Ulaya yazuia matumizi ya chanjo ya Astra Zeneca, Rais Magufuli alikuwa sahihi kutokimbilia chanjo

Ulaya yazuia matumizi ya chanjo ya Astra Zeneca, Rais Magufuli alikuwa sahihi kutokimbilia chanjo

Wee
BBC Dira ya Dunia inaripoti kuwa zaidi ya nchi 10 zimezuia matumizi ya chanjo ya Corona iitwayo Astra Zeneca inayosababisha damu kuganda kwa baadhi ya watu.

Nchi hizo zimesema inabidi zifanye uchunguzi na utafiti wa kutosha kuhusu usalama wa chanjo hiyo kabla hazijaruhusu tena.

Rais Magufuli wa Tanzania aliwaambia wataalamu wake wasikimbilie chanjo za magharibi kabla ya kufanya utafiti wa kutosha kujiridhisha juu ya usalama wa chanjo hiyo.

Maendeleo hayana vyama!
Wee Mama acha kujidhalilisha kwa kumuongelea huyo kichaa..huoni aibu??
Kazuia chanjo halafu covid imemtandika vilevile.
 
We endelea tu kujitoa ufahamu ili kumtetea Jiwe lakini kaa ukifahamu hata huko Ulaya wanaositisha hizi chanjo ni wanasiasa kama Jiwe huku watalaamu wao wakipingana na madai ya hao wanasiasa wanaotaka chanjo isitishwe!! Sasa kama una ufahamu nani dhani pia utakuwa na ufahamu ni nani anayetakiwa kusikilizwa kati ya wanasiasa na watalaamu wa afya huku ukikumbushwa ni wanasiasa hao hao hata huko Ulaya ndio walichangia sana tatizo kuwa kubwa maradufu huko kwao!!!
Hamia huko mkuu
 
Waliochoma mpaka sasa kwa hiyo chanjo ya Astra Zenecca ni zaidi ya milioni 35 waliopata shida ni 35 tu, sasa akili kichwani mwako mjomba na pia jiulize huyo Bwana Mkubwa yupo wapi sasa hivi
Muangalie kwenye chupi yako utamuona
 
Kwa hiyo Magufuli akiwa sahihi basi imetosha? Alichoshauri ni uchunguzi wa chanjo hizo ufanyike. Hivyo basi nafikiri ni muhimu tuarifiwe juhudi zinazoendelea kuchambua chanjo mbali mbali zinazoidhinishwa kuingia sokoni duniani ili tuone zipi zinazotufaa?

Hivyo ndivyo kufanyia kazi mawazo ya Rais. Sio kumsifu tu na kuchekelea kishabiki. Ingependeza zaidi Wizara ya Afya kuanzisha vipindi kuelimisha umma kuhusu chanjo za covid-19, miundo, zinavyofanya kazi, ubora na athari zake.

Tuwe hata na mijadala ya wataalamu wetu wa chanjo yenye tija kwa Watanzania na kuondoa kabisa ushabiki wa kisiasa unaozidi kudumaza jamii kifikra. Tumeachia vilaza matapeli kuja kuhubiri ujinga wa 666, 5G, na NWO kila mahali.
Hatuitaji ripoti ya mara kwa mara kuhusu chanjo.. Serikali ifanye uchunguzi ijilidhishe ndo ilete chanjo ambayo wataona inafaa kwetu sio kutoa update eti leo tumefikia hapa na hapa hiyo ata wewe usingeweza.
 
Usipende kutanguliza matusi. Kwani chanjo iko ya aina moja tu? Chanjo nyingine zinaendelea kutumika wakati unafanywa kuhusu chanjo ya Astra Zeneca.

Amandla...
Atakama nyingine zipo lakini unajiua chanjo iliyopo kwenye mpango wa COVAX? Ni hiyo ya Astrazeneca ambayo nchi za Africa imepatiwa kwa wingi wa kudai kuwa ni bure sijui iko katika program ya kusaidia hivo wanajua kama kununua direct kwetu Africa ni ngumu
 
Ile research imeanza kutoa majibu. Taratibu tu tutakuja kujua chanjo ipi ni salama kwa watu wengi.
 
