Nilikua naendesha gari ya mizigo nikapata kazi kupeleka mavyuma fulani hivi mbweni, sikwenda na mtu ila nilipewa namba ya simu nikaambiwa ukifika maeneo fulani piga simu kuna mtu atakufuata.
Mie huyoooo nilipofika eneo la tukio nikapiga simu full kufoka nimeshafika muda mrefu hapa, dk 0 ikaja V8 nyeusi tiiii. Ikaja kuni block kwa pembeni, jamaa akashusha kioo akasema nifuate.
Asee kila kona tunayokunja ni mijengo ya maana, mitaa mizuriii halafu pako kimyaaa, tukafika mpaka nje ya mjengo mmoja geti kuubwa, lile lango likafunguliwa kwa rimoti tukazama ndani.
Asee ile kuingia ndani nikawa nashangaa shangaa tu hata sielewi, lilikua bonge la jumba, swimming za maana halafu juu ya paa kuna parking ya helicopter, mataa ya barabarani yapo ndani.
Kuna jamaa nahisi aliona shauku yangu, akaniambia "zunguka zunguka uone nyumba ya rais wako ili uende ukasimulie na wenzio" nilizunguka kidogo tu ila maeneo mengi yalikua na makatazo kupita.(nyumba ilikua haijaisha ila ilikua inatisha aseee)