SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Tatizo wengi tunakariri. Ugali umeliwa enzi na enzi katika nchi nyingi tu za kiafrika, kabla hata hayo mahindi hayajaingia katika bara hili.
Nafikiri ni sahihi kuwaita hawa kama wanavyotakiwa kuitwa. Ni magaidi ya mitandaoni. Yani wanajisahaulisha kwa makusudi(Wanajizima data) . Ulaya wanakula Polente. Ni Ugali tu.😂😂😂 Wao ni kukandia kila kitu chenye Utamaduni na Asili ya Mwafrika.
Labda tatizo liwe kwa mahindi, sio ugali. Ugali uko wa aina nyingi, kulingana na unga uliotumika kuandaa. Kuna ugali wa muhogo, ugali wa mtama, ugali wa uwele na ugali wa unga wa mchele. Nasikia pia kuna ugali unaandaliwa kutokana na unga wa ndizi (migomba) japo sijawahi uona
Yaani kama ni Mahindi, basi Wazungu ndi waliodumazwa, kwani
Wakiamka, Cornflakes🤔 Itoshe, ukiwasikia Wanazuoni wa Ulaya huko na Marekani, utawasikia wakisema "I lived on Cornflakes and Noodles while at College"

Hapooo sasa.


.

Sasa iweje mtu akisema ugali basi mawazo yote yanafikiri mahindi tu? Ugali hauna tatizo, wenye tatizo ni waliokariri ugali unatokana na mahindi tu.

Halafu izingatiwe kuwa kula ugali kunaambatanishwa na mboga. Pamoja na ugali kukupa wanga, mboga nayo itakupatia protini, madini na vinginevyo vingi tu.
Hakika.
 
wali, ndizi, Pilau, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi,
Pamoja na kwamba sipendi wala kuushabikia ugali, lakini hakuna tofau kubwa kati ya ugali na vyakula hivyo ulivyovitaja hapo, hususani kwenye maendeleo na ukuaji wa binadamu (prenatal & postnatal growth).

Sababu ni kuwa hivyo vyakula vyote nina carbohydrates nyingi ambazo hazina kazi ya maana katika brain development.

Ningekusifu zaidi kama ungepigia chapuo watu kutumia zaidi vyakula vyenye asili ya protini kwa wingi huku vile vyenye asili ya wanga vikipewa kipaumbele cha mwisho kabisa
 
Binafsi napenda sana ugali lakini upikwe vizuri na moto mkali na usongeke, usiwe na nabija wala unga unga ninapokula.
Na mboga yoyote ile mlenda, majani au mchuzi, dagaa n.k

Lakini kuupenda kwangu hajui ndio ukweli kuwa huenda ni Chakula kinachodumaza akili.
Afrika yote common food no ugali , it is very unfortunate.
 
Inategemea unakula ugali wa aina gani
Mimi nasaga mwenyewe
Mahindi, mahindi ya njano lishe, muhogo, mchele na mbegu za maboga vyote nachanganya..

Huo ugali ni noma wazee
UGALI NI UGALI JEMBE UNAUREMBA SANA AISEE
 
Ugali ni msamisti wa nafaka iliosagwa. Hata mchele, ngano, mtama nk hutoa ugali.
Vilevile mihogo, ndizi nk nao hutoa ugali
Kama lengo lako ni kukataa ugali wa mahindi weka wazi. Ugali ni ubumifu wa waafrika warabu nk hawana ugali kwa sababu hawana ardhi ya kulima nafaka. Ukishindwa kula ugali kula viazi, ndizi, magimbi nk. Kula vyakula vya kunde kama bagia tambi nk.
Je usipo kula ugali wa aina yoyote mwili wako utaimarika kwa kazi ngumu za maisha yetu? Waafrika kazi zetu nyingi ni manual.
 
Hapa Kuna ulakini flani, nchi karibu zote hawali ugali, ila huku ukila ugali unaonekana wa asili,


Kwa tuliosoma shule za kibishi, mkishakunywa uji saa 4 vipindi vinavyofata ilikua kama kukamilisha ratiba tu, watu wamechoka kama wamekula visungura

True story kabisa mkuu, hii kitu kuna namna inapunguza na kudidimiza uwezo wa kufikiri.
Uji wake ni jau vile vile huko mashuleni boarding hizi za kayumba ni mwendo wa kulala kwenye pindi la mathe baada ya kupiga porenga ni msala sana hii kitu.

Hallelujah!!!
Nimekumbuka wakati nipo A level.. baada ya break ya asubuhi, asilimia 90 ya wanafunzi walikuwa wanasinziq kwa sababu ya kunywa uji


Ole uwe umepuliza yaani kunywa uji mkavu😃
Utajikuta umelala hadi unaota ndoto
 
Mahindi yametokea Ulaya ila wenzetu huko wanalishia ng'ombe. Hawali ugali ndo maana hata msamiati wa ugali ama makande kwa lugha zao hawana. Huku tulioletewa mahindi tumegeuza ndio chakula Kikuu, inamaana kabla hayajaja mahindi chakula Kikuu kilikua ni kipi na nini madhara ya kula ugali? Hapa inahitajika wataalamu wafanye utafiti
Sio kweli TZ au Aftica yote. Kigoma tumekulia ugali wa mihogo na magimbi na ndizi kwa mboga za xuwani, maharage, kunde na mboga mbiga. Mahindi hayaliwii sana. Usukumani vyakula ni vingi sena. Mtama, uwele, viazi vitamu. Mbeya wanakula sana ndizi, ndofani, wali na ugali wa mahindi ie watu wa mbeya hawapendi mtama japo unastawi .Wapogoro kwa wali huwaambii kitu.
Mikoa ya kati ndio wala ugali wakuu, hawana mbadala. Pwani wanakula sana wali, mihogo, viazi vitamu na vyakula vya kusindika kama mikate. Wakinga hula ngano nyeusi, viazi mviringo na ugali.
Watu wa kipato cha kati ugali wanakula zaidi mchana, usiku ni wali au take away kama maandazi, chapati.
Wanaoongoza kula ugali wa mahindi ni wanafunzi wa shule za boarding, hawa hamna mjadala. Wanasindikizia na maharage. 80% ni ugali maharage. Matunda hio ratiba haipo. Mwanafinxi wa boarding inaweza kuwa anaongoza kwa lishe duni.
 
