Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Nyie mnaojiona wasomi na wajuaji ndio wachawi nambari moja, uku adharani huwa mnajifanya kuupinga ushirikina kumbe gizani ndizo kazi zenu.

Hakuna watu washirikina kama hawa wasomi na wanaojiita wamestaarabika hawa ndio washenzi kuliko hata hao wajinga, ukitaka ushahidi, nenda kwa waganga utaona wateja wao wakuu ni ninyi wasomi na wajuaji wa mambo mnaoficha tabia zenu kupitia ubishi ubishi.

Ushirikina hauwezi kuzimwa kwa namna mnayoitaka ninyi bali elimu ambayo si hiyo mliyonayo ninyi vilaza wa shule za mkoloni.

Nikipinga uwepo wa Mungu nakua Mungu? Utaanza kuniabudu 😅 Nyie waamini ushirikina ni empty set kabisa can't reason kabisa ndo maana mnaibiwa kiboya. Smh
 
Mimi nimekaa pale, waniroge tuone kama kweli uchawi upo

1718749236461.jpeg
 
unaongea kujifurahisha mkuu na hakuna ujualo

wakenya kuamini watanzania kuwa waganga ni kweli ila tz hawaamini wakenya wao wana amini wakongo

asa unakataa hakuna majini ikiwa yametajwa hadi na vitabu vya dini alafu unataka kuleta ubishi wa kitoto kwe
Huyu ameamua kufurahisha genge achana nae...Mimi Niko serious hapa najaribu kufungua codes ili vijana wanaoteseka Na haya mambo Bila wao kufahamu washtuke Ila yeye analeta mambo ya kisengerema hapa..
 
Uchawi upo mkuu, kuna mwingine nimeukuta daressalam hasa mitaa ya uswahilini mtu anaoga madawa ya kuondoa nuksi mwilini mwake halafu yale maji anayojisuuzia mwilini anayamwaga kwenye njia ambayo watu wanapita hasa njia za vichochoroni,..ebwanaee nyote mtakaopita njia hiyo mapema hasa asubuhi inakuwa imeisha hiyoo yaani moja itakuwa haikai wala mbili haikai...ukija kugundua muda umeenda
Hata mimi nilipoenda Dar nilikuwa nashangaa kuna mdada mama ntilie,ikifika usiku alikuwa anaogea nje getini na ni kila siku,na kuna siku naingia bafuni asubuhi nikashangaa nakuta unga mweusi ndani ya kijibahasha na kimeandikwa ogea ndani ya siku 4,na hapo bado wale wa kuvunja nazi njia panda
 
Du. Hapana. Mimi ni ''bush star''. Nimezaliwa sehemu ambazo hata kuonekana kwa bundi kunaleta kitimtim.
Sasa inakuaje hujawahi kurogwa. We unazijua familia za kiswahili vizuri? Mtu ukila ugali na dagaa wa kukaanga watu wote wajue. Kuna husda huko za ajabu... ukiwa jobless grauduet kutok familia hizo unawez kujinyonga
 
Mwanzoni wakati nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa siamini kabisa haya mambo lakini kadiri nilivyokuwa nakuwa ndio nikaanza kufahamu kuwa kweli uchawi upo, Na mtu akiamua kukuharibia au kukuchafua ndio imeisha hiyoo..uliishawahi kukutana Na mtu ambae Kila janga lazima yumo tena kwa babati mbaya..

Basi kuna ushirikina mmoja upo huko Kagera wanautumia sana wahaya , kwa kirugha unaitwa "nyaamazi" yaani mpakwa mavi au kitu chochote chenye harufu mbaya, uchawi huu mshirikina au mchawi anaetaka kukuharibia uwe ni mtu wa mikosi mwanzo mwisho, Huwa anategeshea Na kukuibia Ile nguo unayoipenda sana kuivaa unaweza kuwa ni tisheti au suruali,..ataipeleka kwa mganga Na kuipaka huo uchawi unaoitwa "nyaamazi" Na baada ya hapo uirudisha kwa kificho Bila ya wewe kufahamu au kujuwa.. mchezo unaanza pale siku utakapoivaa au kuichanganya Na nguo nyingine kama sio mtu wa ibada sana lazima utaanza kuona rangi zote .

Kama ni mtumishi wa ofisi flani Basi utaanza kuona mabadiriko wafanyakazi wenzako wataanza kuku kataa, bosi wako anakuona kama kero tu, jamii inayokuzunguka imani yao kwako inapungua, ikitokea tatizo Basi wanaanza Na wewe, unakuwa huaminiki Na wala hupendeki Na yeyote, Kila unachokifanya kinaonekana ni hovyo tu, hata ufanye jambo zuri vipi...haya nimeyafahamu baada ya kutembea, elewa Neno KUTEMBEA..


uchawi upo hasa huku Africa (shit hole countries) tujikinge kama ni mtu wa ibada Basi sali sana, kama ni mtu wa ndumba Basi oga sana....
Haya mambo yanavuruga na kupunguza nguvu kazi ya taifa
 
😂 😂 😂
Acha kabisa Mkuu haya mambo yapo sana, lakini kwa sababu ya Unafiki wetu huwa hatutaki kuyaandika.