Waliochoma mpaka sasa kwa hiyo chanjo ya Astra Zenecca ni zaidi ya milioni 35 waliopata shida ni 35 tu, sasa akili kichwani mwako mjomba na pia jiulize huyo Bwana Mkubwa yupo wapi sasa hivi
Acha upoyoyo wewe,hizo takwimu wewe umezipata wapi?,lete chanzo cha hizo takwimu,
 
Dunia inahangaika kutafiti na kutengeneza chanjo ya covid-19 KISAYANSI. Mafanikio mpaka sasa ni makubwa. Zimeonyesha kiwango cha EFFICACY cha kuridhisha sana kuzuia maambukizi (66%->90%).

Sisi tumeamua kuwa miongoni mwa skeptics wakubwa wa juhudi hizi badala ya kushiriki kuonyesha kuwa na sisi tumo KISAYANSI. Tumebakia na blabla za kisiasa na conspiracies. Eti tunasubiri wakishafikia hatua ya chanjo “kuaminika” ndio “tutazikubali”. Kazi yetu ni “kuangalia na kusubiri”!

Kwa mtu aliyesoma hadi sekondari atakuwa na uelewa kwamba hakuna chanjo wala dawa duniani yenye EFFICACY ya 100% kwa watu wote katika mazingira yote. Kinachotafutwa ni kiwango kinachokubalika kutatua tatizo na cha side effects zake. Hesabu za statistics zinatumika kupima hivi vigezo. Hii ni kwa teknolojia zote. Kwa mfano parts za ndege hubadilishwa kwa makadirio ya efficacy na reliability ya aina ya parts hizo kulingana na mwenendo wa ndege, masaa ya miruko na hali za hewa.

Sasa kama sisi kazi yetu ni kukaa tu na siasa zetu uchwara kusubiri dunia “ikamilishe kazi” na kuja kututhibitishia kwamba sasa chanjo ni 100% na side effects ni 0%, tusishangae kwa nini tunaendelea kuwa watumwa wa “mabeberu”!

Inasikitisha kuona kama vile tumeamua kwamba hatutaki wataalamu wetu wafanye kazi zao badala yake muda mwingi wanatumika kuunga mkono matamko ya ajabu ajabu ya wanasiasa kwa hoja zisizo na mashiko.
 
IMG_0509.jpg
 
Mbona hata hueleweki? Kwa ufupi kabisa nataka nikueleze kuwa sisi TZ tumekataa kufanyiwa majaribio hizo chanjo bado hazijafikia kiwango cha kuwa chanjo kamili ndiyo maana watoa chanjo hizo wameshasema they cannot held responsible for any problem occurs while the so called chanjo used by human being until the research completed. Wataalam walikuwa bado wanaendelea na research yao lakini wazungu wanasiasa wakasema zianze kutumika. Be informed please!!
 
Alikuwa sahihi kusikilizia kwanza madhara ya chanjo, alichokosea ni kukebehi na kuponda hadharini wakati hakuna nchi iliyolazimishwa kuchuka chanjo. Haikutakiwa kuwaponda na kuwakebehi wakati chanjo zote za watoto zinatoka kwao. Ilitakiwa tuseme kwamba bado tunajiridhisha kwanza.
 
BBC Dira ya Dunia inaripoti kuwa zaidi ya nchi 10 zimezuia matumizi ya chanjo ya Corona iitwayo Astra Zeneca inayosababisha damu kuganda kwa baadhi ya watu.

Nchi hizo zimesema inabidi zifanye uchunguzi na utafiti wa kutosha kuhusu usalama wa chanjo hiyo kabla hazijaruhusu tena.

Rais Magufuli wa Tanzania aliwaambia wataalamu wake wasikimbilie chanjo za magharibi kabla ya kufanya utafiti wa kutosha kujiridhisha juu ya usalama wa chanjo hiyo.

Maendeleo hayana vyama
Mtoa mada unafahamu kuna chanjo ngapi za COVID ukiacha hiyo Astra Zeneca? siyo kila chanjo ya COVID ni Astra Zeneca. Tofautisha sayansi na siasa.
 
