Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Natoroka kulipa bili nakimbilia kwa mshkaji wangu nakutana na mshkaji wangu naye anatoroka kulipa bili anakuja kwangu.

Tukaenda zetu kukaa baharini kuanzia asubuhi mpaka saa nne usiku tukaenda kulala kwa mshkaji wetu mwingine na ndiyo tumeamka hapa.
Hahaha life la kininja
 
Nipo mkoa mmoja wenye baridi nyanda za juu kusini, nipo geto hapa godoro tu nimeliweka chini pamoja na jiko la gesi la kupikia, maisha yanasonga mdogomdogo.
Kila lakheri mkuu
 
Sikuwahi kutilia maanani sana huu uzi. Lakini kwa mara ya kwanza nimekutana na kitu. Link nilitumiwa na member wa jf mwaka juzi, lakini Leo baada ya kukosa cha kufanya nikaona niingie hapa. Mbarikiwe, naamini hadi kufika mwisho nitakuwa nimetoka na kitu.
Karibu sana mkuu
 
Mtaani kugumu! Hamna alierudisha mpira kwa kipa?
Vijana wameamua kukomaa kitaa mpaka kieleweke, japo kwenye upambanaji unapoona umezidiwa mashambulizi na mpinzani wako unaamua kuretreat ili ujipange upya inakuwa siyo udhaifu bali kupata muda wa kusoma mbinu za adui yako ili urudi upambane naye.

Maisha siku zote ni mapambano kuna kupiga, kuna kupigwa, kuna kupata matokeo suluhu na kukubaliano nayo.

Ila mbishi na mpambanaji asiyechoka na kukata tamaa ndiye siku zote hushinda.
 
Natoroka kulipa bili nakimbilia kwa mshkaji wangu nakutana na mshkaji wangu naye anatoroka kulipa bili anakuja kwangu.

Tukaenda zetu kukaa baharini kuanzia asubuhi mpaka saa nne usiku tukaenda kulala kwa mshkaji wetu mwingine na ndiyo tumeamka hapa.
Hii inaitwa "kheri ya jana ",unakula kwa namba, unalala kwa kubuni [emoji41][emoji41][emoji41]
 
Back
Top Bottom