None, but yourself can free your mind. Msiwekezeke sehemu ambazo hazina tija. Ushirikina unatudumuza sana waafrika sababu hautaki tufikirie zaidi ya hapa tulipo. Kila kitu tumerogwa
 
Mtu akijua jina lako na la mama yako anakufanyia uchawi.

Akishindwa kujua jina la mama yako atakufanyia uchawi kwa kuchukua vitu vyako vya karibu kama mavazi, nywele zako kwenye kitana n.k

Akishindwa hayo atakutegeshea kwenye mazingira ambayo unayapenda. Kama ikiwa chakula ni kwenye chakula hata kwa kukununulia, njia unayopita, mahali unapopenda kukaa sana.

Mara zote anayekufanyia uchawi ni mtu ambaye yupo karibu nawe.

Kuna wengine wanakupiga pini kwenye nyumba yenu ya wazazi wenu. Yaani ninyi mpo kwenye makazi yenu lakini watu wanafanya mambo yao kisha wanayazika kimazingara hapo nyumba mliyokulia kwa wazazi wenu.

Ukipigwa hii pini hata usomewe visomo vipi haufungui hii pini. Kila kiongozi wa dini utamuona hafai. Utakumbwa na nuksi, mikosi, gari ukikaa wewe haiwaki akiendesha mwengine inafanya kazi. Ukipeleka kwa fundi inachekiwa haina tatizo na inakuzimikia wewe tu. Pesa hazikai kimazingara zinapotea. Yaani ndiyo unafilisika hivyo!

Ili uichomoe inabidi kisomo kikafanywe kwenye nyumba uliyokulia huko kwa wazazi wako kwa sababu mambo yao ndiyo wameyazikia huko. Haya mambo usiombe yakukute.

Mdogo mmoja na ni wa mfanyabiashara mkubwa sana hapa Bongo na wana miliki timu huwa wana Sheikh wao wanamtoa Oman. Wanamgharamikia gharama zote za kuja na kuondoka.
Sema hivyo vyote unaweza kuvitoa kwa powers zilizomo ndani yako. Mtu mpk anafikia kukuloga na mwili wako umekubali kulogeka unatakiwa utumie vitu vilivyomo ndani yako kujinasua.
 
Mi mpaka nishuhudie huo uchawi Kwa macho yangu vinginevo ni stori tu za abunuwas sina mda wa kuamini visivoonekana . Waafrika vichwani wamejaa mawazo ya kishirikana tu mara kwenda Kwa waganga , juzi mtoto wa miaka miwili albino kauwawa kwasababu ya mijitu iliyoamini uchawi😥😠 Yani mtu unatoa makafara kibao na Bado huwapiti akina Elon musk na bil gates Kwa utajiri, shame on you. Sijawahi kuskia hadithi za kishirikina uko ulaya sijui mtu kapaa na ungo anawanga uchi. Uko ulaya stori za kusadikika labda ni zombie na ma vampire na aliens ila Africa ni uchawi wa kuruka na ungo na kuroga uchi usiku sasa unajiuliza ko huu uchawi upo Africa tu🤔 uko uzunguni ata sisikiagi mambo ayo ety mtuu kapandisha mashetani sijui katoa kafara.
 
😂 😂 😂 😂
Wengi humu ni Wanafiki tu huo uchawi umeshaandikwa mpaka kwenye vitabu vitakatifu vya imani nashangaa humu mnajifanya Wanafiki, halafu unaweza ukakuta wengi wenu humu ni Washirikina wakubwa
 
Mi mpaka nishuhudie huo uchawi Kwa macho yangu vinginevo ni stori tu za abunuwas sina mda wa kuamini visivoonekana . Waafrika vichwani wamejaa mawazo ya kishirikana tu mara kwenda Kwa waganga , juzi mtoto wa miaka miwili albino kauwawa kwasababu ya mijitu iliyoamini uchawi😥😠 Yani mtu unatoa makafara kibao na Bado huwapiti akina Elon musk na bil gates Kwa utajiri, shame on you. Sijawahi kuskia hadithi za kishirikina uko ulaya sijui mtu kapaa na ungo anawanga uchi. Uko ulaya stori za kusadikika labda ni zombie na ma vampire na aliens ila Africa ni uchawi wa kuruka na ungo na kuroga uchi usiku sasa unajiuliza ko huu uchawi upo Africa tu🤔 uko uzunguni ata sisikiagi mambo ayo ety mtuu kapandisha mashetani sijui katoa kafara.
Hiyo ndio afrika
 
Back
Top Bottom