SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Mahindi hapà East Afrika yaliletwa na mreno ,mahindi sio zao la asili la hapà Africa ni zao la asili ya huko Amerika kusini huko na ndiko huko inatumika kama chakula cha mifugo mpaka leo , wanalishwa ng'ombe ,punda ,farasi , nguruwe ,kuku ,Bata nk ili kupata nyama na hawali hili zao kwa kiasi kikubwa , wanakula ngano sana ,nyama ,maziwa ,matunda na mbogamboga
Sisi huku ndio staple food sasa ,ujinga .
Ilibidi watu tulime sana ngano na tupate chakula cha kueleweka maana bei za ngano zitakuwa himilivu na mwishowe watu wataondokana na huu utapia mlo wa kula vyakula vya mifugo
 
Tatizo ni sembe, dona na mahindi mabichi ni vyakula bora
 
Kwani ukila ugali na kupata nguvu, kesho yake huwezi kula hivyo vingine ukapata akili? Kwani unakula hicho hicho kila siku.

Hiyo mikoa uliyotaja, jaribu kuchunguza, ile dini haipo kwa wingi.., ila angalia sehemu zote zenye ile dini kwa sana, mfano Lindi na Mtwara…, yaani popote penye ile dini, bila kujali wanakula nini, lazima IQ iwe ndogo.
 
Wasukuma mnisamahe ila ukweli lazima tuuweke wazi
MKuu Mimi siyo Msukuma!

Mimi ni Mkurya kutoka wilaya ya Tarime Kijiji Cha Mogabiri !

SWALI KWAKO MLETA MADA

Unazungumzia Ugali wa Aina gani?,kwasababu ugali upo wa aina tofauti tofauti!

1.Upo Ugali unaotokana na Unga wa Ubuyu

2.Upo Ugali unaotokana na mchanganyiko wa nafaka (Mahindi,Mtama,Muhogo,Uwele na Ulezi) huu uitwa DONA

3.Upo Ugali unaotokana na mchele

4.Upo Ugali unaotokana na Viazi vikavu (Michembe)

5.Upo ugali unaotokana na kuchujwa Kwa nafaka (SEMBE)

Sijajua wewe unazungumzia Ugali UPI kati ya GALI nilizoziainisha hapo!

Mkuu Uncle bright hebu fafanua Ili nikupe nondo zenye Ujazo ,ninapaswa nichomoe vitu kadhaa kwenye Ubongo wangu niliotunukiwa na Mungu ili ukusaidie kuelewa na Kuwa na ufahamu!

Haya nakusubiri!
 
Sasa kama unaleta nguvu kwanini tusile? Hatujafikia level ya kutotumia nguvu mkuu! Unataka watu wafe njaa? Au hujui mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe?

Ugali mnausingizia IQ kubwa ni kama kipawa kuna mtu anakua nacho hata ale ugali usiku na mchana siku 365 atakua na IQ kubwa tu mana mtu wa aina hio huwaga ni mdadisi elimu haimtafuti anaitafuta mwenyewe.
 
Na huo ugali wa mtama pia walileta wao?
ni ushamba watu kudhani ugali ni mahindi pekee!

mtama na uwele unafaa kuliko ngano wanayokula wao!

nasema tu mwafrika hana akili Tu wala si chakula.

ulaya wamejenga na kutengeneza teknolojia mbalimbali kabla ya kuja afrika,hem angalia afrika walikuwa na nini kabla ya ukoloni?

hata barabara haikuwepo,wanakaa nyumba za tope,wachawi,kunywa pombe na mkuu wa wachawi kijijini ndio anapewa uchifu wakati ulaya wachawi walikuwa wanauawa.

Kuna nyumba za gorofa ulaya,na Asia zenye miaka 200+ na zipo imara,zimejengwa na wazee wao miaka hiyo,Sisi wazee wetu wakiwa wanawapenda machifu wao hadi kuamua chifu akifa mtu aliye hai azikwe nae,hizo ndio akili walikuwa nazo bila ugali.

Ulaya mashariki kuna sehemu wanatumia mahindi,na IQ ziko sawa.

Leo mwandishi aseme kisa ugali?,na kwa IQ yake anajua ugali ni mahindi pekee,anashindwa kutambua hata mkate ni ugali wa ngano na mafuta kidogo.

Mahindi yanalimwa ili mifugo wale yale majani si nafaka,tusikariri.
 
Upo sawa kabisa
Anadhani ulaya wameendelea overnight tu

Jamaa walikuwa wajinga kama sisi na wakaukataa ujinga wametoka mbali sana sana before hata kuja huku Africa

Halafu bado ngano anaona ni sawa tu?
 
View attachment 3148384

View attachment 3148392
View attachment 3148393
View attachment 3148394

Mahindi hapà East Afrika yaliletwa na mreno, mahindi sio zao la asili la hapà Africa ni zao la asili ya huko Amerika ya kusini wao huyatumia thankkama chakula cha mifugo mpaka leo, wanalishia ng'ombe ,punda ,farasi , nguruwe ,kuku ,Bata nk ili kupata nyama.

