Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Mwanzoni wakati nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa siamini kabisa haya mambo lakini kadiri nilivyokuwa nakuwa ndio nikaanza kufahamu kuwa kweli uchawi upo, Na mtu akiamua kukuharibia au kukuchafua ndio imeisha hiyoo..uliishawahi kukutana Na mtu ambae Kila janga lazima yumo tena kwa babati mbaya..Basi kuna ushirikina mmoja upo huko Kagera wanautumia sana wahaya , kwa kirugha unaitwa "nyaamazi" yaani mpakwa mavi au kitu chochote chenye harufu mbaya, uchawi huu mshirikina au mchawi anaetaka kukuharibia uwe ni mtu wa mikosi mwanzo mwisho, Huwa anategeshea Na kukuibia Ile nguo unayoipenda sana kuivaa unaweza kuwa ni tisheti au suruali,..ataipeleka kwa mganga Na kuipaka huo uchawi unaoitwa "nyaamazi" Na baada ya hapo uirudisha kwa kificho Bila ya wewe kufahamu au kujuwa.. mchezo unaanza pale siku utakapoivaa au kuichanganya Na nguo nyingine kama sio mtu wa ibada sana lazima utaanza kuona rangi zote .kama ni mtumishi wa ofisi flani Basi utaanza kuona mabadiriko wafanyakazi wenzako wataanza kuku kataa, bosi wako anakuona kama kero tu, jamii inayokuzunguka imani yao kwako inapungua, ikitokea tatizo Basi wanaanza Na wewe, unakuwa huaminiki Na wala hupendeki Na yeyote, Kila unachokifanya kinaonekana ni hovyo tu, hata ufanye jambo zuri vipi...haya nimeyafahamu baada ya kutembea, elewa Neno KUTEMBEA..uchawi upo hasa huku Africa (shit hole countries) tujikinge kama ni mtu wa ibada Basi sali sana, kama ni mtu wa ndumba Basi oga sana....
Wasambaa wanao huo uchawi wanauita KISIMO.
Nadhani Tanzania kwa roho mbaya msambaa Ni wa tatu. Namba moja of course Ni mngoni akifuatiliwa na mpare.
Msambaa hapendi maendeleo ya MTU yoyote hata ndugu yake toka ntoke.
 
Hii nchi watu wajinga bado wengi sana. Tatizo sio katiba wala ccm ila watu wajinga bado wengi. Mleta uzi na ndevu zake anaamini ujinga kama huu tena anashare kabisa. Smh

Kuamini uchawi ni ugonjwa wa akili.
kwamba wewe unafahamu zaidi kuliko manabii walio utaja uchawi kwenye vitabu

hauamini uchawi ila una amini kitabu kitakatifu una akili timamu kweli
 
Waamini uchawi utawajua tu. 1. Kwao mganga kiboko ni yule anayevaa matambala na kukaa kwenye vijumba vya udongo au nyasi tena porini kabisa. 2. Kuna kipindi nilitembelea Kenya, nikakuta wanaamini waganga wakali wako Tanzania na washirikina wengi walikuwa wanavuka mpaka kuja kwa waganga wa Tanzania. Ukienda kwa upande wa Tanzania nako, watu wengi wanaamini waganga wakali wako Kenya, na watu wengi hupoteza fedha kwenda Kenya kufuata waganga. Sijui kwa nini hizi dhana zipo sana i.e mganga mzuri ni yule mwenye maisha ya kifukara, bibi mzee au babu mzee, anaishi sehemu za porini na yuko mbali na pale mteja anapokaa. NB: hakuna uchawi na nishaomba sana kama kuna mtu mwenye nyumba yenye majini au mizimi awasiliane na mimi niende nikalale huko. Au sehemu yoyote ya kukatisha yenye majini.
unaongea kujifurahisha mkuu na hakuna ujualo

wakenya kuamini watanzania kuwa waganga ni kweli ila tz hawaamini wakenya wao wana amini wakongo

asa unakataa hakuna majini ikiwa yametajwa hadi na vitabu vya dini alafu unataka kuleta ubishi wa kitoto kweli
 
kwamba wewe unafahamu zaidi kuliko manabii walio utaja uchawi kwenye vitabu

hauamini uchawi ila una amini kitabu kitakatifu una akili timamu kweli

Nani kakwambia naamini bedtime stories?
 
