Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Wewe jamaa ni mjinga.Umeanza lini kumkejeli mh.raisi acheni dharau zakishamba uku kwenye mitandao.Mama ataona mwenyewe kipi kinamfaa kulingana na kilichompeleka uko sasa wewe ni nani hadi ujifanye mshauri wa raisi tena kwa kukejeli.acha ulimbukeni.
Haya, BRN nyingine hii hapa.

Ushuhuda ulio wazi.
 
Sasa "MASWALA" ndio nini,unashauri matumizi ya kiswahili kumbe kiswahili chenyewe haukijui,tabu sana[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ni kweli lazima tulinde legacy ya Mwendazake katika kuongea KISWAHILI.
 
Usikariri kama kasuku wa kufugwa.

Hata Kiswahili ni "international language" pia.

Vinginevyo labda hujui maana ya neno "international".
Unachekesha wewe! Jinsi unavyo waza na kuandika najiwa na fikra jee mwendazake hakwenda ila alijibadili na kuitwa Ambokile Amanzi nini?
Maana akili zenu zinafanana! [emoji3][emoji3]
 
Kwakuwa mwendazake alikuwa hajui king'eng'e, mnataka kila mtu awe kama yeye, Mama ana uhuru wa kutumia lugha yoyote,na lengo haeleweke kimataifa
 
Pointi yako ni ya maana Sana ...lakini subiri matusi na kejeli humu
 
Kumbuka mama anaenda kuhutubia bunge la Kenya ili ujumbe wake uwafikie walengwa nisawa kutumia lugha inayokubalika na wengi huko ambayo ni kiingereza, target audience yake kwa wakati akiwa huko si wewe au Mwanjuma alie Naliendele Lindi. Hivi ina make sense mathalani unataka kudeliver message yako kwa mrusi na unafahamu kirusi halafu unaongea Kiswahili kwasababu unajivunia lugha yako ya asili? Tuache siasa
 
Uganda akiongea Kiingereza, sawa tu manake wale jamaa wana bifu na Kiswahili!!

Kenya, kwa kuwakomoa tu, anapaswa atumie Kiswahili manake Kiswahili wanakijua vizuri lakini kutokana na ulimbukeni wao wa kumsujudia Mzungu, wanajifanya hawakijui!!
Wabongo bhana vitu vingi tunatumia vya mzungu ila kwenye lugha ya kimataifa ya biashara mnaona ni kusujudia...jamiiforum hii ipo hapa kwa ajili ya tekinolojia za mzungu ndio mimi na wewe tunasawaliana tumeacha hadi kupanda punda...
 
Maza piga ung'eng'e
Naunga mkono hoja.
Mleta mada ukitaka kujua umuhimu wa lugha ya kiingereza, fanya utafiti kidogo uone ni kiasi gani cha fedha
Waingereza wanachopata kwa kuuza lugha yao kote duniani kutokana na mitihani ya IELTS na TOFEL.
 
Aongee lugha yeyote nachohitaji ni ushirikiano mwema kwenye biashara maisha yaende mambo ya Nchi jirani kufungiana mipaka ni upori pori fulani maana chakula cha Tanzania kinaliwa hadi Sudan na huko Kenya kaskazini kuna ukame wanahitaji chakula waje tuwauzie hayo mambo ya Lugha mtajua wenyewe ..
 
Kumbuka katika ziara ya uganda palikuwep na washitiri wengine ambao hawajui kiswahili,hivo ilikuwa lazima aongee kiingereza
 
kingereza ni lugha ya Dunia, ni lugha ya biashara ya za kimataifa. huwezi kufanya biashara na dunia kama hujui lugha zinazotumika na wateja duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…