Ulianzaje kukaa gheto?

Hata ikiwa hivyo kama huna maneno mengi mbona unaishi tu. Tatizo la nyumba za hivyo kunakuwa na uswahili.

Sipendi sehemu ambazo watu hufungulia subwoofers Kama wanashindana.

Hapa nilipo unaweza hisi hakuna binadamu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa ndo penyewee.
 
Sikuwahi kukaa ghetto maana niliacha udom nikaenda college afya na chakula kilikuwa hapo hapo na vyumba vilikuwa apoapo sikukaa MDA marefu nilipata kazi Duuuuh nilitafutana nilikuwa na demu lakin tuliachana ndan ya week Tu baada ya kupata kazi Kwa ajili ya ubize wa kazi, mahali nilipopata kazi mwanamke wa kuowa sioni. Saiv natafuta mfanya kazi wa ndani mdogomdogo wa kike Ila nitamwambia nimeowa mke yupo mkoa mwingine kikazi Ila atakuja MDA wowote
 
Wasiopenda pika wengi wao hawajui pika
Hapo umenena yaan najua kupika ugali tu. Hivyo vingine aiseee ni jau tupu. Home nilikua na dada 3. Nilikua nakula tu na kuchota maji, kupika sikuwahi.
Nina mwaka wa 2 cjawahi kupika chochote ghetto, hata chai tu. Ni mwendo wa kubadilisha migahawa tu.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kumla kizembe usipolua makini.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Jifunze pika, vyakula vya mahotel, migahawa mingi viko kibiashara kuliko kiafya
 
Afu kuna hii nimesahau kusimulia hapo juu.

Ilikuwa hivi mwezi Juni kuna mwana alikua na getho zuri Town centre bei kitonga akawa anahama anahamia kwake basi akasema anipasie.
Nikafuata ushauri humu ya kwamba unaweza panga afu huku uko unakaa home unajivuta na kununua au kuweka vitu mdogomdogo. Basi nikajikusanya nikapata kodi ya miezi mitatu. Nikalipa. Hapo nasubiri mishe fulani itiki then nisepe home nihamie kwa hilo getho nililolilipia..
Hee si mishe ikabuma nikazidi kujipa moyo. Mwezi wa kwanza, wa pili hadi wa tatu unakata sijawah hata peleka chochote wala nilale.
Mwezi wa tatu yaani ule mwez kodi ndio inaisha mwenye nyumba yuko Dar akanipigia akanambia Sparta mbn kumbe hujahamia miezi yote hiyo. Nikamdanganya nikamuambia ya kuwa mzee niko porini tunapasua mbao so niko camp sijapata muda wa kuja Town.
Akanambia ya kuwa kuna watu wanamsumbua wanakitaka chumba dah kama veep nikurdishie kodi ya mwezi mmoja. Nikasema sawa kishingo upande.
😂😂😭😭
Nikacheka wee na kulia kwa pamoja.
Ukiona mtu kahamia full getho mpe heshima yake kwa kweli.

Elfu sitini yangu ikaenda bure na sijawahi kumuambia mtu dadeki.



Lakini hii leo nimeweza hamia rasmi na uwezo wa kulipa bills na korokocho nyingine ninao.
Sasa inatakiwa nitafute muda niitengeneze kabati langu la nguo na style hii hapa.
 
Hama.

Kuna mtaa huwa napita kuna vyumba kama 30 kila mtu anapiga wimbo wake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], hapa kwetu hakuna huo mtindo, tupo wastaarabu na tulio elimika.
 
[emoji23] mkuu naona umeamua kuwakanya vijana katkat ya uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…