Ulianzaje kukaa gheto?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipanga geto nikiwa na miaka 19,nafanya kazi kwenye kihoteli kwa mtu baada ya muda nkauza kila kitu nkaenda dar nkapanga geto kigamboni kwa mparasinge baada ya muda

Nikauza kila kitu nkaenda kukaa kwa Braza nkaja kupanga chumba upya juzi tu nikiwa na ajira rasmi namshukuru Mungu serikali iliniajiri nikiwa na umri mdogo sana 21yrs hvyo nilianza kujitegemea mapema nlivyopewa hela ya kuanzia maisha nkanunua kitanda kikubwa, subwoofer, fridge, jiko la gas sahani mbili, vyombo vya ndani.

Mungu nsaidie mwaka huu nianze ujenzi wa nyumba yangu pale mlandizi
 
Dah mim nlpata kazi wilaya furanii.ikabidi nlilipoti ujio wangu siku tatu mbele bwana bwana!! Nfukoni nlikua na elf90 niliyopata kwnye ufundi redio wangu nkatumia elf tano kama nauli then kama elf kum hiv kununua vijimahtaj kidogo

basi nkalipoti hilo eneo lakaz kwakufkia nyumba ya wageni,uzuri wa hapa bwana vyumba sio tabu, dah kesho yake nkapambana kutaftata had nikakipata, bas nkanunua zangu mkeka.

mwanaume nkahamia magetoni....
Nakumbuka ule usiku ulikua mrefu kwangu .kunawadudu wanaitwa sungu sungu walipigiana simu aise nadhani waliambiana ...oy mazee uko nje mje kunapilau hapa ndaniiii muwai.

Ila MUNGU MKUBWA leo nnamiezi kama mi 4'ukizama geto unaeza usitoke mziki kama woootee

Voxser empire
 
Hii siredi inanipa hamasa kubwa mno, mimi kwasasa sipo kwa wazazi maana wazazi wako pande za Bujumbura na mimi niko pande za papa misifa(Kinshasa DRCongo) na nna mwaka mmoja tangu nidondoke pande hizi nina job japo hailipi sana ki vile ila bado nnaisha na brother.

Nnapanga kumtoka bro na haifiki october maana kama brother hanipi freedom lote tayari maandalizi ya vitu vya ndani nimesha yaanza nina godoro langu, feni na vingine vidogo vyakuanza ghetto life ila kila nikisoma comments nnatamani ata nipasuwe kesho yani

#Proud_to_be_a_domo_ZEGE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaitwa get it how you live.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah bigup mkuu...kwaiyo sungu sungu basi saiz
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii thread ina mizuka sana...uyo bro muhesabie siku tu..atafrahi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Big up kwa huyo mwamba wako, mwanaume harudishi nyuma majeshi kizembe
 
Mkuu hapa ni gheton kwangu yaani kukuazima siku moja umeshakuja kuosha Jf. ! Natania mzee

Mimi nilianza kujinunulia vitu vya ndani nikiwa form 3 nilijibana sana nakumbuka nilikua nina sutuali mbili na flana 3 na shati 1 pesa yote niliyokuwa napewa na brother zangu na mshua niliibana ninunue vitu vya ndani,,,

Nilipoanza chuo ndo nikaenda kupanga huku nikiwa full kwa 90% mpaka leo,,sikuwa na kazi lakini nilijiban na kupiga ishu ndogo ndogo kwahiyo vijana wenzangu msiogope kutoka home ikiwa una uwezo wa kupata hata buku 5 kwa siku.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikubali mkuu huko ni kujishushia heshima unapokaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah mkuu we ukiona geto kali tu unasema lako [emoji3]

Sema ww ulianza ona mbali,kama tangu form 3 ulishaanza mipango

Ushaur wako mzur kaka,wana tuache uoga as long mtu unaeza pata buku 5 bas maisha ya geto tunayaweza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kuna baadhi ya vijana wenzangu wao hufurahia kuwa na gheto kwa ajili ya kufanya tu umalaya badala ya kufikiria kuwa ni hatua ya kwanza ya maisha yake aitumie nafsi aliyoipata kusogea mbele, mwisho wa siku anaishia kuzalisha wanawake hovyo anakuja kuoa mwanamke asiyekuwa na matarajio nae wanazaa watoto wakiwa chumba kimoja kipato chake hakijakuwa umaskini tayari maana inakuwa too late

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geto ukikosea mipango tu unaitwa baba bila kupenda..maisha mwisho yanakugonga[emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh mimi nijaribu kupanga gheto moja hivi maeneo flani hapa mwanza nililipa kodi ya miezi minne, lakini nikawa sina mchongo hata hela ya kula ikawa tiz,.nikawaza sana nikapata jibu kuwa hata yesu nae alirudi kwa baba yake, time hii niko na dogo tunakatiana kitumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…