7seven
JF-Expert Member
- Mar 27, 2022
- 3,729
- 7,966
Hii inawatokea wanaume wengi, hatujaumbiwa hizi kazi lazima tuwe na wasaidizi wa hizi kazi.Hii ni kweli Mimi nilikuwa naipenda kupika na maswala ya kuoa nilikuwa sitaki kusikia. Nilipoanza kuchoka kupika hata miezi sita haikupita nakaweka wife geto
Fikiria umetoka safari ya wiki nje ya nyumbani kwako, una nguo chafu, vyombo vichafu, mazingira ya nyumba ni machafu yanahitaji kufanyiwa usafi, una uchovu wa wiki nzima , ongeza na upweke noma huwezi kujisikia vizuri lazima hapa uanze kufikiria mke.
Ila upande mwingine, umerudi unakuta maji ya moto ya kuoga, chakula kizuri, nguo ulizoacha ni safi, nyumba iko safi, kwanini hapa mwanaume usiwe na utulivu wa akili?
Ila hongera mkuu kwa kufanya maamuzi sahihi.Kila la kheri muishi vizuri na mke wako.