SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Hapa Kuna ulakini flani, nchi karibu zote hawali ugali, ila huku ukila ugali unaonekana wa asili,


Kwa tuliosoma shule za kibishi, mkishakunywa uji saa 4 vipindi vinavyofata ilikua kama kukamilisha ratiba tu, watu wamechoka kama wamekula visungura
Wenzetu east africa wanakula but si mahindi. Ni mihogo na nafaka nyingine which zina virutubisho vingi

Ugali wa huku ni tatizo, most of the time hauna virutubisho, ila sababu ndio low cost food na ni available kwa wingi inawa force watu kukimbilia huko
 
H
View attachment 3114645

ugali umetulea na kutukuza tulio wengi lakini imefika wakati lazima tuweke mambo wazi, tufikirie nje ya box tuachane na ile misemo "la msingi shibe ipatikane ili tuendelee kuishi"

.................................

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, Pilau, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k, Ugali ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

Ni chakula maarufu zaidi kwenye sehemu za mateso kama jela, watoto wasiojitambua wanalishwa kinguvu ni kinyume na nature.

Mahindi yaliletwa Africa kutoka Ulaya mwaka wa 700, ni chakula kizuri kinapokuwa bado kibichi mfano kuandaa mahindi yaliyochomwa, kuchemsha, kande za mahindi mabichi, n.k. Shida ya ugali ni kusubiri mpaka mahindi yakauke na kuyasaga.

hapo zamani mahindi yalipoletwa kutoka ulaya, babu zetu walizoeshwa kula ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri na kuwaongezea nguvu za kufanya kazi mashambani, Mtu anaweza kuwa genius anaekula ugali lakini ilibidi awe mara 4 zaidi bila ugali.

Ushahidi / Proof kwa hapa nchini ukifuatilia makabila yanayotoa vichwa (Wakerewe, Wachaga, Wahaya, Wanyakyusa waliokulia vijijini) utagundua hawali sana ugali, na bado sio uwezo wao kamili kwasababu siku mbili au tatu za wiki wanafinya matonge ya ugali.

Ni kweli Mboga za majani na samaki huongeza akili lakini kosa linalofanywaa ni kuvila kwa ugali, huu ugali unayeyusha / ku dilute virutubisho.

Ushauri wa bure kabisa, Muweke mbali mtoto na ugali ili kumsaidia kutunza uwezo wa akili zake, ugali unadumaza zaidi akili utotoni hadi balehe kipindi ambacho ubongo unapanuka.
Hapo umeshinda mkeka wa laki tu
 
Kuwaulia how? sijakuelewa hapo mjukuu wangu
Tizama IQ za Wala ugali popote pale duniani. Ugali ni symbol ya udumavu wa akili,fikra, maono, upeo unajua ugali ni symbol ya UMASKINI.

Nirudi kwenye hoja ugali for years umetumika Kama silaha ya kuangamiza jamii maskini hapa ulimwenguni ili zizidi kua duni zaidi
 
Ushauri wa bure kabisa, Muweke mbali mtoto na ugali ili kumsaidia kutunza uwezo wa akili zake, ugali unadumaza zaidi akili utotoni hadi balehe kipindi ambacho ubongo unapanuka.
1728289200598.png

Nilikula ugali karibu kila siku, form one mpaka form four, na form five hadi six, na JKT, na UD nilienda na nilikuwa kipanga tu. Sasa sijui unataka kuniambia nini? Kwamba nisingekula ugali ningekuwa zaidi ya Einstain?
 
Ugali wenyewe tunaukoboa na kutupa protini yote, tunakula wanga mtupu.

Lile dona ndo lina virutubisho vya protini, ugali mweupe ni wanga mtupu, energy tu, hauna virutubisho.
Virutubisho tafuta kwenye mboga.. ugali iwe kwa ajili ya starch tu
 
Virutubisho tafuta kwenye mboga.. ugali iwe kwa ajili ya starch tu
Dunia ya leo ni ya kufanya mambo mengi kwa pamoja.

Starch ni empty calories. Kwa watu wanaohesabu calories zao ni bora kupata calories zenye virutubisho.

Ina minimize caloric intake na ku maximize nutrients per calorie.

That is the idea behind my point.
 
Nikitoka nje ya nchi nitaukumbuka sana ugali siwezi kupitisha week sijala ugali....ugali ni mboga Yako hauna maringo umauweka vyote na mboga yoyote ni kama k tu hakuna namna itawekwa ishindikane[emoji41] naomba Nisamehewe kama Kuna mtu nimemkwaza.
 
Nikitoka nje ya nchi nitaukumbuka sana ugali siwezi kupitisha week sijala ugali....ugali ni mboga Yako hauna maringo umauweka vyote na mboga yoyote ni kama k tu hakuna namna itawekwa ishindikane[emoji41] naomba Nisamehewe kama Kuna mtu nimemkwaza.
Wewe ni mtu wa kanda ya ziwa au nyanda za juu kusini??
 
Ugali unalika bila mboga mkuu sema kwa nyie wala sembe ndio hamuwezi kula bila mboga.
 
Ugali sio chakula ni basi tu limekosekana jina sahihi kuwakilisha hayo mauji uji.

Ukishaona msosi official wa jela ni ugali, ndio hapo ambapo unatakiwa ujifikirie mara mbili kujiuliza ugali ni nini na umefata nini jela.

Kumbuka jela ni sehemu ya mateso, kila chochote kinachofanyika kule ni kwa ajili ya kuwa sehemu ya hayo mateso.

Sera ya jela ni kuwa hawawezi kukupa chochote ambacho kitakufanya wewe ujisikie raha.

Sasa ugali kama ni chakula, umefikaje kule?

Kuna namna ambayo ugali unatumika kama instrument of torture sema bado watu hawajastukia tu.
Aisee mkuu umetisha sana yaani nimesima hii comment nacheka mwenyewe njiani
 
Mleta mada ni Gen Z! Siyo Bure!
Eti anasema ugali bila mboga hauliki akifananisha na mkate sijui maandazi??... Hivi hayo maandazi au mkate unaoutetea, uliwahi kuula ukiwa hauna chumvi au sukari? Ugali wa mtama au uwele nao vipi? Unalika bila mboga siyo?
Hebu kuwa serious
 
Ninao ushahidi ila kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu sitoweza kuziweka hapa....ila ukae ukijua kitaaluma we africans tupo vizuri mno kuliko race nyingi tu!
Chinese mzee wanakimbiza sana ktk STEM
 
Nilishagundua hata wanyama wengi hawahufagilii kabisa ugali,ila kuna wakati wanakula tu bas kupoza njaa

Kuku,mbwa,nyau na nguruwe pamoja na kuwa huyu bwana hakosagi apetitte na anakula chochote lakin ugali huwa haupend kabisa
Kweli mkuu, yale ni kama makapi flani hivi. Nakumbuka mbwa wetu alikua ukiweka ugali na nyama atakula nyama then atafyonza mchuzi alafu atasepa zake.
 
Back
Top Bottom