usingizi kunaambatana na uchovu na hali ya uchovu unaathiri utendaji wa ubongo.
Unataka umlishe pizza mbeba nguzo za Tanesko ??
 
View attachment 3114645

Ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

Ni chakula maarufu zaidi kwenye sehemu za mateso kama jela, watoto wasiojitambua wanalishwa kinguvu.

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k,

hapo zamani watumwa walilishwa ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri, ni dawa iliyotumika kupunguza uwezo wa kufikiria (Thinking capacity), Mtu anaweza kuwa genius anaekula ugali lakini ilibidi awe mara 3 zaidi bila ugali.

kwa hapa nchini ukifuatilia sehem zinazotoa vichwa utagundua hawali sana ugali, lakini bado sio uwezo wao kamili kwasababu siku mbili au tatu za wiki wanakula ugali.

Mboga za majani na samaki wanaweza kuongeza akili lakini kosa linalofanywaa huwa ni kutumia ugali, nguvu ya ugali inaenda kuyeyusha / ku dilute virutubisho vya ubongo.

Ushauri wa bure kabisa, ukitaka kumuongezea mtoto uwezo wa akili usimzoeshe ugali, kiwe ni chakula cha kufanyia mazoezi ajifunze kufinya matonge ili ugenini asitie aibu.
Mtoa mada ugali, wali, chapati zote ni chakula cha aina moja hebu chukua mda ujisomee kidogo kabla ya kuanzisha uzi
 
Nyie mnakosea sana, kinacholeta shida kwa mswahili sio kua ugali bali ni intake ndogo ya vyakula vya makundi vingine.

Ingetakiwa kwamba mtu ale ugali ukubwa wa ngumi yake na mboga iwe nyama nyingi au samaki mkubwa sana (protein).

Sasa mswahili anabugia li ugali likubwa kama kisado na mboga yenyewe ni maharage ya kuchemsha unategemea nini
 
Nbona mnatuchanganya nyie Ze Comedy, Kuna yule Demu wako wa Stand up comedy sijui ni mchungaji yule anasema

"Sipendi mwanaume anayekula wali"
 
Unaukosea heshima sana #UGALI kumbuka ugali umekukuza ndugu mwandish licha ya hivo ugal umekupa protin za kuzidi, yaa ugali nikitu ambacho dah sijui nisemeje nakumbuka kipind flan ambapo wewe, see more....
 
True story kabisa mkuu, hii kitu kuna namna inapunguza na kudidimiza uwezo wa kufikiri.
Uji wake ni jau vile vile huko mashuleni boarding hizi za kayumba ni mwendo wa kulala kwenye pindi la mathe baada ya kupiga porenga ni msala sana hii kitu.

Hallelujah!!!
Sasa anaedawa kuwa mwana wa Mungu,
kaingiaje tena kwenye 'Inshu' ya NGUNA??
 
Unaukosea heshima sana #UGALI kumbuka ugali umekukuza ndugu mwandish licha ya hivo ugal umekupa protin za kuzidi, yaa ugali nikitu ambacho dah sijui nisemeje nakumbuka kipind flan ambapo wewe, see more....
Unapaswa kushtakiwa kisha uhukumiwe adhabu ya kufanana na atakayopewa 'PIDIDI'.
Toka lini Ugali ukawa na 'Protini' au hujui maana ya protini?

Hiyo ni Elimu ya Sayansikimu ya Darasa la Tatu ujue.
 
Hv anajua ugal kitimoto uyu.
Au nyamachoma.


Alafu mbongo akishaenda nje akija utaanza kumsikia
Analeta kanuni za ulaji wa mambele bongo.
Anajiona mjaaanja
Mtu mwenyewe afya mbovu, tumbo limejaa,kutembea shida
Afya haieleweki.
Mtu fundi gereji anataka ale chips.
Achana nao,na wasitupangie
 
Ugali sio chakula ni basi tu limekosekana jina sahihi kuwakilisha hayo mauji uji.

Ukishaona msosi official wa jela ni ugali, ndio hapo ambapo unatakiwa ujifikirie mara mbili kujiuliza ugali ni nini na umefata nini jela.

Kumbuka jela ni sehemu ya mateso, kila chochote kinachofanyika kule ni kwa ajili ya kuwa sehemu ya hayo mateso.

Sera ya jela ni kuwa hawawezi kukupa chochote ambacho kitakufanya wewe ujisikie raha.

Sasa ugali kama ni chakula, umefikaje kule?

Kuna namna ambayo ugali unatumika kama instrument of torture sema bado watu hawajastukia tu.
Hili nalo neno
 
Back
Top Bottom