SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa
Unajua watanzania tunaona Kwa sababu ugali ni mgumu basi tunaona ndio unatufanya tuwe wagumu na miguvu, lakini hamna chochote. Bora wanaokunywa urojo wanapata virutubisho vya aina mbalimbali lakini ugali ni wanga Tu.
 
Nini kilitangulia kati ya wakoloni na kilimo cha mahindi,.!?,nyie watu mna matatizo kichwani hata kutumia google hamjui. Ila mna justify upumbavu wenu kwasababu nyepesi nyepesi..
Mbona kama unateseka sana?
Hujaambiwa usile ugali, kama unaona ni mchongo we fakamia tu.... ila ukae ukijua unakula chakula cha mufugo.
 
Hivi hizi Pumba munazoshusha hapa JF huwa munazitolea wapi?
 
Na sehemu wakoloni waliyokuja kumaliza mchezo kwa kuwavuruga akili mazima wazee wetu ni pale walipoingia porini kutafuta majani yanayoteleza na kuyapa jina la mlenda na kufanya hiyo ndio combinations bora ya mlo wa ugali.
Usielewe hata ukichanganya bamia na mboga ya maboga unatengeneza mlenda! Poor you.
Muda mwingine punguzeni ujuaji
 
Mihogo na mtama vilikuja karne ipi?
 
Na hivyo vyakula vyao ndo vinawafanya kuwa laini laini na kuwapa hamu ya kufukuliwa nyuma na kuwapa akili za kutambua haki za Mashoga, endelea kuika damiza familia yako kwa kuleta uzungu wa kishamba
 
Aiii sikuwahi kujua ugali ni mbaya kiasi hiki..
 
Habari Mtoa Mada ngara23
Unaweza kuwa unahoja lakini uwasilishaji wako Ukavuruga hata maana ya amada yako uliyoitoa..

Ni kweli kuna baadhi ya vitu unaweza ukawa ulisema kweli..

Kama uliposema (Ntanukuu)

"Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli"

Hili ni Kweli kabisa watu wengi wanaamini hivyo Ilihali si kweli...Kuna vyakula vingine vya kuupa Mwili nguvu vya kiasili kama magimbi,Viazi aina zote,Mihogo n.k

Hilo ni jambo ambalo kati ya yote Ndilo uliloelezea ukweli mengine ila mengine yanatia mashaka

MisInformation Ulizotoa Kuhusu Ugali

  • KUHUSU SUMU Na KUWA UGALI HAUNA NUTRIENTS ZOZOTE
Ugali Ni Sumu , Jibu "Partially True and Partially false "Ni ukweli na pia ni Uongo"

ni kweli kwamba kuna baadhi ya mahindi, Unga na hata ugali una chembe chembe za Heavy metal ambazo ni mycotoxins zinazoitwa Aflatoxins au kwa jina jingine Aspergillus flavus zipo kiwango kidogo sana yaani (μg g−1)..

Japo kama utakula Wingi sana wa mahindi na ugali wenye chembe za Aflatoxin..Utapata Kitu kinaitwa kitaalam aflatoxicosis..
Ambazo inaweza kukusababishia maradhi mengine kama cancer, Infertility, organ failure hasa Kidney..

Lakini Angalizo ni kuwa Si kila Ugali au kila unga unakuwa na Mycotoxin mpaka uwe umekula Mahindi au Ugali wenye Toxin hiyo ndo utapata hayo maradhi...


Lakini kwa Tanzania Kuna case ambazo.ni chini ya 2% ya wagonjwa wote waliowahi kutibiwa kwa kupata Aflatoxicosis...
Kwahyo Tanzania Tuko safe na ugali tulionao..

  • KUHUSU UGALI KUTOKUWA NA NUTRIENTS YOYOTE
Hili lina Ukweli kwa 0.001% na lina uongo kwa 99.99%
kwanini..?

Katika vyakula vya Asili,Ugali ni miongoni mwa vyakula vyenye Lishe bora sana na hasa chanzo kikubwa cha wanga na Nishati..
Katika kila 100 grams ya Unga wa Ugali kuna viti vifuatavyo (Kumbuka Mtu mzima anakula Walau robo ya Ugali ila hapo kwa kila Tonge au Nusu tonge)
  • Calories 370
  • Total Fat 1.8 g ambayo ni sawa na 2% ya Daily value kama utakula hivyo kila siku
  • Saturated fat 0.2 g daily value ya 1%
  • Trans fat regulation 0 g
  • Cholesterol 0 mg
  • Sodium 7 mg0%
  • Potassium 142 mg4%
  • Total Carbohydrate 79 g26%
  • Dietary fiber 3.9 g15%
  • Sugar 1.6 g
  • Protein 7 g14%
  • Vitamin C0%Calcium0%
  • Iron6%Vitamin D0%
  • Vitamin B610%
  • Cobalamin0%
  • Magnesium8%
Hapo ni kwa kiasi sijataja zote halafu unakuja unasema kuwa Haina Nultrients unajua maana ya Nutrients??

Umezungumzia kuhus Mataifa mengine afrika kwmaba hawali Ugali

Hapa ndo nilipogundua kumbe kuna uwezekano hujatembea hata Afrika yote hata kenya Tu hujafika! Uganda pia Hujafika?

Sasa nisikilize!
Hakuna nchi Afrika ambayo haili ugali..

Uganda na Kenya na Tanzania wote wanakula Ugali..
  • Ukienda kenya watauita Sima/Nsima
  • Ukienda uganda wataita Posho
  • Tanzania wataita Ugali/Nguna/Dona/Bondo
  • Central Africa na zambia,Malawi pamoja na Kongo huko wanaita Nshima
  • Zimbabwe wanaita Sadza
  • South Africa na sehemu na Botswana wanaita Pap kwa ule mlaini ila ule wenyewe wa Kisukuma mgumu wanaita Bogobe au
    Stywe
  • Sierra Leone, Guinea, Liberia, Cote D'Ivoire, Burkina Faso, Benin, Togo,Nigeria, Cameroon, Angola na Gabon huko wao wanaita Fufu
  • Ghana wanaita Banku au Akple
Kama kuna Nchi au sehemu sijataja nikumbushe nitakuambia wanaitaje..

Mwishoni Umeweka sawa kuwa hupendi ugali bhasi kitu ambacho hukipendi usikipakazie Mambo mabaya ili na wngine wakichukie..
Hata mimi sipendi ugali ila siwezi kuufanya wengine wasile
 
Ww hujasafiri africa yote wanakula ugali huko nigeria chakula kikuu ni ugali hakuna mtu mweusi ambae hali ugali huko kwenu kagera ndio mkoa maskini zaidi tz sasa kama hamli ugali huoni umaskini wenu unatokana na kutokula ugali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…