SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Ugali ni hata vitamini na madini hauna,
Je unazungumzia ugali upi? kulingana na mchanganuo wa UMUGHAKA
:AweeWoo:
1.Upo Ugali unaotokana na Unga wa Ubuyu

2.Upo Ugali unaotokana na mchanganyiko wa nafaka (Mahindi,Mtama,Muhogo,Uwele na Ulezi) huu uitwa DONA

3.Upo Ugali unaotokana na mchele

4.Upo Ugali unaotokana na Viazi vikavu (Michembe)

5.Upo ugali unaotokana na kuchujwa Kwa nafaka (SEMBE)
 
Kwa nini ugali huwa hauliwi kwenye sherehe??
 
MKuu Mimi siyo Msukuma!

Mimi ni Mkurya kutoka wilaya ya Tarime Kijiji Cha Mogabiri !

SWALI KWAKO MLETA MADA

Unazungumzia Ugali wa Aina gani?,kwasababu ugali upo wa aina tofauti tofauti!

1.Upo Ugali unaotokana na Unga wa Ubuyu

2.Upo Ugali unaotokana na mchanganyiko wa nafaka (Mahindi,Mtama,Muhogo,Uwele na Ulezi) huu uitwa DONA

3.Upo Ugali unaotokana na mchele

4.Upo Ugali unaotokana na Viazi vikavu (Michembe)

5.Upo ugali unaotokana na kuchujwa Kwa nafaka (SEMBE)

Sijajua wewe unazungumzia Ugali UPI kati ya GALI nilizoziainisha hapo!

Mkuu Uncle bright hebu fafanua Ili nikupe nondo zenye Ujazo ,ninapaswa nichomoe vitu kadhaa kwenye Ubongo wangu niliotunukiwa na Mungu ili ukusaidie kuelewa na Kuwa na ufahamu!

Haya nakusubiri!
Ugali wa mahindi
 
Chakula na vina Saba ni tofali Mazingira yanasimama Kama mjenzi.
Kama Akili huna angalia hata waliokuzunguka kama wanazo au mambugila tu .
 
Mahindi hapà East Afrika yaliletwa na mreno, mahindi sio zao la asili la hapà Africa ni zao la asili ya huko Amerika ya kusini wao huyatumia kama chakula cha mifugo mpaka leo, wanalishia ng'ombe ,punda ,farasi , nguruwe ,kuku ,Bata nk ili kupata nyama, wao wakila mahndi basi ni mara chache yale mabichi ya kuchemsha au kuchoma.

Huu ugalii tumeanza kuula baada ya wakoloni kuleta mahindi, tulipumbazika kwamba unashibisha haraka na kuleta nguvu.

Vyakula vyetu vya asili ni Magimbi, Ulezi, Mtama, Ndizi, samaki, Senene, Nyama choma, n.k.

Propaganda zimesambazwa tangu enzi za ukoloni kuusifia ugali unaleta nguvu huku suala la akili likipuuzwa, mwili wa binadamu wenye nguvu bila akili kuna tofauti ndogo sana na wanyama, atawaza zaidi kuzaliana, kuridhika haraka, kukosa malengo, ya muda mrefu, starehe, n.k.

UNABISHA ?? Chunguza vizuri hata kwa hapa Tz wasomi wengi wanatokea mikoa ambayo hawakuacha kutumia vyakula vya asili Kuanzia kinara wao Ukerewe, Unakuja Kilimanjaro, Unaenda Kagera, Unashuka Mbeya lakini nao wameanza kuushobokea ugali, wajitafakari.

Mtoto anaweza kuzalwa na IQ ya 300 lakini ugali unamshusha hadi 200, ni kweli anaweza kuwa na akili sana lakini huo sio uwezo wake halisi, uwezo wake original ilibidi uwe zaidi.

Kuchanganya ugali na vyakula vinavyoongeza akili kama samaki na mboga za majani ni sawa na kutumia ndoo yenye tobo kuchota maji kisimani. unaingiza madini lakini yanaharibiwa na ugali.
Mtoto yupi huyo aliyewahi kuzaliwa na IQ ya 300 duniani?

Natamani nimuone au nimsikie na kumsoma tu.
 
View attachment 3148384

View attachment 3148392
View attachment 3148393
View attachment 3148394

Mahindi hapà East Afrika yaliletwa na mreno, mahindi sio zao la asili la hapà Africa ni zao la asili ya huko Amerika ya kusini wao huyatumia kama chakula cha mifugo mpaka leo, wanalishia ng'ombe ,punda ,farasi , nguruwe ,kuku ,Bata nk ili kupata nyama, wao wakila mahndi basi ni mara chache yale mabichi ya kuchemsha au kuchoma.

Huu ugalii tumeanza kuula baada ya wakoloni kuleta mahindi, tulipumbazika kwamba unashibisha haraka na kuleta nguvu.

Vyakula vyetu vya asili ni Magimbi, Ulezi, Mtama, Ndizi, samaki, Senene, Nyama choma, n.k.

Propaganda zimesambazwa tangu enzi za ukoloni kuusifia ugali unaleta nguvu huku suala la akili likipuuzwa, mwili wa binadamu wenye nguvu bila akili kuna tofauti ndogo sana na wanyama, atawaza zaidi kuzaliana, kuridhika haraka, kukosa malengo, ya muda mrefu, starehe, n.k.

UNABISHA ?? Chunguza vizuri hata kwa hapa Tz wasomi wengi wanatokea mikoa ambayo hawakuacha kutumia vyakula vya asili Kuanzia kinara wao Ukerewe, Unakuja Kilimanjaro, Unaenda Kagera, Unashuka Mbeya lakini nao wameanza kuushobokea ugali, wajitafakari.

Mtoto anaweza kuzalwa na IQ ya 300 lakini ugali unamshusha hadi 200, ni kweli anaweza kuwa na akili sana lakini huo sio uwezo wake halisi, uwezo wake original ilibidi uwe zaidi.

Kuchanganya ugali na vyakula vinavyoongeza akili kama samaki na mboga za majani ni sawa na kutumia ndoo yenye tobo kuchota maji kisimani. unaingiza madini lakini yanaharibiwa na ugali.
Mnadangayana tu mahindi ndio chakula kikubwa hata Huko Ulaya. Moja ya sababu Wamarekani wana unene kupita Kiasi ni ulaji wa Mahindi kupindukia. Sababu wao hawali ugali haimaanishi Hawali mahindi.

Vile vyakula vitamu vitamu vya wazungu unavyoona supermarket kama Vile biskuti, Cereal, Sukari, makaroni, wafers na vingine vingi ni mahindi.

On average mmarekani anakula kama gram 200-250 hivi za Mahindi kila siku.
 
Huu ni uongo
 
Kasomea historia , mreno kaleta ugali 1600 ukoloni umeingia 1800 , mmelishwa ugali Kwa miaka 200
Sasa kama walikuwa na IQ kubwa waliwezaje kuacha asili Yao ya kula mizizi na kichutumia vyakula vya wageni?
 
Kweli mti wenye matunda hupigwa mawe, yani niache kula ugali dagaa wa ku rost na mtindi, serious? you must be out of ur mind.
 
Back
Top Bottom