Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?


Mkuu naomba niku inbox unipe namna hapa
 
Duuuh hongera sana mkuu
 
Mwaka 2016 baada ya kumaliza chuo,Maisha yalikuwa magumu Sana,nilikuwa siwezi hata kupata vocha na Kula kulikuwa ni kwa manati.nikaanza kufanya kazi za saidia fundi kujenga nyumba,,KWA KWELI NILIDHARAULIKA SANA PALE MTAANI!!,niki-apply kazi siitwi hata kwenye interview,nikipeleka CV door to door,wanaishia tu kusema CV ni nzuri lakini kazi sipewi!!home hali ni Mbaya,nikimuangalia mama nasikitika sana, mana Kipindi niko shule ilikuwa inafika kipindi anauza ardhi na vitu muhimu ili nisome, lakini ajira hakuna!!Mwaka 2017 nikaweka vyeti pembeni nikaanza kuokota vyuma chakavu(screper)kwenye Madampo na Mahali popote pale nitakapo pata ilimradi tu isiwe ya kuiba,ilikuwa ni fedheha lakini nilikuwa sina namna nyingine,mwezi wa Saba nikawa nimefikisha tani1½ nikauza nikapata laki5,baada ya hapo nikanunua piglets8 wa kienyeji@30000,nikatumia kama Laki2½ hiv,2wakafa maana nilikuwa nawafuga kibabe, wakabaki6 nikawakuza hadi mwezi3,2018,nikaja kuuza kila mmoja lak1.75 nikapata million 1na elf50..nilikaa mwezi mzima nikitafakari ni biashara gani naweza kufanya..baada ya hapo niliamua kufanya biashara za kujumua mpunga mwezi 5,,nikawa naenda Mbalari na Kamsamba-ya ziwa Rukwa.nilikuwa nachukua shambani kwa Bei rahisi nakuja mjini Mbeya nakoboresha nauza. Mwezi wa 9 pesa ikawa imeshakua million 2.8.msimu wa mpunga ukawa umeisha.nikarudi home kutafakari tena nifanye nini..siku moja napitia baadhi ya timu barani ulaya na africa nikaona Kama Kuna fursa flani,.(maana wakati niko kwenye msoto,ilibidi nijifunze kubeti) ,nikasema potelea mbali wacha nirisk elf 30 leo,nikaingia parimatch wakati ule walikuwa hawakati Kodi nikaweka Odd 35.6,KWELI NIKAAMINI MWENYE NACHO HUONGEZEWA,,tiketi ika-WIN nikapata mili1.10 hiv.,wakati nafanya kazi za saidia fundi hakuna tiketi niliyo bet na ika-WIN..na hakuna pesa niliyopata kiurahisi Kama hii..baada ya hapo nikawa nafanya scalping natafuta odd ndogo nastake pesa kubwa nikakuta pesa inakuwa kiutani utani hadi najishangaa..sikumoja nikajiRISK tena nikaweka STAKE ya mill.2 kwa ODDS.3 nikapata milioni 6,sikuamini Kama ni pesa yangu,,NIKAJIULIZA MBONA KIPINDI KILE KWENYE MSOTO MAMBO HAYAKUWA HIVI,?!maana niliitumia takriban karibu miezi7 kupata Tani moja ya vyuma chakavu!!BAADAE ukafika msimu wa kilimo Nikaenda Mbeya vijijini kulima viazi mviringo nikatumia Kama milio1.8,nikavuna nikapata millioni3.4.mpaka Sasa naendelea kujishughulisha na kilimo ufugaji na NA PESA YANGU TAYARI ILISHAVUKA MILION10,naelekea 20mill.
 
Maisha haya! Input yako ya ntaji mbona haiendani na output ya faida?

Mimi niliwekeza milion 1.9 na kila siku nikawa natengeneza net profit ya 300k kwa miezi kadhaa!
Biashara Gan mzee
 
Ukifikisha mil 20 unataka uzifanyie nini
 
Nilipata kazi kwenye mradi ambayo monthly plan ya kila mwezi ni lazima nibakie na 3.5m -4m kila mwezi..

Km nimeomba million sita ya kazi basi 3.5m ni yangu kwahiyo mwendo ulikuwa huo kwa kama miaka 3,baada ya hapo wabongo walivyo wangese wakaanza kuleta uswahili kwenye pesa za wezi wa madini yetu ikawa inashuka tu mara 2m mara million moja kufika mwaka wa tano wa kazi hela ya kupiga ilikuwa 500k tu kwa mwezi...


Kwahiyo million 10 niliipataga ndani km ya miezi mitatu ya kaZi.Nashukuru sikuwa na mambo mengi hivyo ile pesa ilinifikisha mbali.Mradi umeisha nimepata kazi kwenye kampuni eti deal kwa mwezi unapata km 200k tu [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] yaani maisha haya .

Nikikumbuka nilipotoka basi nacheka tu
 
Ushauri mzuri, sema changamoto ipo hapa "Tafuta biashara ndogo ndogo ufanye ili zikuongezee kipato", kupata hiyo "biashara ndogo ndogo" ndio changamoto kwa walio wengi wetu
 
Hapo kwenye kuuza laki nane kwa siku hapo mmmh kweli magenge yanalipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…