Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Usa naishi San Diego california. Hio $5000 ilikuwa enzi hizo. Sasa hivi mshahara ni $15000 au zaidi kwa mwezi. Ni kazi ya travel rn. Mfano wake ni lini hii hapa chini: Au google, apply for travel RN san diego, california.. hii hapa inalipa $3360 kwa wiki. Taxes toa 10% hivi.

Yaan mkuu ushanichanganya kabisa na huu ushuhuda
 
Mimi ni raia wa Tz, na kwa USA ni permanent resident. Kwa hio sishughuliki na embassy tena. Unaruhusiwa kukaa nje ya USA kwa muda mrefu tu, ila inabidi ufuate rules fulani za US immigration.
Sawa sawa mkuu, maana kuna mtoto wa shangazi alikuwa ameolewa huko kaachika akarudi huku akakaa wee ( like five yrs) naona wanamkata jina hapo osterbay
 
Ndiyo hivyo. Shida kubwa watu wengi wakienda shule kidogo anaona biashara za mtaani ni kama kushika uchafu. Kuna kijana mmoja mwalimu s/msingi wa kichaga alipanga chumba kwetu akaona fursa akafungua genge la mbogamboga hapo nje kalitengeneza kwa mabanzi tu ya kawaida. Saizi anauza laki 8 kwa siku. Tunataka kuanza kumtoza kodi lakini tunajishtukia kwa aibu, coz ni kasehemu ambacho wala hatukujua kuwa ni potential. Sasa mwambie graduate wa Mzumbe au Udsm afungue genge.
Mbona umeenda mbali sana, wewe ambaye upo hapo ni kwenu mbona hukufungua hilo genge ama we sio graduate 🤣🤣🤣
 
Sawa sawa mkuu, maana kuna mtoto wa shangazi alikuwa ameolewa huko kaachika akarudi huku akakaa wee ( like five yrs) naona wanamkata jina hapo osterbay
Nampa pole sana. Ukiolewa na US citizen unapewa uraia, lakini ndoa ikivunjika, unaweza poteza uraia pia. Sijajua situation yake. Ila pia kukaa sana nje ya USA, ni tatizo usipofuata sheria za US immigration.
 
Aliupoteza uraia ndio, ila sasa alinyang'anywa watoto na huyo mlatino, ndo anataka arudi akalete battle huko
 
Ukiona mtu anasave hadi inafika kiasi hicho bila kuzila ina maana anazo za kuzila hio ni ziada. Vile vile sio kwamba Hana cha kufanyia, za kufanyia shughuli nyingine zipo zinafanya vitu hizo zinazowekwa ni ziada.
Mwingine kwenye mapato yake ya biashara anatenga kiasi fulani cha kodi ya pango la hio biashara na gharama nyingine zitakazojitokeza.
Ila nimekuelewa wengine kila hela ikipatikana inapata matumizi/kazi.
Yah, savings ni matokeo ya kuwa na excessive earnings. Huezi kuwa unapata elfu 5 ambayo haitoshi hata milo kwa siku kisha uniambie utasave...Unasave nini hapo?

Tofauti na mtu ambaye anapata maybe 15K per day. Atakula 7K kisha 7K ingine anai save. Inawezekana kabisa. Kitu kimenishinda ni kujitesa na njaa ati kisa na save. Mi huwa nakubaliana na hali halisi tu sina kipato cha ku save natulia na kubuni mbinu tu nitapataje zaidi.

Raha ya ku save uwe na excess cash.
 
Aliupoteza uraia ndio, ila sasa alinyang'anywa watoto na huyo mlatino, ndo anataka arudi akalete battle huko
Mambo ya ndoa ni magumu sana sana hasa watoto wakiwepo. Kisheria, huwezi ondoka na watoto kama mwenza wako hajakubali. Kwa hio kama aliondoka bila ex wake kukubali, hapo ndio tatizo kubwa sababu inakuwa child kidnapping kwa USA hata kama ni watoto wako.
Nampa pole na kumtia nguvu asikate tamaa. Kila kitu kinawezekana. Japo itachukua nguvu nyingi na muda mwingi na resources nyingi sana.
 
Haya mambo mara nyingine inawezekana kabisa mkuu.
Mie ni suppliers wa raw materials kiwanda fulani(japo siko peke yangu). Ila mzigo wa kujaza gari 1(pulling) unanigharim 1.2M. Mwenye kiwanda anatuma gari kwa gharama zake.
Ukifika kiwandani mie napata net profit sio chini ya 2M kwa gari 1. Na ni kazi ya siku 2 au 3 tu gari imejaa.
Kila mtu ana akili yake katika kubuni miradi na ku realize profits. Ndio maana kwa 50M hio hio ukipewa wewe na mimi lazma mitego itatofautiana tu. Imagine mwenzio anapata laki1 kila siku ila wewe unapata laki 2M within 3 days. Tofauti ni kubwa sana.
 
Nimewahi sana na nikihisi tu ni cha wizi huwa nina team yangu ya manunuzi (sinunui mimi)

nawatonya wanakuja,nawapa hela wananunua kisha wanasepa,muuzaji hatojua kama n mimi

nimenunua na team yangu ya manunuzi haikai mtaa niliopo hao wanakuja kwa case maalum tu
Hii biashara ina hela ila ni risky, siku ikiletwa mali ya Contawa ukakutwa nayo wewe basi umeisha.
 
Kila mtu ana akili yake katika kubuni miradi na ku realize profits. Ndio maana kwa 50M hio hio ukipewa wewe na mimi lazma mitego itatofautiana tu. Imagine mwenzio anapata laki1 kila siku ila wewe unapata laki 2M within 3 days. Tofauti ni kubwa sana.

Mkuu alisema 2M yaan 2 million si laki mbili
 
Back
Top Bottom