SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
=
Twende kwa facts,

## Mchango wa Vinasaba na Mazingira katika IQ ya Mwanadamu

IQ (Intelligence Quotient) ya mwanadamu inategemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na vinasaba na mazingira. Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba lishe bora, hasa katika kipindi cha utoto, ina umuhimu mkubwa katika kuathiri IQ na uwezo wa utambuzi wa watoto.

**** Vinasaba na IQ

Vinasaba vina jukumu muhimu katika kuamua uwezo wa akili wa mtu binafsi. Hata hivyo, mazingira yanayomzunguka mtu, ikiwa ni pamoja na lishe, yanaweza kubadilisha au kuimarisha athari hizi. Kwa mfano, watoto walio na historia ya familia ya matatizo ya akili wanaweza kuwa na hatari zaidi ya kupata IQ ya chini, lakini mazingira bora yanaweza kusaidia kupunguza hatari hii.

**** Athari za Lishe

1. Lishe Duni: Utafiti umeonyesha kuwa ukosefu wa virutubisho muhimu kama protini, madini, na vitamini unahusishwa na kiwango cha chini cha IQ. Watoto wanaokosa lishe bora mara nyingi wanakabiliwa na changamoto za utambuzi na kujifunza[3][4].

2. Mchango wa Lishe Bora: Utafiti mmoja ulionyesha kwamba watoto wanaokula a breakfast mara kwa mara wana kiwango cha juu cha IQ ikilinganishwa na wale wanaokosa breakfast. Walio na chakula bora walionyesha ongezeko la alama za IQ kati ya 5 hadi 6[7].

3. Matokeo ya Utapiamlo: Utapiamlo unachangia kupungua kwa uwezo wa kujifunza na kukumbuka. Watoto walio katika mazingira yasiyo bora ya lishe wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kuwa na IQ ya chini[5][6].

**** Mifano ya Utafiti

- Utafiti wa Denmark: Utafiti uliofanywa nchini Denmark uligundua kuwa uzito wa kuzaliwa na ukuaji wa mtoto katika miezi ya mwanzo una uhusiano mzuri na IQ. Watoto walionyesha ongezeko la alama za IQ kulingana na uzito walioupata katika kipindi cha utotoni[8].

- Utafiti kuhusu Lishe: Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa watoto wanaopata lishe bora tangu utotoni huwa na uwezo mzuri wa kujifunza, huku wale walio kwenye mazingira magumu wakikabiliwa na changamoto kubwa za kisaikolojia[4][6].

Kwa ujumla, ni dhahiri kwamba IQ ya mwanadamu inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mchanganyiko wa vinasaba na mazingira, hasa lishe anayopewa mtoto tangu utotoni. Hivyo basi, kuwekeza katika lishe bora ni muhimu kwa maendeleo bora ya akili ya watoto.
Code:
Citations:
[1] https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/36854137/
[2] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC11428586/
[3] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC10877903/
[4] https://www.semanticscholar.org/paper/8286b8e9783cf62f5019970848e3e782098783db
[5] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC8894195/
[6] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC9857183/
[7] https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/31224517/
[8] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7326594/
=
Je kwa upande wako waweza kutupatia chanzo au uthibitisho wa hiki ulichokiandika?
Kwanini wakoloni walituletea mahindi wakati kwao ni chakula cha mifugo ?
 
Ugali sio chakula cha kitamaduni wala asili kwa mwafrika, TULIPIGWA. wakoloni walituletea mahindi wakati kwao ni chakula cha mifugo ? inakuingia akilini kweli ?


Huu ugalii tumeanza kuula baada ya wakoloni kuleta mahindi, tulipumbazika kwamba unashibisha haraka na kuleta nguvu.

Vyakula vyetu vya asili ni Magimbi, Ulezi, Mtama, Ndizi, samaki, Senene, Nyama choma, n.k.

Propaganda zimesambazwa tangu enzi za ukoloni kuusifia ugali unaleta nguvu huku suala la akili likipuuzwa, mwili wa binadamu wenye nguvu bila akili kuna tofauti ndogo sana na wanyama, atawaza zaidi kuzaliana, kuridhika haraka, kukosa malengo, ya muda mrefu, starehe, n.k.

UNABISHA ?? Chunguza vizuri hata kwa hapa Tz wasomi wengi wanatokea mikoa ambayo hawakuacha kutumia vyakula vya asili Kuanzia kinara wao Ukerewe, Unakuja Kilimanjaro, Unaenda Kagera, Unashuka Mbeya lakini nao wameanza kuushobokea ugali, wajitafakari.

Mtoto anaweza kuzalwa na IQ ya 300 lakini ugali unamshusha hadi 200, ni kweli anaweza kuwa na akili sana lakini huo sio uwezo wake halisi, uwezo wake original ilibidi uwe zaidi.

Kuchanganya ugali na vyakula vinavyoongeza akili kama samaki na mboga za majani ni sawa na kutumia ndoo yenye tobo kuchota maji kisimani. unaingiza madini lakini yanaharibiwa na ugali.
Katika maadui wetu wa taifa tulio aminishwa tangu uhuru ni UJINGA, UMASKINI NA MARADHI Sasa tuna janga lingine ambalo ni adui wa taifa ambalo ni UGALI.

Tuanzishe campaign.
#stop using ugali
#ugali is destroy IQ
#BAN UGALI FOR BRAIN 🧠 HEALTH
#
 
Kwani huo ugali unaula bila ya mboga ? Wenzako tunapokula ugali tua angalia zaidi mboga mfano ugali na samaki na njegere na tembere au mchicha pamoja na kachumbali nk .....labda wewe unakula ugali na picha ya samaki(wapale style) ndiyo maana unakuwa na mapungufu hadi ya akili ....wataalamu tunasema ugali ni mboga..
Kwani ukila ugali na samaki au nyama choma au na tembere sindiyo hayo hayo unayotaka .....songa ugali ....pika na mboga 7 na mtindi pembeni ....tumia akili wacha kulalamika kama mwanamke mpumbavu
.
 

Attachments

  • 20241109_135001.jpg
    20241109_135001.jpg
    593.5 KB · Views: 2
Lakini sio lazima sana kula ugali wa mahindi,sisi tuna ugali wa ndizi zilizoanikwa zikakauka vizuri na mihogo,kuna ugali wa mtama,uwele
 
Unakula chakula cha kulishia nguruwe na bata halafu ujidanganye utapata Iq ya kupiga hesabu kali za kubuni vyombo vya kwenda mars na mwezini .
Never
 
Back
Top Bottom