Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapi nimesema kusujudia?!Wabongo bhana vitu vingi tunatumia vya mzungu ila kwenye lugha ya kimataifa ya biashara mnaona ni kusujudia...jamiiforum hii ipo hapa kwa ajili ya tekinolojia za mzungu ndio mimi na wewe tunasawaliana tumeacha hadi kupanda punda...
Ulishakaririshwa kwenye shule ya kata uliyosomea kwamba, ili biashara iwe ya "kimataifa" lazima ihusishe ulaya ambapo kuna Kiingereza.kingereza ni lugha ya biashara za kimataifa
Kiswahili kinakufanya vipi ushindwe kusogea?!Vyote kwa pamoja.
Kwani Kivukoni hakufundishwi kiengereza??Uganda akiongea Kiingereza, sawa tu manake wale jamaa wana bifu na Kiswahili!!
Kenya, kwa kuwakomoa tu, anapaswa atumie Kiswahili manake Kiswahili wanakijua vizuri lakini kutokana na ulimbukeni wao wa kumsujudia Mzungu, wanajifanya hawakijui!!
Dooh!Usituletee mawazo ya Nyerere ambayo kwa sasa hayana tija.
Wanajavi wenzangu kama Mama Atasoma speech zake zote kwa Kiingreza ni sawa tuu, Ila Mama anaongea Kiingereza cha kueleweka. Kuongea kwa ufasaha wa kujivunia lugha ya Kiingereza bado kidogo aongeze jitihada.Tumesikia Bi. Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.
Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya.
Hivi majuzi tu alipoenda Uganda, tuliona anatumia kizungu kuhutubia.
Wengi wa wananchi wetu nina uhakika hawakuelewa hata anachozungumza.
Ifahamike kwamba, Kiswahili si lugha ngeni Afrika Mashariki. Tuachane na Viingereza pasipo na ulazima.
Sijui ni nani aliyewalaghai kwamba kuongea kizungu ni ufahari na usomi?
Hata katika mazingira yasiyohitaji kizungu, bado watu watajing'ang'aniza kuongea kizungu hata kama hawakiwezi na tunajua kwa hakika kwamba hawakiwezi.
Hebu tuachane na hizi "You Know You know ofcozi zea zea" mingi mingi. Tunajiaibisha na kujidunisha.
Tunayo lugha adhimu ya Kiswahili. Tuitumie hiyo.
Nasubiri kuona hiyo Kesho vile Bibi SASHA atakavyojitutumua na viingereza vyake uchwara.
Ashauriwe vyema. Maana shughuli za aina ile sio mahali pa kuonesha mbwembwe za kuzungumza kwa lafudhi bandia za kimalkia.
Tunahitaji kusikia "maswala" yakijadiliwa na kuzungumzwa. Hatuhitaji mikogo ya lafudhi bandia za Kizungu.
Hilo nalo ni tatizo!!!Kosa letu ni kuwaanzisha watoto wetu elimu ya msingi kwa lugha ya Kiswahili . Halafu tunabadika secondary watoto wakishakuwa na aibu ya kuongea broken English. Ni mpango wa ajabu sana
Wewe ndie mwenye kiingereza uchwara! Mama anatiririka sio wewe!Tumesikia Bi. Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.
Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya.
Hivi majuzi tu alipoenda Uganda, tuliona anatumia kizungu kuhutubia.
Wengi wa wananchi wetu nina uhakika hawakuelewa hata anachozungumza.
Ifahamike kwamba, Kiswahili si lugha ngeni Afrika Mashariki. Tuachane na Viingereza pasipo na ulazima.
Sijui ni nani aliyewalaghai kwamba kuongea kizungu ni ufahari na usomi?
Hata katika mazingira yasiyohitaji kizungu, bado watu watajing'ang'aniza kuongea kizungu hata kama hawakiwezi na tunajua kwa hakika kwamba hawakiwezi.
Hebu tuachane na hizi "You Know You know ofcozi zea zea" mingi mingi. Tunajiaibisha na kujidunisha.
Tunayo lugha adhimu ya Kiswahili. Tuitumie hiyo.
Nasubiri kuona hiyo Kesho vile Bibi SASHA atakavyojitutumua na viingereza vyake uchwara.
Ashauriwe vyema. Maana shughuli za aina ile sio mahali pa kuonesha mbwembwe za kuzungumza kwa lafudhi bandia za kimalkia.
Tunahitaji kusikia "maswala" yakijadiliwa na kuzungumzwa. Hatuhitaji mikogo ya lafudhi bandia za Kizungu.
Kama Kivukoni ya akina Polepole, sina shaka wanakifundisha... huoni JPM alivyokuwa anabonga ung'eng'e huku akiwashangaa wale wanaosema hajui Kiingereza wakati amesoma "Uraya"!Kwani Kivukoni hakufundishwi kiengereza??
Kuna ulazima gani kuhutubia kwa Kiingereza cha kusoma kwenye Karatasi wakati hadhira yote (ya Kenya na Tanzania) inakijua Kiswahili?Wanajavi wenzangu kama Mama Atasoma speech zake zote kwa Kiingreza ni sawa tuu, Ila Mama anaongea Kiingereza cha kueleweka. Kuongea kwa ufasaha wa kujivunia lugha ya Kiingereza bado kidogo aongeze jitihada.
Mwisho ya wapi?
Mbona unalazimisha watu, hata rais kufuata mawazo yako ya ajabu kabisa!!!Kwa sasa Kiswahili kimepanuka karibu nusu nzima ya Afrika.
Somalia, Kenya, Sudan, DRC, Uganda, msumbiji, Uganda, Rwanda, Botswana, Malawi, Burundi, China, South Afrika...
Huko kote Kiswahili kinaenea kwa kasi.
Weka uthibitisho."Maswala" ni masuala
Ufasaha wa Kiingereza kama lugha hata mama bado kuna taabu.huyu yupo flexible,jiwe hakujua kingereza
Wewe huna japo uwezo mduchu wa kuelewa mtiririko wa majadiliano.Mbona unalazimisha watu, hata rais kufuata mawazo yako ya ajabu kabisa!!!
Kwani mh. Rais akiongea Kiingereza huko Kenya kutazuia Kiswahili kuendelea "kuenea kwa kasi", if at all it's true?
Duh!Wewe huna japo uwezo mduchu wa kuelewa mtiririko wa majadiliano.
Umezoea ile midahalo ya sekondari ya maji ni bora kuliko chumvi.
Kama huwezi angalau kusoma na kuelewa, basi kaa kimya — usinipotezee WAKTI.
Hata kutamka "invitation" hawezi!Ufasaha wa Kiingereza kama lugha hata mama bado kuna taabu.
Ukitaka kumfurahisha mgeni au mwenyeji wako zungumza lugha yake.Tumesikia Bi. Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.
Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya...
On point.Kuna ulazima gani kuhutubia kwa Kiingereza cha kusoma kwenye Karatasi wakati hadhira yote (ya Kenya na Tanzania) inakijua Kiswahili?
Na itakuwa ni ajabu sana, mwenyeji wake wa Kenya azungumze Kiswahili, halafu yeye mtanzania aanze kutusomea hotuba za Kizungu-butu!..