Hawawezi kusema jambo ambalo halijatokea na ndo maana wao wanaripoti kile kinachotokea! Aidha, hao unaosema "wenyewe" ni Wanasiasa lakini sio watalaamu! Na kama nilivyosema hapo awali, achilia mbali na JPM wa Tanzania, hata huko Ulaya na Marekani ni wanasiasa hao hao ndio walichangia tatizo kuwa kubwa zaidi kwenye nchi zao baada ya kupinga miongozo ya watalaamu! Sweden kwa mfano, serikali ikapingana na miongozo ya watalaamu na matokeo yake nchi ikaathirika vibaya sana hadi ikafungiwa mipaka na majirani zake nchi za Scandinavia! Kama sio mfuatiliaji wa siasa za kimataifa bali angalau utakuwa unafuatilia siasa za Marekani! Watu tulikuwa tunamsikia Trump alivyokuwa anafanya mzaha huku akipingana na watalaamu! Kule Iran kiongozi wao akatangaza Iran italindwa na Allah!!

Mataifa yote hayo, hadi wanakuja kushtuka na kufuata maagizo ya watalaamu ikawa too late kwa sababu tayari corona ilishaingia mtaani na ikawa ngumu kudhibiti hadi kesho!!! Hao ndio unaowaita "wenyewe"! Yaani viongozi wa kisiasa wanaoenda kinyume na maagizo ya kitaalamu! Hapo wakiendelea kufyekwa zaidi, kama ambavyo utafiti uliotoka huko Sweden kwamba hii variant ya sasa inaathiri hadi watoto; hapo ndipo wataanza tena kutafutana na kutafuta chanjo wakati ishakuwa too late kama wakati huu ugonjwa ulipoingia!!
Hapa tunazungumzia ubora wa chanjo iliyotolewa na sio namna maamuzi ya kudeal na ugonjwa yalivyotolewa.
 
Atakama nyingine zipo lakini unajiua chanjo iliyopo kwenye mpango wa COVAX? Ni hiyo ya Astrazeneca ambayo nchi za Africa imepatiwa kwa wingi wa kudai kuwa ni bure sijui iko katika program ya kusaidia hivo wanajua kama kununua direct kwetu Africa ni ngumu
Watu zaidi ya milioni 17 wamechanjwa na Astra Zeneca ulaya peke yake. Katika hao ni 37 ambao wamepata matatizo, proportion ambayo ni sawa na wao matatizo hayo bila hata vaccine. Mpaka sasa hamna uthibisho kuwa hayo matatizo yametokana na chanjo hio.Kwa odds hizo mimi nitakubali kuchanjwa tu.

Aidha, hii chanjo inapendekezwa kwa Afrika kwa sababu utunzaji wake ni rahisi kuliko chanjo ya Pfizer ambayo inahifadhiwa kwenye baridi ya -70. Sehemu nyingi kwetu hazina uwezo wa kuzihifadhi kwa baridi ya kiasi hicho.

Amandla....
 
BBC Dira ya Dunia inaripoti kuwa zaidi ya nchi 10 zimezuia matumizi ya chanjo ya Corona iitwayo Astra Zeneca inayosababisha damu kuganda kwa baadhi ya watu.

Nchi hizo zimesema inabidi zifanye uchunguzi na utafiti wa kutosha kuhusu usalama wa chanjo hiyo kabla hazijaruhusu tena.

Rais Magufuli wa Tanzania aliwaambia wataalamu wake wasikimbilie chanjo za magharibi kabla ya kufanya utafiti wa kutosha kujiridhisha juu ya usalama wa chanjo hiyo.

Maendeleo hayana vyama!
Kwa mazingira na tamaduni zetu ambapo mikusanyiko haikwepeke, chanjo ndio muokozi wetu pekee. Kama hatuwezi kuzuia watu kujazana kwenye mabasi, sokoni, misiba, kanisani, msikitini n.k. basi heri watu wachanjwe ili waweze kuendelea na shughuli na tamaduni zao.

Kwani waliochanja wanaruhusiwa kukusanyika?
 
Mtoa mada unafahamu kuna chanjo ngapi za COVID ukiacha hiyo Astra Zeneca? siyo kila chanjo ya COVID ni Astra Zeneca. Tofautisha sayansi na siasa.
Na wewe tofautisha siasa na sayansi!
 
Back
Top Bottom