Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Enzi hizo nipo form six tumetoka shule jumamosi kufanya test tukaenda nyumbani kwa rafiki yetu huyo..

Dah..tumefika tu tunakuta maagizo kwa house girl wao eti mama yake ameacha laki 100,000... jamaa akachukue chakula cha paka da nilishtuka sana.. nikamwambia jamaa yaani paka wenu hawa wanabudget nzuri hivyo kuliko watanzania wengi sana kweli maisha hatufanani.... akacheka tu.

Paka wenyewe wawili 2 nikiwaangalia kama wa mitaani tu..wamejilaza kwenye makochi
Hiyo ni mwaka 2014..

Kifupi jamaa hata chuo akwenda hakusubili matokea akasepa zake state hadi leo yupo huko alisoma chuo hukohuko ameoa hukohuko kifupi maisha kwenu yakiwa kwenye hali nzuri kuna uwezekana mkubwa sana watoto pia wakaishi maisha mazuri tu hata wakikuwa.

Yule jamaa napiga nae story hadi leo namkumbusha wale paka anasema walikufa.yeye anawaita na majina kabisa.
Chaiii...
 
Miaka ya 89's nyumbani tulikuaga na Tv, fridge, washing machine,choo Cha kukaa, nyumbani Kuna umeme, mashine ya kunyolewa, jiko la umeme , oven , pressure cooker N.K
Kumiliki ivyo vitu enzi izo yaani mnaonekana matajir wakubwa Sanaa 😊

Maisha yamebadilika Sanaa Sanaa sikuizi hivyo vitu sio big deal tenaa...
hvyo vitu bado ni big deal hadi leo hii mzee uwezi ad leo kuna watu hawana hvyo
 
Miaka kama 10 ilopita nikiwa ndo nimeanza kazi za benk na nipo customer service. Alikuja father mmoja ambaye alikuwa na kiasi kikubwa kwenye account ambacho aliniambia kilitokana na kuuza hisa zake.

sasa katika kupiga piga story za hapa na pale akanieleza kuwa hobby yake kubwa siku za weekend huwa ni kwenda kuendesha zile ndege ndogo ndogo.. Nikajua hapa huyu pesa ipo nyingi

Aliniachiaga na business card na sikuweza mtafuta tena
 
Wee kumbe wa kishua...
Ndo mana ulikua una akili sana class
😂😂😂😂
Mzee wangu alitokea familia ya kimaskini Sana.
Babu alikuaga na ngo'mbe wengi Sanaa
Kimiujiza miujiza miaka ya 60's watoto wa Babu kwa miaka tofauti tofauti walikua wanafaulu darasa la saba na kuchaguliwa shule za SERIKALI

Walisomaga zamani na wakabahatika kupata kazi nzurii serikalini na wote wamekua watumishi mpaka Kustaafu kwao utumishi serikalini.

Kwenye tumbo la mama tupo wa 5 hakuna hata mtoto mmoja ambae Hana degree wa mwisho ndio kamaliza hapo Udsm mwaka huu

NB.
Kuna familia ukizaliwa unakua mwenye bahati na chance kubwa ya kuwa na option mbali mbali za kutimiza ndoto/goals E.t.c
 
Duuuh hiyo inaitwa luck bloodline.. (pedigree)...
Nyie kwenu mna hatali mno hizo akili za upande wa kama au wa baba au wote kwa pamoja
 
Miaka ya 89's nyumbani tulikuaga na Tv, fridge, washing machine,choo Cha kukaa, nyumbani Kuna umeme, mashine ya kunyolewa, jiko la umeme , oven , pressure cooker N.K
Kumiliki ivyo vitu enzi izo yaani mnaonekana matajir wakubwa Sanaa 😊

Maisha yamebadilika Sanaa Sanaa sikuizi hivyo vitu sio big deal tenaa...
sio kweli. sisi wenyewe mzee alikua anaenda zambia hio 80s ilikua colgate na ndara zile subutu ukutwe nazo na serikal .gari alinunua Niva kwa rafiki yake mzungu alikua kigoma UN ndio yule mzungu alikua anaruf kwao akamuuzia friji.heater pressure cooker.even us we had those things
 
Back
Top Bottom