Maisha hatufanani..kabisa nimekuja kuona tena kitu kama hicho kwa boss wangu mmoja mzungu nae anapaka wake nyumbani wanabudget kubwa kama laki 4 kwa mwezi isee mapaka manene hadi kutembea yanashindwa..
paka wananunuliwa hadi toy za kuchezea..
Jamaa akaniambia hawa paka waliokotwa kwenye jaa kwanza hawataki mazoea na rangi nyeusi kabisa wakiwaona wanaondoka na yule mzungu alivyo mweu anasema hataki wageni kwake wanawapa stress paka wake..
Nikacheka sana nikasema hao paka wanajua balaa la jua kali huko nje wamekubali kuwa machawa hapa maisha yaende..mzungu aamini hivyo anaamini wale paka wanapata msongo wa mawazo sababu sisi waafrica tuna watisha na kuwapiga ovyo bila sababu.