Huu ugalii tumeanza kuula baada ya wakoloni kuleta mahindi, tulipumbazika kwamba unashibisha haraka na kuleta nguvu.

Vyakula vyetu vya asili ni Magimbi, Ulezi, Mtama, Ndizi, samaki, Senene, Nyama choma, n.k.

Propaganda zimesambazwa tangu enzi za ukoloni kuusifia ugali unaleta nguvu huku suala la akili likipuuzwa, mwili wa binadamu wenye nguvu bila akili kuna tofauti ndogo sana na wanyama, atawaza zaidi kuzaliana, kuridhika haraka, kukosa malengo, ya muda mrefu, starehe, n.k.

UNABISHA ?? Chunguza vizuri hata kwa hapa Tz wasomi wengi wanatokea mikoa ambayo hawakuacha kutumia vyakula vya asili Kuanzia kinara wao Ukerewe, Unakuja Kilimanjaro, Unaenda Kagera, Unashuka Mbeya lakini nao wameanza kuushobokea ugali, wajitafakari.

Mtoto anaweza kuzalwa na IQ ya 300 lakini ugali unamshusha hadi 200, ni kweli anaweza kuwa na akili sana lakini huo sio uwezo wake halisi, uwezo wake original ilibidi uwe zaidi.

Kuchanganya ugali na vyakula vinavyoongeza akili kama samaki na mboga za majani ni sawa na kutumia ndoo yenye tobo kuchota maji kisimani. unaingiza madini lakini yanaharibiwa na ugali.
Ugali siyo chakula salama kwa afya ya akili na mwili. Upande wa afya ya mwili kulaa ugali ni hatari mara 5 zadi ya kunywa soda.
Ugali unapaswa kuliwa kidogo sana ili kuuwezesha mwili kupata nishati, mboga inapaswa kuwa nyingi kuliko ugali, lakini siyo kuula kwa ndalilo kama watu wanavyoula.
 
Ama kweli ugali hauongezi akili 😅😅

Mla ugali mwenzetu anakuambia tusile ugali ila tule magimbi, ndizi 😅😅
 
View attachment 3148384

View attachment 3148392
View attachment 3148393
View attachment 3148394

Mahindi hapà East Afrika yaliletwa na mreno, mahindi sio zao la asili la hapà Africa ni zao la asili ya huko Amerika ya kusini wao huyatumia kama chakula cha mifugo mpaka leo, wanalishia ng'ombe ,punda ,farasi , nguruwe ,kuku ,Bata nk ili kupata nyama.

Huu ugalii tumeanza kuula baada ya wakoloni kuleta mahindi, tulipumbazika kwamba unashibisha haraka na kuleta nguvu.

Vyakula vyetu vya asili ni Magimbi, Ulezi, Mtama, Ndizi, samaki, Senene, Nyama choma, n.k.

Propaganda zimesambazwa tangu enzi za ukoloni kuusifia ugali unaleta nguvu huku suala la akili likipuuzwa, mwili wa binadamu wenye nguvu bila akili kuna tofauti ndogo sana na wanyama, atawaza zaidi kuzaliana, kuridhika haraka, kukosa malengo, ya muda mrefu, starehe, n.k.

UNABISHA ?? Chunguza vizuri hata kwa hapa Tz wasomi wengi wanatokea mikoa ambayo hawakuacha kutumia vyakula vya asili Kuanzia kinara wao Ukerewe, Unakuja Kilimanjaro, Unaenda Kagera, Unashuka Mbeya lakini nao wameanza kuushobokea ugali, wajitafakari.

Mtoto anaweza kuzalwa na IQ ya 300 lakini ugali unamshusha hadi 200, ni kweli anaweza kuwa na akili sana lakini huo sio uwezo wake halisi, uwezo wake original ilibidi uwe zaidi.

Kuchanganya ugali na vyakula vinavyoongeza akili kama samaki na mboga za majani ni sawa na kutumia ndoo yenye tobo kuchota maji kisimani. unaingiza madini lakini yanaharibiwa na ugali.

Inabidi utambue maana kwanza ya neno ugali. Pia utambue kuna ugali wa aina nyingi.
Ugali ni unga ulikorogwa kwenye maji ya moto na kuchanganyika. Sasa unaweza kutumia unga wa aina tofauti tofauti. Kama unga wa mchele. Mtama, magimbi, mihogo, ngano, ndizi, viazi nk.

Wanigeria, Ghana, Gambia, Senegal nk wanakula ugali wanaita gari, au pounded yam. (Magimbi)

Wazungu, waarabu wanakula ugali mkavu, uliokaushwa unaitwa macaroni, pasta unachanganywa na mboga. Mkate ni ngano,unga ulichangwa na maji na vitu vingine viwili vitatu.

Wahindi, Waarabu wanakula ugali mkavu ngano, Naan bread, inachanganywa na maji, halafu inakaangwa.

Ngano, mahindi, viazi, mchele, vyote hivyo ni wanga. Kupata minerals inategemea na utayarishaji wako kutoka shambani.
 
Back
Top Bottom