Ulianzaje kukaa gheto?

M napenda kuwa na fridge ndogo kama iyo yako siku moja ,Bei yake inaenda kias gan na uimara wake na kampuni ipi nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekupata mkuu, ila kama tukisema tuieweke kimakundi hiyo Fridge basi haitokaa kwenye kundi la Fridge ndogo labda picha tu ndo imefanya uhisi ni ndogo, ila hiyo tuiite size ya Kati ambayo inafaa ata kwa wenye Familia maana ina ujazo wa 141 Litres

Sasa tukija upande wa bei ndomana me nimemwambia ndugu yangu Depal kuwa ni Hisense mkombozi wa Wanyonge kutokana vitu vyao kuwa na ubora kiasi chake ila pia bei zake ni rafiki, hiyo me nilichukua 680k tu Mkuu
 
Hiyo friji sio ndogo
Ni medium
Akitaka ndogo yake ziko za mlango mmoja kwa 450.


Nilipo ni 650
Bei ya kujuana mwisho 630 ‘ mpaka mjuane ile ya uhakika.
 
Wadau nina 800k nataka ninunue kitanda na godoro zuri vya kudumu ila juzi kati nilienda kwa fundi wa vitanda akaniambia kitanda kizuri cha mbao za mninga minimum niwe na 800k akanionesha na picha baadhi ni vizuri kiukweli nikamwambia nitarudi ngoja nijipange, ninachotaka kujua ni kweli vitanda vya mninga vina bei kiasi hicho? au kama kuna mtu anajua sehemu naweza pata kitanda kizuri cha kudumu aniambie wakuu at least 600k naweza kununua.
 
Kwa Mninga mkuu ni kweli kabisa, tofauti na hapo labda uwe na fundi mzuri Mkoani kisha akutengenezee design unayotaka wewe akuagizie ndio utapunguza gharama na kufikia 550-600k
 
Ulikosea sana kurudi nyumbani.

Mimi bado nipo chuoni Mwaka wa mwisho ila ninaishi getto, nitanunua kila kitu kadri ya uwezo, ili nikimaliza chuo nisirudi home.
Really aiseee. Maana sometime unaeza pata nafas ya kumuonesha muelekeo mzaz au mlez kwakua umeonesha nia ya kuyaanza
 
Ushauri mzuri sana umempa,ila kama kero anazokutana nazo zinazidi hata kero za kulala chini na kula mkate na maharage. Basi namshauri ahamie kwake mapema sana.
Mkuu hiko chupa ni inches ngapi?
 
Uko mkoa gani Mkuu? Huku niliko mninga ni 950k-800k (6*6), 5*6 ni 750k-600k.
 
Kabisa nataka nitoke full package mkuu hm na job ni karibu.
 
Mti wa mninga unapatkana mkoa gan?? Na ntajuaje kwamba hk ktanda kweli kimetengenezwa kwa mninga?
Ni ngumu kujua mkuu kama huna uzoefu na mbao, ila mara nyingi waga ni busara za fundi tu kama unajuana nae hawezi kukupiga

ila kwa baadhi ya sifa za Mninga ni mbao nzito sana tofauti na mbao zingine lakini pia unakuwa hauna Rangi moja, unakuwa na mabaka mabaka

Pia ukipigwa tu msasa na kupigwa vanish unawaka hatari unaweza kusema umepigwa mapambo ya Kipemba kumbe vanish tu

Kwa upande wangu Mara nyingi Mninga nilifanikiwa kuona Tabora na Iringa ila Dar sinaga kabisa imani nao
 
Ushauri mzuri sana umempa,ila kama kero anazokutana nazo zinazidi hata kero za kulala chini na kula mkate na maharage. Basi namshauri ahamie kwake mapema sana.
Mkuu hiko chupa ni inches ngapi?

Ni kweli mkuu uko sahihi...! Aisee hiyo chupa ni 55" tu kishkaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…