Ulevi na Kulewa Wikiendi: Kufurahia Maisha au Kutoroka Realities?

Last_Joker

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2018
Posts
272
Reaction score
414
Ijumaa ikifika tu, watu wanasema "leo tuna-drop stress zote, tunaweka shida chini na kutupa mikono juu" halafu Jumamosi inafuata na vileo juu ya vileo, kubanjuka, vijiwe nongwa. Lakini je, huu ni utamu wa maisha ama ni njia ya kutoroka yale tunayoshindwa kuyakabili kwa macho ya nyama na damu?

Maisha Magumu, Weekend Iwe Tamu​

Let’s be real – maisha yanakandamiza! Kodi, madeni, pressure za kazini/vibaruani, kutopata ajira, mapenzi yanayovunjika ovyo… so ikifika wikiendi watu hawataki kusikia kitu chochote cha “serious.”
Ni muda wa kubadilika – kutoka kwa mtaabikaji wa wiki hadi "Mr. Enjoyment" wa usiku wa manane. Wengine wanatumia hiyo kama healing, wengine kama kiki, wengine kama kimbilio.

Lakini Vipi Wale Waliozidi Dozi?​

Unakuta mtu kila weekend lazima alewe, lazima apotee hadi aokotwe. Ni kama kulewa ndio stress-reliever ya pekee aliyobakiza. Ukimuuliza anasema, “Bro unajua stress zangu?”
Lakini je, hii ni furaha au ni temporary escape tu?
Je, tunaburudika au tunaji-stress bila kujua?

Kunywa Kistaarabu au Kuwa Mlevi Mbwa?​

Kulewa kila week ni kama kuwa na mpango wa kudumu na pombe. Haina tofauti na kuwa addicted.
Kama ni furaha ya kweli, kwanini ifuatiwe na hangover kali, kupoteza vitu, au kujikuta ummetext ex wako?
Na cha kushangaza zaidi – wengi wanapenda ile attention wanayoipata wakiwa wamelewa… “ulevi unatoa confidence” – kumbe confidence ya bandia.

Tujiulize...​

Ukiambiwa usilewe kwa mwezi mmoja tu – je, unaweza?
Ukiambiwa weekend hii usiende club – je, inakuuma au ni sawa tu?
Ukiwa sober, unahisi maisha yako yako boring sana hadi uhitaji kileo ili yawe interesting?

Kama majibu yanauma, basi jibu tayari lipo – huwezi kusema unafurahia kama kila raha yako inahitaji gambe.

Mwisho wa Siku…​

Kunywa au kulewa si kosa, lakini je, unafanya kwa sababu unajifurahisha au unajaribu kusahau maisha yako halisi?
Tufurahie, lakini tujitunze. Raha ni nzuri ikiwa haileti madhara kesho yake.

Drop Maoni Yako​

Wewe huonaje? Kunywa kila weekend ni lifestyle ya starehe au ni njia ya kutoroka matatizo?
Tuongee ukweli bila kupendeleana.
 
Mkuu unao ugonvi na sisi wapiga tungi kwani?😂😂😂

Life is a daily struggling to survive na naturally mwili na nafsi zinahitaji kumpumzika baada ya kazi........ Ndio maana tuna masaa ya kazi, weekend off na hata likizo

Starehe maana yake sio KUONDOA shida wala sio KUHAIRISHA shida
Starehe maana yake ni kuupumzisha mwili kwa kuburudisha mwili na nafsi baada ya struggling

Na Starehe sio POMBE tu kama unavyodhania, kuna michezo, kutoka out na michepuko/familia, kwenda kula mdudu, kucheza pooltable or whatever your find it pleasurable

Sio sahihi kudhania kwamba starehe ya pombe inatakiwa aifanye mtu ambaye HANA CHANGAMOTO....... Hakuna asiye na changamoto
 
Wanywa vyoda wana hasira soda 500 chupa moja bia moja 5000 mpaka 10000 na mtu anakunywa 8 lazima povu litoke😅
jamaa wana-complicate maisha sana.

muda mwingi wanatumia kubishana mpira-wakimaliza mpira ndio wanaanza kutunanga...baada ya hapo wanatupiga mabomu ya pesa
 
Mkuu unao ugonvi na sisi wapiga tungi kwani?😂😂😂

Life is a daily struggling to survive na naturally mwili na nafsi zinahitaji kumpumzika baada ya kazi........ Ndio maana tuna masaa ya kazi, weekend off na hata likizo

Starehe maana yake sio KUONDOA shida wala sio KUHAIRISHA shida
Starehe maana yake ni kuupumzisha mwili kwa kuburudisha mwili na nafsi baada ya struggling

Na Starehe sio POMBE tu kama unavyodhania, kuna michezo, kutoka out na michepuko/familia, kwenda kula mdudu, kucheza pooltable or whatever your find it pleasurable

Sio sahihi kudhania kwamba starehe ya pombe inatakiwa aifanye mtu ambaye HANA CHANGAMOTO....... Hakuna asiye na changamoto
Kwa hiyo tule tu gambe mangi?
 
Yani mnaokunywa soda bana mna wivu sana,mtu akitoroka iyo reality akasahau shida zake wewe inakuuma nini??
Endelea kukumbuka izo shida zako acha watu wafurahi!
Nyie kila siku kufungua uzi tu afu mna maisha magumu sana,afu wambea kinoma
 
Back
Top Bottom