Mpaka anachukua nguo yako unayoipenda na kuirudisha, wewe unakuwa wapi??
Km unahisi hivyo kunywa mkojo wako wa asubuhi ila usiwe wa pombe.
Mtu akijua jina lako na la mama yako anakufanyia uchawi.

Akishindwa kujua jina la mama yako atakufanyia uchawi kwa kuchukua vitu vyako vya karibu kama mavazi, nywele zako kwenye kitana n.k

Akishindwa hayo atakutegeshea kwenye mazingira ambayo unayapenda. Kama ikiwa chakula ni kwenye chakula hata kwa kukununulia, njia unayopita, mahali unapopenda kukaa sana.

Mara zote anayekufanyia uchawi ni mtu ambaye yupo karibu nawe.

Kuna wengine wanakupiga pini kwenye nyumba yenu ya wazazi wenu. Yaani ninyi mpo kwenye makazi yenu lakini watu wanafanya mambo yao kisha wanayazika kimazingara hapo nyumba mliyokulia kwa wazazi wenu.

Ukipigwa hii pini hata usomewe visomo vipi haufungui hii pini. Kila kiongozi wa dini utamuona hafai. Utakumbwa na nuksi, mikosi, gari ukikaa wewe haiwaki akiendesha mwengine inafanya kazi. Ukipeleka kwa fundi inachekiwa haina tatizo na inakuzimikia wewe tu. Pesa hazikai kimazingara zinapotea. Yaani ndiyo unafilisika hivyo!

Ili uichomoe inabidi kisomo kikafanywe kwenye nyumba uliyokulia huko kwa wazazi wako kwa sababu mambo yao ndiyo wameyazikia huko. Haya mambo usiombe yakukute.

Mdogo mmoja na ni wa mfanyabiashara mkubwa sana hapa Bongo na wana miliki timu huwa wana Sheikh wao wanamtoa Oman. Wanamgharamikia gharama zote za kuja na kuondoka.
 
Hivi kwann Mungu aliruhusu uchawi uwepo? Kuna watu wamehribiwa maisha yao sababu ya uchawi,wengine ni machizi sababu ya uchawi,kuna waliokua vizuri kiuchumi ila wamefirisika baada ya kurogwa, yaan ni kero juu ya kero, wezi nao na wazinzi wana dawa za kichawi kufanikisha ayo,
Kwann Mungu aliruhusu uchawi ana faida nao gani yeye?
Wewe kama ni mtu wa dini piga maombi/visomo mtu akijaribu mambo yake ya uchawi afe na akatike kichwa kama amechinjwa.
 
Hii nchi watu wajinga bado wengi sana. Tatizo sio katiba wala ccm ila watu wajinga bado wengi. Mleta uzi na ndevu zake anaamini ujinga kama huu tena anashare kabisa. Smh

Kuamini uchawi ni ugonjwa wa akili.
Nyie mnaojiona wasomi na wajuaji ndio wachawi nambari moja, uku adharani huwa mnajifanya kuupinga ushirikina kumbe gizani ndizo kazi zenu.

Hakuna watu washirikina kama hawa wasomi na wanaojiita wamestaarabika hawa ndio washenzi kuliko hata hao wajinga, ukitaka ushahidi, nenda kwa waganga utaona wateja wao wakuu ni ninyi wasomi na wajuaji wa mambo mnaoficha tabia zenu kupitia ubishi ubishi.

Ushirikina hauwezi kuzimwa kwa namna mnayoitaka ninyi bali elimu ambayo si hiyo mliyonayo ninyi vilaza wa shule za mkoloni.
 
Kuna huu uchawi wa kupewa mikosi na kufungwa kupitia pesa
Yaani una hela ukipokea kutoka kwa mtu fulani ni kuandamwa na. Mikosi tu

Mimi mwaka wa tatu huu napewa pesa yenye mabalaa na watu watatu tofauti lakini wa ofisi moja na wote wana asili ya milimani

😢
 
Mkuu katika pita pita yako umehai kutana na mafundi wa ukweli? Maana wengi hapa mjini matapeli sana, eti fundi anavaa cheni na ana account insta!
😂😂😂 unakuta anacheza mbaka forex sijui crypto curency
 
Back
Top Bottom