Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Pointi yako ni ya maana Sana ...lakini subiri matusi na kejeli humu
Wajuaji huwa hawakosekani humu!

Lakini bahati nzuri ni kwamba, wengi wao ni wajuaji wasiojua kitu.

Ninawamudu sana hawa.
 
Kumbuka mama anaenda kuhutubia bunge la Kenya ili ujumbe wake uwafikie walengwa nisawa kutumia lugha inayokubalika na wengi huko ambayo ni kiingereza, target audience yake kwa wakati akiwa huko si wewe au Mwanjuma alie Naliendele Lindi. Hivi ina make sense mathalani unataka kudeliver message yako kwa mrusi na unafahamu kirusi halafu unaongea Kiswahili kwasababu unajivunia lugha yako ya asili? Tuache siasa

Wewe bwana acha blah blah ....

Hadhira lengwa hapa ni wakenya na watanzania.

Na lugha pekee ambayo ni lugha-unganishi ni KISWAHILI.
 
Hata Kiswahili ni lugha ya kimataifa na ya kibiashara pia.

Kenya, Uganda, Rwanda, Congo... huko kote tunawasiliana nao na kufanya nao biashara kwa lugha ya Kiswahili...
Dunia ni nchi hizo ulizozitaja? Mwendazake kakuharibu
 
Lugha yenyewe watz wengi siku hizi ni shida, hata afadhali kule Mombasa Kenya wanatushinda,,tumebaki na kiswahili cha mitaani kisicho rasmi...Mama wewe soma hotuba ya kiingereza tu ujiondokee...
Imemaliza mjadala, Safi conclusion
 
Ukitaka kuendelea kuonekana kituko kwenye nchi za Commonwealth endelea kuongea Kiswahili.

Hivi mnataka kuendelea na UMBUMBUMBU wa Mwendazake ambaye anadai ana PhD ya Chemistry lakini hawezi kutengeneza sentensi ya English yenye correct grammar??

Hapana, Hapana, Hapana. Tutaongea Kiswahili kwenye masuala yetu lakini kwenye jumuiya za kimataifa kuna lugha 7 kubwa; Chinese, English, French, Portuguese, Spanish na Russian
Imemaliza kazi
 
Dhima ni kurudisha mahusiano ya kimataifa kwa speed nzuri kabisa, na kama lugha unaimudu tiririka tuu🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom