Getto kuishi nilianza nikiwa na miaka 19..Nimesoma bweni kuanzia form one mpka six,nkajiapiza chuo sikai hostel hata kwa dawa,na kwakua nilikua na lengo la kusaka life dar,nilichagua vyuo vya dar tu na nikabahatika kupata kimoja wapo,kuna ndugu yangu alikua na nyumba dar na akahamishiwa mkoani,so akapangisha nyumba nzima na kikabaki chumba kimoja kibovu sana hakina hata sakafu ya cement,nikanunua godoro,kitanda na kapeti maza aliniagizia toka home life likaanza,kutokana na nilivyolelewa home ile familia iliyopanga ile nyumba yote pale walinipenda sana nikawa kama mwanafamilia hivi wakanipa Tv niweke geto kwangu,misosi napewa yani hakuna tofauti na home,ikafika kipindi had nkichelewa kurud naulizwa,siku niliingiza demu kiwizi kinoma na asubuhi kumtoa wakanisaidia masista watoto wa yule mama,nikaona hapa siwezi endelea nikahamia mabibo pale chumba 50k,na huku natafta mishe mana chuo nilikua nasoma jioni,mpaka na maliza chuo nilikua na nshapata mishe ya videography na picha so haikua ngumu sana,mpaka sasa niko fresh namhudumia maza mkoa,namsomesha mdogoangu na naishi life ninalotaka dar kama kijana,nilihamia geto self contained baada ya kuona kipato kinaruhusu sasa nataka nichukue nyumba nzima,kipindi kigumu nimepitia sana ila sijawah kosa kula kwakua kila ninapokaa naishi vzur sana na wapangaji wenzangu na mimi napenda sana watoto hivyo kama unavyojua mwanamke yeyote ukimpenda mtoto wake anakuona wa maana sana hivyo misosi hii nakula sana,siku nisipopika wanajua tu utashangaa unaletewa tu msosi,ndomana naitwa ANKO sababu ya watoto.
Usiogope kuanza kujitegemea mana ukishindia mkate siku 3 akili inafunguka yenyewe.
Am only 23.
Sent using
Jamii Forums mobile app