Nimekua nikiufuatilia huu uzi tangu nipo shule mpaka nimeajiliwa kwenye kampuni fulani hapa jijini Dar na ninaishi nyumbani lakini ni muda sasa wa kwenda kupanga ila changamoto kila chumba ninachopelekwa na madalali hakina sifa ninazozihitaji mimi yaani sijui wenzangu mnatumia mbinu gani ya kupata magheto makali
Mkuu Kwani wewe unataka kupanga maeneo gani?
Madalali wanazingua sana, ata kama ana vyumba vizuri anaanza Kwanza kukuonesha vibaya ili ye apate tu ile hela ya kukutembeza
Njia nzuri ya kuanza kupanga Kwa mara ya Kwanza ni kutafuta ghetto Kwa kuulizia washkaji wanaokaa mazingira unayotaka wewe kuishi
Hutopata Kwa haraka lakini hakuna ubaya Kwa sababu home hujafukuzwa kwahiyo inakuwa rahisi watu kukuvumilia, ila ukajifanya una haraka utawapa sana hela madalali na kuishia kupanga nyumba ambayo unakuwa huna ata hamu ya kurudi nyumbani
Ukishapata ghetto lako la Kwanza hapo ndio utapanga aina ya ghetto la pili litakavyokuwa, ghetto la kwanza unaweza kukaa ata miez 3 tu kisha ukabadirishia Gia angani
Wakati me naanza kukaa ghetto sikuwa na mambo mengi kulingana na uchumi wangu hivo nikaangukia mitaa ya kigogo, Kwa sababu vyumba bei rahisi
ila baada ya miez 4 nikahamia Kumara suka, huko ndio sikuhangaika kabisa kutafuta nyumba kwakuwa mishe niliyokuwa napiga nilikuwa napiga kila siku kwahiyo ata muda wa kuonana na madalali nikawa sina
Nikaingia Instagram na kutafuta madalali wa kimara/ubungo/mbezi nikakuta wanapost nyumba na sifa zake, kwahiyo me nikacheki weee hadi nikaridhika, siku moja nikaomba hudhuru kwenda kucheki mjengo na kulipia moja Kwa moja maana kila kitu ushaona kwenye picha
Kama unataka nyumba yenye fence utachagua mwenyewe, tile's, gypsum, Aluminium window,mpya au used,self contained,kushea maji au umeme....! So unachagua mwenyewe unatakaje
Kwahiyo kama utakuwa uko Dar na unataka maeneo ya ubungo/kimara/mbezi/tegeta/bunju nk, jaribu kutembelea account za madalali mjini Instagram inaokoa muda lakini pia ina save gharama ambazo sio za ulazima