mimi kipindi nasoma chuo nilifikiri sana baadae yangu, ni nini ntakua nafanya baada ya kumaliza chuo, ntakua wapi!?, sikupenda kurudi home na kukaa tu, so nilianza na plan ya kuweza kuanza kujiingizia kipato so nikawanafikiri ni njia gani nitumie ili niweze kujiigizia kipato, nikapata wazo nianze na biashara, sasa mtaji na aina ya biashara ikawa mtihani, nilikua napenda sana kucheza video games(playstaion) so ikabidi nipate wazo la kufungua frem ya kuchezesha ayo magame, nikaanza na kununua moja moja kwa kujibana kwenye ela yangu ya matumizi, kila semister nikawa najibana nanunua tv na playstion yake, nikafanikiwa kununua kama 3 ivi, ikawa mtihani kwenye kodi sasa, mwaka wa mwisho nikaminya kidogo kwenye ada nliopewa na mzee nikafungua frem ya kuchezesha ayo magame, apa ikawa ndo mwanzo wangu wa kuanza kujiingizia kipato mwenyewe still bado nikawa napewa pesa ya matumizi home, ikumbukwe kipindi chote iki naishi hostel, kwaiyo baada ya kuweza kujitengenezea pesa mwenyewe ndo likaja wazo la kutafuta gettoh sasa na apo ndo nikapata gettoh na maisha yakaanzia apo, pamoja na yote lakn kipindi nafanya saving nilipitia kwenye kipindi kigumu sana cha kiuchumi.
nawashauri tu unapofikiria kutafuta gettoh fikiria na njia za kupata pesa walau ata kama ni kidogo laa sivyo unaweza jikuta unaingia pabaya kwasababu ya shida ya pesa maana gettoh sio kodi tu pekee kuna bills za kila mwisho wa mwezi kama umeme, maji, usafi nk.