Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Kutoka ndani ya uvungu wa moyo nakuombea mkuu kikubwa usichague kazi kamwe huwez kupata kazi kama hauna kazi humu humu kwny maofisi tunayoanza nayo ndiyo tunakutana na fursa mpya.

Kikubwa kuwa muadilifu na mchapakazi kuna watu wanakufatilia pasipo wewe kujua hii ndiyo kitu pekee ilonifanya nikawa shifted kutoka nilipokuwa mpaka nilipo, jali na upende unachofanya.
kuchapa kazi najitahidi ili siku ikitokea nafasi niitendee haki. shukrani kwa neno mkuu
 
Kuna watu wana kila kitu nyumbani kwao hasa vya kuonekana lakini nyumba inadaiwa home loans ya mabilion ya shilingi na hawalali kwenye hizo nyumba kwa raha. Wanaishia kuvuta miskakanka na kamari.
Usione ukadhan ndugu
 
Huyo alikudanganya mkuu, kwanza EWURA hawawezi kutoa kibali na pia OSHA hawawezi wakatoa kibali cha kuweka fuel station kwenye makazi ya mtu.
Jidanganye, hao ewura na osha ni kwa maskini lakni sio wenye pesa zaoo.. Nenda nyumbani kwa Abood Morogoro ndio utaona kiwa Ewura wamekufaa
 
Miaka ya 89's nyumbani tulikuaga na Tv, fridge, washing machine,choo Cha kukaa, nyumbani Kuna umeme, mashine ya kunyolewa, jiko la umeme , oven , pressure cooker N.K
Kumiliki ivyo vitu enzi izo yaani mnaonekana matajir wakubwa Sanaa 😊

Maisha yamebadilika Sanaa Sanaa sikuizi hivyo vitu sio big deal tenaa...
Kipindi hicho unaweza miliki hivyo vitu lakini uko kwenye nyumba ya kupanga, kujenga nyumba wkt huo ilikuwa ngumu sana
 
Enzi hizo nipo form six tumetoka shule jumamosi kufanya test tukaenda nyumbani kwa rafiki yetu huyo..

Dah..tumefika tu tunakuta maagizo kwa house girl wao eti mama yake ameacha laki 100,000... jamaa akachukue chakula cha paka da nilishtuka sana.. nikamwambia jamaa yaani paka wenu hawa wanabudget nzuri hivyo kuliko watanzania wengi sana kweli maisha hatufanani.... akacheka tu.

Paka wenyewe wawili 2 nikiwaangalia kama wa mitaani tu..wamejilaza kwenye makochi
Hiyo ni mwaka 2014..

Kifupi jamaa hata chuo akwenda hakusubili matokea akasepa zake state hadi leo yupo huko alisoma chuo hukohuko ameoa hukohuko kifupi maisha kwenu yakiwa kwenye hali nzuri kuna uwezekana mkubwa sana watoto pia wakaishi maisha mazuri tu hata wakikuwa.

Yule jamaa napiga nae story hadi leo namkumbusha wale paka anasema walikufa.yeye anawaita na majina kabisa.
daah nimelia sana😭
 
Back
Top Bottom