Mie nilianza rasmi kuvuta bange miaka ya 2001.
Iko hivi:
Baada ya kufeli darasa la saba mwaka 1998 (sababu sikuwa na akili darasani) kipindi hicho mzee akamind sana ikabidi nisepe zangu mikoani kusaka mishe.
Nimepiga zangu mishe mishe za town miaka kadhaa ndo nikakutana na jamaa mmoja alijulikana kwa jina la Dura. Alikuwaga mpigaji flani wa hizi mishe mishe za mjini ikiwemo wizi wa mafuta ya transformers na vyuma chakavu.
Huyo jamaa ndo alinishawishi nikajiunga na group lao tukaanza rasmi wizi wa mafuta ya transformers ambayo kwa kipindi hicho yalikuwa yanalipa sana na tulipata hela sana kipindi hicho, japo kazi ilikuwaga ngumu na ya hatari sana kiasi kwamba nilijikuta naanza kuvuta bangi na hao masela wangu.
Bange ilituongezea ujasiri na umakini kwenye mission zetu zote na kiasi flani tulifanikiwa kupata hela na kuanza kumiliki mageto ya maana (japo tulikuwa tumepanga).
Ila ndo hivyo hakuna marefu yasiyo na ncha, miaka kadhaa mbele likatokea tukio baya tukiwa kwenye transformer flani; kuna makosa yakatokea ikaripuka wenzetu watatu walikufa hapo hapo na tuliopona tulijeruhiwa vibaya sana kiasi kwamba ilichukua muda kuwa sawa na ndo ikawa mwisho wangu wa hizo mishe.
Ingawaje sasa nishakuwa mtu mzima ,ninamiliki biashara kubwa ya majeneza ndani na nje ya mkoa lakini huwa navuta bange mara moja moja japo kwa siri sana, maana mwonekano wangu haufanani kabisa (ni bonge la mtu kiasi kwamba wasiofahamu biashara yangu huwa wanajua ni boss flani kwenye kampuni) [emoji1787].
Je, wewe ulianzaje kuvuta huu mmea?
Kwa mara ya Kwanza navuta mmea wa Baraka ilikuwa 2007.
Nimenyonga kwa kutumia gazet kisha nikavuta japokuwa sikunyonga kawaida.
Nikavuta mmea wangu asee baada ya hapo nikachukuwa dafatari nisome sasa,asee niliona maandishi ni madogo sana na mwanga wa taa naona umepungua kishenzi asee. Ghafla bro kaangia ndani akaniambia asee umevuta bangi nilibisha kinoma. Kumbe ile kitu bana mvutaji haskii harufu hata kidogo.
Kuanzia siku hiyo skuvuta tena. Ilipofika 2022 nikiwa na washakaji zangu tunaendaga Sana club siku Za weekend, Sasa bana sku moja nikamwambia mwana anipe kitu. Nikavuta asee nilianza kucheka kinoma nikiwachek wale wanaocheza mziki pande ndani ya club afu naona hawana akili kabisa yaani wameacha kitanda usiku ule walipaswa walale.
Alafu baada ya muda maswali yakaanza kuja kwangu mwenyewe Sasa wale wanacheza mziki inamana wanafurahi sana au baadhi yao wanaekti kuwa Na furaha alafu hawana.? Vipi na Mimi hapa nimekuja hapa club kuwashangaa watu waliocha kulala na kuja kutumia pesa zao asee huu ni upumbavu.
Wakuu skuichukuwa muda mrefu nikawaambia wanangu tuamsheni asee muda umeenda.
Sasa nikawa nakula kitu kinoma asee.
Stimu zinakuja za kujiuliza maswali magumu sana kuhusu hii DUNIA kuhusu NGUVU KUU YA HUU ULIMWENGU (MUNGU)
maswali kuhusu kufanya kazi Kwa mtu na kufanya kazi mwenyewe faida na hasara yaani Ni balaa tu. Nachambua faida na hasara baada ya muda napata majibu alafu naanza kutabasamu mwenyewe.
Wakati mwingine nikivuta navuta nipo ndani inanijia picha kwamba flani anakuja hapa ndani asee Kweli baada ya muda kidogo jamaa huyo anakuja Na wakati mwingine naenda Mbali sana kihisia kwamba akija atafanya hivi atashika hiki ataongea hivi alafu Mimi nitamjibu hivi akianza kuleta stori ambazo sizitaki nakaa kimya nafanya kama sjamskia hivi.
Wakuu asee mambo ambayo nilikuwa Na waza mtu Yule akifika asee Kweli bana baadhi yake alikuwa anafanya yaani kwenye 100% ya mawazo yale basi unakuta anafanya 80% Na Kweli akianzisha stori ambazo sizitaki nakaa kimya nakuwa bize na simu.
Hii NGUVU ya mawazo yale sjui ilikuwaga nini wakuu.?
Kiufupi bangi haitaki makelele.
Kwa sasa NIMEACHA kuvuta kabisa.