Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Huwa namshangaa sana mtu anaesema uchawi haupo😀😀😀 Nina imani yanakuwa
Mkuu huwezi amini yameshanikuta sana haya majanga tena kwa kusomewa dua tu. Mtu unatapika nywele na viini vya njano kama mayai, kubwa kuliko 1 month ago tena ilikuw6ni kama incident tu Boxer yangu imebanwa kufuri na t-shirt yangu kama miaka 10 iliyopita ilifukuliwa. Imagine 😅
Aisee
 
Uswahilin kuna mambo sana mkuu. Mm niliwh kukaa mazibgira flan hiv wamakonde kibao. Nilisaga meno, hali si hali. Hupati hata mia wiki nzima. Ilifika kipindi natoka pale kwenda Kunduchi Mtongan nd napigiwa na kupata sim za hela. Ilifika kipindi unapogiwa sim ya hela ukiwa kunduchi ukirud home tu ile dili lazim ipinde 😁
Ulikua unaishi sehemu ya kuitwa maputo bilashaka
 
Hivi kwann Mungu aliruhusu uchawi uwepo? Kuna watu wamehribiwa maisha yao sababu ya uchawi,wengine ni machizi sababu ya uchawi,kuna waliokua vizuri kiuchumi ila wamefirisika baada ya kurogwa, yaan ni kero juu ya kero, wezi nao na wazinzi wana dawa za kichawi kufanikisha ayo,
Kwann Mungu aliruhusu uchawi ana faida nao gani yeye?
 
Mimi huwa naomba yanikute lakini cha ajabu hayanikuti. Unajua nyumba yenye majini au mashetani na imeshindikana watu kukaa humo? Kama unaijua niambie nikalale humo.
IMG_20240614_182631_687.jpg

Aisee hakuna mtu anayejua shida au matatizo huwa inakuja vipi?
 
Mwanzoni wakati nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa siamini kabisa haya mambo lakini kadiri nilivyokuwa nakuwa ndio nikaanza kufahamu kuwa kweli uchawi upo, Na mtu akiamua kukuharibia au kukuchafua ndio imeisha hiyoo..uliishawahi kukutana Na mtu ambae Kila janga lazima yumo tena kwa babati mbaya..Basi kuna ushirikina mmoja upo huko Kagera wanautumia sana wahaya , kwa kirugha unaitwa "nyaamazi" yaani mpakwa mavi au kitu chochote chenye harufu mbaya, uchawi huu mshirikina au mchawi anaetaka kukuharibia uwe ni mtu wa mikosi mwanzo mwisho, Huwa anategeshea Na kukuibia Ile nguo unayoipenda sana kuivaa unaweza kuwa ni tisheti au suruali,..ataipeleka kwa mganga Na kuipaka huo uchawi unaoitwa "nyaamazi" Na baada ya hapo uirudisha kwa kificho Bila ya wewe kufahamu au kujuwa.. mchezo unaanza pale siku utakapoivaa au kuichanganya Na nguo nyingine kama sio mtu wa ibada sana lazima utaanza kuona rangi zote .kama ni mtumishi wa ofisi flani Basi utaanza kuona mabadiriko wafanyakazi wenzako wataanza kuku kataa, bosi wako anakuona kama kero tu, jamii inayokuzunguka imani yao kwako inapungua, ikitokea tatizo Basi wanaanza Na wewe, unakuwa huaminiki Na wala hupendeki Na yeyote, Kila unachokifanya kinaonekana ni hovyo tu, hata ufanye jambo zuri vipi...haya nimeyafahamu baada ya kutembea, elewa Neno KUTEMBEA..uchawi upo hasa huku Africa (shit hole countries) tujikinge kama ni mtu wa ibada Basi sali sana, kama ni mtu wa ndumba Basi oga sana....
 

Attachments

  • IMG-20240618-WA0026.jpg
    IMG-20240618-WA0026.jpg
    98.8 KB · Views: 13
Huyo ulie mtag nadhani alifanikiwa kupata connection maana zile nyuzi zake za kutafuta fundi haandiki kwa sasa. Saizi ana andika nyuzi za kutaka ushauri wa madili ya mamilioni ya pesa. Hatari sana

Mbona kama katapeliwa tapeliwa sana, au anatuchora kumbe alipata mganga konki

Aigle usitufanyie hivi, naomba namie mganga basi, kuku nnao wa kutosha
 
Huwa namshangaa sana mtu anaesema uchawi haupo😀😀😀 Nina imani yanakuwa hayajamkuta.
Tangu nilipokutana na mmoja ya vigogo wakubwa wa serikali nchi jirani ambaye sikuwahi kumwona live zaidi ya kwenye tv
Lakini siku hiyo alipotimba kwa mtaalamu wa ndumba na gari lake akiwa na mwanaye na mkewe usiku wa manane kwa mtaalamu wa ndumba analia machozi alikuwa na msala mkubwa ambao ulihatarisha ajira yake mtaalamu akampiga setting usiku kucha asubuhi anawasha gari kuondoka wengi tuliolala pale kwa mganga tulimwona hakuna aibu wala kuogopa! Baada ya siku chache msala ukaisha kimya kimya na kupandishwa cheo juu!
Hapo ndo niliamini kweli uchawi upo!!!
 
Ukiwa na nafasi utupe mkasa tucheeeke, make uliyoyapitia ni mengi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
We acha tu. Ila ndio hivyo nimeamua kumsujudia mwenye mali na fahari za ulimwengu ili anipe access.. haya mengine ni katika changamoto tu..vibweka na mikasa ya kila aina.
 
Back
Top Bottom