Ulifikiria nini kujibatiza username unayoitumia JamiiForums

Ulifikiria nini kujibatiza username unayoitumia JamiiForums

jogoolakigoma. said:
Mkuu kwani hili neno lina maana gani 'tutigite'...na kwanini wewe hutigiti Jogoo la kigoma?

Tutigite-tucheze
Wi shavu ameneke-mwenye hasira apasuke.
Mr Q ki msingi, nimeathiriwa na hizi stori za kijasusi. Ambapo watu hujipachika majina kama Mr x, na mengineyo.(ikiwa ni harakati za kuficha majina yao halisi)
Sikuwa na sababu zaidi ktk uchaguzi wa username zaidi ya kuchukuwa jina mojawapo ya wahusika ktk stori hizo.
 
ilikuwa mnamo tarehe 29th September 2010 siku ya jumatano majira ya saa 4 na nusu hivi asubuhi nikiwa nimeshashiba chai na vitumbua vyangu, ndipo nikawa nimekaa na laptop yangu naperuzi JF kama kawaida, wakati huo nikiwa bado sijajiunga rasmi na jf lakini baada ya kuwa utamu wa JF unazidi kunoga ndo nikaamia sasa nijisajili rasmi siku hii. Jina langu sijui nini kiukweli halina maana yoyote...wakati wa kuregister JF sehem ya username niliwazaaa wee nikakosa cha kuweka, nikabaki nawaza "sijui niweke nini hapa..!!?:confused2::confused2:" maana nina username kibao katika mitandao tofauti na nyingine mpaka nlishazisahau..so wakati nawaza nikasema : bwana eeh mi sijui nini nijiite..afu nakaandika hapohapo sijui nini ...hii ndo historia yangu ya maisha yangu ya JF.
 
Last edited by a moderator:
Hongera sn wana Jf! Huwa naridhka sn kuona akina Fulani humu ndani mnaleta Mitazo ilokaa poa sn kama y huyu "Gwandagum"
{Katuduchu} jamaa yngu kitambo enzi hzo, alinipa jina hili alipoona cna makuu, watu wanaponitafutia 7bu tugombane. Akimaanisha "kujishusha/Kadogodogo"
 
Sure kina Aspirin, kongosho, Lara1,mtambuzi,Father of all,Fazaa,erickb52,Cacico,,hawa wote majina yao yana maana gani?

Mkuu wangu mi nimezaliwa kwa ajili ya kuwapunguzia watu (hasa wanawake) maumivu hasa ya kichwa yanayosababishwa na mastress makazini na majumbani.

Wakisoma posts zangu na kunigongea like, maumivu yanapungua taratiibu!

Ningongee like kama huamini. Uzuri wa tiba yangu haina side effect na inaambatana na ukaguzi kwa mabinti...
 
Mkuu wangu mi nimezaliwa kwa ajili ya kuwapunguzia watu (hasa wanawake) maumivu hasa ya kichwa yanayosababishwa na mastress makazini na majumbani. Wakisoma posts zangu na kunigongea like, maumivu yanapungua taratiibu! Ningongee like kama huamini. Uzuri wa tiba yangu haina side effect na inaambatana na ukaguzi kwa mabinti...[mkuu sina mbavu kwa kweli, umenipa a very definite definition of your username!
 
Asprin said:
Mkuu wangu mi nimezaliwa kwa ajili ya kuwapunguzia watu (hasa wanawake) maumivu hasa ya kichwa yanayosababishwa na mastress makazini na majumbani. Wakisoma posts zangu na kunigongea like, maumivu yanapungua taratiibu! Ningongee like kama huamini. Uzuri wa tiba yangu haina side effect na inaambatana na ukaguzi kwa mabinti...[mkuu sina mbavu kwa kweli, umenipa a very definite definition of your username!
 
Baada ya kugundua wengi humu mnatalk nonsense+pumba za kutosha ikabidi nije Mkare_wenu to put everything clear
 
Jaguar,hii ilitokana na mimi kumkubali sana jaguarpaw katika filamu ya apocalypto.
 
mysteryman said:
...Nadhani utakuwa mtu mwenye "maajabu" sana.Lakini utakapodhihirisha maajabu ndipo siri ya wewe ni nani itakapotoka!
 
Langu sababu ya tumia ID yangu nilishaitoa fuatili post zangu.
 
mi napenda kuwa halisi hivyo sikuona umuhimu wowote hata wa kutumia jina la kuchonga,mc ni kazi yangu mimi mshereheshaji na Tilly Chizenga ni majina yangu halisi
 
Mi mwenzenu pesa tangu napata akili,nimezaliwa kwenye pesa na bado naelea elea kwenye mapesa ndo mana nkajiita bwana mapesa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Jina hili nilipewa na wangu wa moyoni kama miaka 35+ iliyopita nikiwa 'O' level.
 
langu mimi limekuja kwasababu sikubali na kimoja nilichokuwa nacho ndio maana ikaleta Tamaa
 
Mkare_wenu said:
[Naamini utakuwa mpenzi wa bongo fleva na kati ya wimbo ulioupenda ni ule wa P-Unit .Ndiyo maana upo tofauti na Jaguar anayeamini kuishi vizuri na watu na kukumbuka maadili yanayotolewa na wazazi...Wapenda bongo fleva wengi wanajiona wako juu ya wenzao na hakuna tatizo vile binadamu tunafanana lakini hatuendani.
 
Kuna siku nilimpa nyau wangu valuu 6, alilewa sana na akawa bwii, ndo ikabidi nianze kuitumia hiyo ya Nyaubwii
 
Back
Top Bottom