Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Wakuu,

Disclaimer🫢 Hapa hatuongelei pesa madafu

Kuna mtu alisema ameenda kwa rafiki yake akakuta wana pump ya mafuta kwao🤣🤣🤣🤣

Yaani mambo za kwenda sheli si habari zao. Wanamaliza tuu hapo nyumbani

Hata mimi ningeshtuka kwa kweli 😀

Wewe ni nini uliona kwa Watu ukajua pesa ipo?
Ndio huku nini ?
1000015587.jpg
 
Nilikua naendesha gari ya mizigo nikapata kazi kupeleka mavyuma fulani hivi mbweni, sikwenda na mtu ila nilipewa namba ya simu nikaambiwa ukifika maeneo fulani piga simu kuna mtu atakufuata.

Mie huyoooo nilipofika eneo la tukio nikapiga simu full kufoka nimeshafika muda mrefu hapa, dk 0 ikaja V8 nyeusi tiiii. Ikaja kuni block kwa pembeni, jamaa akashusha kioo akasema nifuate.

Asee kila kona tunayokunja ni mijengo ya maana, mitaa mizuriii halafu pako kimyaaa, tukafika mpaka nje ya mjengo mmoja geti kuubwa, lile lango likafunguliwa kwa rimoti tukazama ndani.

Asee ile kuingia ndani nikawa nashangaa shangaa tu hata sielewi, lilikua bonge la jumba, swimming za maana halafu juu ya paa kuna parking ya helicopter, mataa ya barabarani yapo ndani.

Kuna jamaa nahisi aliona shauku yangu, akaniambia "zunguka zunguka uone nyumba ya rais wako ili uende ukasimulie na wenzio" nilizunguka kidogo tu ila maeneo mengi yalikua na makatazo kupita.(nyumba ilikua haijaisha ila ilikua inatisha aseee)
Eeeh
 
Hawawezi kutoa kwako mkuu lakini kwa nchi hii daa acha tu
Hupewi kibali kwa ajili ya familia yako, haiwezekani mkuu. Ila kama una shughuli za kibiashara zinazohitaji ulazima wa kuwa na pump yako unapewa.

Halafu, tajiri gani atakubali huo usumbufu na gharama za kurun pump nyumbani kwake kwa ajili yake na mkewe na watoto? Maana ni gharama na usumbufu.
 
Dr am 4 real PhD
Dactar hivi kuna faida ya kunywa maziwa mtindi... Kwa faida ya wote tupe na madhara yake kabisa (sorry nje ya mada)

Kuna mtu hapa anapenda mambo ya jabu ajabu
Namaanisha wewe ERoni
Yana faida kadha wa kadha mkuu ILA YAWE MAZIWA HALISI YA MTINDI NATURAL I.e NG'OMBE

Sio artificial MTINDI kwa uchache nimeelezea 🙂😊
 
Back
Top Bottom