View attachment 3114645

ugali umetulea na kutukuza tulio wengi lakini imefika wakati lazima tuweke mambo wazi, tufikirie nje ya box tuachane na ile misemo "la msingi shibe ipatikane ili tuendelee kuishi"

.................................

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, Pilau, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k, Ugali ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

Ni chakula maarufu zaidi kwenye sehemu za mateso kama jela, watoto wasiojitambua wanalishwa kinguvu ni kinyume na nature.

Mahindi yaliletwa Africa kutoka Ulaya mwaka wa 700, ni chakula kizuri kinapokuwa bado kibichi mfano kuandaa mahindi yaliyochomwa, kuchemsha, kande za mahindi mabichi, n.k. Shida ya ugali ni kusubiri mpaka mahindi yakauke na kuyasaga.

hapo zamani mahindi yalipoletwa kutoka ulaya, babu zetu walizoeshwa kula ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri na kuwaongezea nguvu za kufanya kazi mashambani, Mtu anaweza kuwa genius anaekula ugali lakini ilibidi awe mara 4 zaidi bila ugali.

Ushahidi / Proof kwa hapa nchini ukifuatilia makabila yanayotoa vichwa (Wakerewe, Wachaga, Wahaya, Wanyakyusa waliokulia vijijini) utagundua hawali sana ugali, na bado sio uwezo wao kamili kwasababu siku mbili au tatu za wiki wanafinya matonge ya ugali.

Ni kweli Mboga za majani na samaki huongeza akili lakini kosa linalofanywaa ni kuvila kwa ugali, huu ugali unayeyusha / ku dilute virutubisho.

Ushauri wa bure kabisa, Muweke mbali mtoto na ugali ili kumsaidia kutunza uwezo wa akili zake, ugali unadumaza zaidi akili utotoni hadi balehe kipindi ambacho ubongo unapanuka.
Kwa hiyo makande ni bora kuliko Ugali?
 
Chakula huendana na utamaduni, mila na desturi pia na mazingira ikiwemo upatikanaji...

Basi Wanaokula vyura na kono kono tungewaiga maana Wana akili sana kuliko sisi.
Wazungu wanalima sana mahindi ila wanaishiabkulisha nguruwe na ngombe,mahindi sio utamaduni wa mwafrika yaliletwa afrika kutokea bara la amerika ya kusini.

Chakula chetu cha asili ni mtama,ulezi,uwele mihogo.


Narudia tena ukiona chakula hakiliwi ulimwengu wa kwanza japo wanakilima jiulize vzri,wazungu sio wajinga,pay attention to small things.
 
Kims
Wanaongelea Virutibisho na manufaa ya chakula wewe unaongelea hizo Addiction zako za ugali ambazo ni sawa na yule mlevi ambaye asipolewa/kunywa kilevi anapagawa.

Wazazi wameharibu watoto kwa kuwaendekeza chakula cha aina moja, matokeo yake watoto nao wameshakuwa addicted na aina hiyo ya vyakula hata ambavyo havina faida kiafya.

Ndiomaana akili za Watanzania wengi zinazidi kuwa dumavu sababu ya ulaji wetu mbovu wa mazoea na ubishi wa kufuata madactari/washauri wa tiba.

Inaumiza kuona mpaka wasomi nao hawajui wale nini, kutwa kushinda na hayo mavyakula ambayo ni useless ktk miili yao.

Tuache mazoea.
KImsingi nmeacha kabisa kula ugali na shauri watu waendelee kuachana na matumizi ya ugali wa mahindi.
 
Aki
Baada ya kupitia michango ya watu wengi, nimeshutuka sana lakini pia nimegundua kuwa, tuna tatizo kubwa sana la uelewa wa masomo ya Sayansi. Kama mtu aliyefika kidato channe (hata kama ana D mbili) hana uwezo hata wa kutambua uzuri /umuhimu wa Ugali nafikiri tunatatizo kubwa.....
Hivi unataka, mafundi ujenzi, wakulima, wabeba mizigo, nk nk wale chips au piza???
Akili ndogo sana wewe,kwahiyo nchi nyingine ambazo hawali ugali wa mahindi hao mafundi ujenzi hula piza?
 
Mahindi yametokea Ulaya ila wenzetu huko wanalishia ng'ombe. Hawali ugali ndo maana hata msamiati wa ugali ama makande kwa lugha zao hawana. Huku tulioletewa mahindi tumegeuza ndio chakula Kikuu, inamaana kabla hayajaja mahindi chakula Kikuu kilikua ni kipi na nini madhara ya kula ugali? Hapa inahitajika wataalamu wafanye utafiti
Hili limesha jadiliwa humu several times..

Kwa kuongezea nafaka ya ugali ni chakula Cha kuwaulia wanyama walio shindikana ie. Marekani

Screenshot_20241005-091550.png
 
Back
Top Bottom